Search This Blog

Wednesday, December 12, 2012

EXCLUSIVE: MRISHO NGASSA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI NA KUPEWA MILLIONI 10 - AHAIDIWA NYINGENE MWISHO WA MSIMU

Huku masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea muda ambao msemaji wa klabu ya El Merreikh alioutoa kwa mchezaji Mrisho Ngassa kujitokeza alikojificha na kufanya taratibu za uhamisho wake kwenda Sudan - mapema asubuhi ya leo, kuna taarifa za ndani kabisa kwamba mchezaji huyo ameamua rasmi kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya mitaa ya jangwani.

Chanzo cha habari kilicho karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga ni kwamba Mrisho Ngassa tayari amekubaliana kimsingi na Yanga kwamba atajiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo uliobakisha miezi isiyopungua sita  na klabu ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna Niyonzima.

"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na pre-contract na Yanga ya miaka miwili, kwa sasa hivi amepewa millioni 10 na fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu. Sasa hivi mchezaji amejificha ili kuepeuka usumbufu wa El Merreikh na Simba pamoja na Azam."

Mrisho Ngassa amekuwa katika vichwa vya habari kwa takribani wiki mbili sasa juu ya usajili wake wa kwenda kujiunga na El Merreikh ambao wamemuahidi mshahara wa $4000 kwa mwezi pamoja na $75000 kama ada ya usajili, huku vilabu vyake vya Simba na Azam FC vikilipwa $100,000. 

32 comments:

  1. Sitaki kuamini habari hizi,lakini kama kuna ukweli katika hili Ndugu yetu(Ngassa) kajichimbia kaburi mwenyewe! Hivi wachezaji wetu wanajielewa kweli? Au maisha kwao ni Simba na Yanga tu? Sasa vijana wanaochipukia waige nini kutoka kwa kaka zao waliowatangulia? Upuuzi mtupu! Wanajiaribia maisha yao na soka letu kiujumla! INASIKITISHA SANA!

    ReplyDelete
  2. DOGO ANAJICHANGANA MWENYEWE HUYU AMA KWELI WACHEZAJI WA TANZANIA NA VIONGOZI WA SOKA WA TANZANIA WA SOKA NI VILAZA.....SHAFFIH TANZANIA KUSONGA MBELE KISOKA MPAKA WAFE WALIOPITA ENZI ZA UHURU..

    ReplyDelete
  3. Kama ni kweli,basi wapenda soka tumfanyie maombezi huyu dogo kwani kuna tatizo analo ambalo haliwezi kumtoka bila maombezi,hivi inaingia akili kweli kukataa mkataba wa madolali kibao na kwenda kwenye mikataba yetu ya ubabaishaji au dogo anataka kuendeleza kale kamtindo alikoanza ka kurekodi video zake za ajbu ajabu,maana sudan upuuzi huo hakuna

    ReplyDelete
  4. Ngassaaaaaaaaaaa,karibu nyumbani.najua huko ulikuwa unatembea tu.Welcomu ooh!

    ReplyDelete
  5. SUDAN KITU GANI? PERSONAL WILLINGNESS JUST A MATTER.SIMBA NA AZAM WOTE LAO MOJA WAKIJARIBU KUTENGENEZA FAIDA KIMIZENGWE,NGASA ALITOKA AZMZAM KWA MIZENGWE KWENDA SIMBA NA BAADA YA KUONA MWISHO A MKATABA WAKE UNAKWISHA NA UWEZEKANO WA KUMBAKISHA HAUPO WANATAKA KUPIGA DILI LA MWISHO.KUSEMA NGASA ATAFUNGIA WACHEZAJI WA TZ KUCHEZA SUDAN SIDHAN KAMA HILO LINAMVUTO, KWA SUDAN NI NINI? AU NI WAPI? DOES THE WORLD MEANS SUDAN?.$4000 ZA UGENINI SI KITU BORA HATA ALIPWE $3000 AKIWA NYMBANI MAANA ANAUHAKIKA WA KUFANYIA YA MAANA ZAID.KAMA KUENDELEZA MAISHA YAKE YA SOKA, SOKA LINACHEZWA POPOTE NA LINAKIKOMO HAWEZI ETI KWENDA SUDAN NDIO ATACHEZA HATA AKIWA NA MIAKA 90! ACHENI UVIVU WA KUFIKIRIA

    ReplyDelete
    Replies
    1. GOOD THINKING!!! HATA MIMI NINAWAZA KAMA WEWE SUDANI KITU GANI BWANA MUACHENI APANGE ANAVYOTAKA. IWE SIO MUMLISHE MAWAZO YENU.

      Delete
  6. Kama ni kweli kaka kunajambo ambalo lipo nyuma ya pazia bada ya kutakiwa akapime afya hapo ndipo mtihani ulipojitokeza angeambiwa kujiunga bila vipimo angeenda mwenyewe sudani bila kushurutishwa.wachezaji wengi wa kiafrika afya zao zina utata,mchezaji ukimtajia tu vipimo hata umwambie utalipwa milioni ishilinni kwa mwezi anakimbia jibu tunalo

    ReplyDelete
  7. Ndo kusema Yanga kuna maslahi zaidi ya El-Merreikh?,Nenda kaangalie maisha mbele dogo, Cmba na Yanga ni siasa tu.

    ReplyDelete
  8. habari ya Ngasa kila siku inabadilika kiasi kwamba ni vigumu kujua ukweli ni upi..mwanzo Azama walisema wamemuuza kwa UDS 75,000. jana Simba na Azam watachukua wa pamoja UDS 100,000 (@ 50,000 USD). naona kama kuna ujanja ujanja mwingi kiasi kwamba hata Ngasa mwenyewe wanaweza wakawa wanamchanganya. Bora atulie kama nikwenda Yanga aende ili kwanza ili lipite, awe huru kufanya maamuzi sahihi.

    ReplyDelete
  9. HUYU NGASA KWELI NI WA HAPA HAPA DILI LA LOVHAM NORWAY LILIKWAMA, SEATTLE SOUNDERS USA LILIKWAMA, ELMEREIKH LISHAKWAMA AKUMBUKE MPIRA WA TZ HAUNA FAIDA SANA ZAIDI YA KIKOMBE CHA TENGA HAKUNA JINGINE MEREIKH NI TIMU KUBWA NA INASHIRIKI VIKOMBE VYA AFRIKA KILA MWAKA SIMBA NA JANGWANI HAKUNA KITU AKACHUKUWE USHAURI KWA LUNYAMILA KUHUSU MPIRA WA BONGO

    ReplyDelete
  10. Ngasa ameamua kulipiza kisasi?
    Kwa AZAM na Simba?
    Mi sijui nauliza tuu.

    ReplyDelete
  11. Wachezaji wa kibongo wengi wao wanaogopa challenge wakienda kuchezea timu za nje ya nchi.
    Mojawapo ya challenge hizo ni swala la kupima afya.Wanaogopa sana swala la kupima afya kwa kuwa wengi wao ni wagonjwa.(Just thinking loudly)

    ReplyDelete
  12. Mrisho Ngasa unaaibisha Nchi, Mpira wa Miguu na Watanzania kwa ujumla. Watu wametoka Sudan kuja kufanya Deal mwanzoni ukakubali deal then unabadilika unasema hujui chochote kinachoondelea cha kushangaza zaidi unazima simu na ukiwasha hupokei kweli tunataka mpira wetu ukue kwenye level ya professionism kwa style hii ya kina mrisho ngassa?Kama deal unataka kui cancel kwa nini usikutane na hawa jamaa na kuwaambia hutaki tena kukamilisha deal nao?hv unajua ni wachezaji wangapi utakaowaharibia kwa hili? tutumie akili watanzania hizi siasa zinazoingia kwenye mpira zitakuja kuleta maafa makubwa sana kama hazitatatuliwa mapema

    ReplyDelete
  13. Kama ni kweli amesaini Yanga, basi namwonea huruma Ngasa anavyohangaika. Ni tamaa ya pesa au ni ulimbukeni?. Sielewi Baba yake yuko wapi kumsaidia mwanae kwenye hili suala.Anaacha kwenda El Merreikh na kung'ang'ania kucheza ligi yetu ya madafu?. El Merreikh ni timu kubwa Africa yenye level za TP Mazembe, Al Ahly Zamaleikh na timu kama Keizer Chiefs. Kwa sasa ina tiketi ya kushiriki mashindano ya Africa mwakani. Ni timu ambayo huwa inafikia hatua za juu kwenye mashindano ya Afrika, ambako ndiko hasa timu za ulaya zinakochagua wachezaji.Hiyo Yanga aliyoikimbilia, ndio ile ile aliyoiacha, haina tiketi ya kushiriki ligi ya Africa mwakani, nafasi ambayo ingemwezesha kuonekana na timu kubwa zaidi, yeye anakimbilia kwa ajili ya pesa au kushangiliwa uwanja wa Taifa?. Kwa hatua iliyofikia, hakutakiwa kuendelea Simba, wala kurudi Yanga, wala kwenda Azam. Yeye alitakiwa moja kwa moja aende El Mereikh. Hamwoni mwenzake Tegete hatima inavyomkuta ndani ya Yanga, ataishia kwenda Toto Africa kucheza kwa mkopo. Alirudishwa ulaya ili aje kucheza mechi ya ligi. Leo ananuka ndani ya Yanga. Pole sana Ngassa. Ulaya mchezaji anahama timu kwasababu imekosa tiketi ya kushiriki mashindano ya kimatifa. Huku kwetu ni kinyume!

    ReplyDelete
  14. Wachezaji wa namna hii sijui nani anawashauri, anaacha mshahara wa TZS 6,400,000 kwa mwezi kwa miaka 2 pamoja na signing fee ya TZS 80M na kukimbilia uswahilini! Vilabu vya TZ vinajulikana kwa uswahili sijui Ngasa kama ameangalia mbali au kaangalia miaka 2-5 tu. Alistahili awaangalie wachezi wenzake waliowika miaka hiyo jinsi wanavyoishi sasa nina hakika kama angefikiria maisha yake baada ya kustaafu asingekataa ofa ya El mereikh.

    ReplyDelete
  15. shaffii soka la bongo halitakuja kuendelea

    ReplyDelete
    Replies
    1. ngasa mdogo wangu unaachia dola 75000 kwa milioni kumi wenzako wangapi wanahitaji pesa kama hizo dah nakusikitikia sana , hao yangu ukicheza vibaya kidogo hiyo mitusi yake hebu kumbuka msajigwa kafanyiwa nn yanga na AFC leopard walishamchukua alivyorudi yanga unaona alichokipta na mm mwenyewe nilimshauri Nsa usirudi yanga hona sasa fikiria mara 2

      Delete
  16. shafii ngasa atakuwa anaogopa vipimo vya afya ndo maana amekacha. umri unaotajwa kwenye vyeti ni tofauti na umri halisi wa mchezaj. bongo kuendelea kisoa kazi ipo.

    ReplyDelete
  17. Simlaumu Ngassa,kila kitu huwa ni maandalizi tangu ukiwa haujakomaa,hivi ndivyo ngassa alivyoandaliwa kabla ya kuja kuwa staa,hata timu watu washauri wake sio wazuri,ila nawasifu kwa kweli kwa juhudi walizofanya hadi kukaribia kumbakisha bongo ili waendelee kunufaika zaidi kwa jasho lake..Hili liwe somo na fundisho kwa chipukizi wote,..

    ReplyDelete
  18. Mie nasema hata kama Sudan angeingia mkataba wa 1m(Tzs) angeenda nakuachana na SOKA FITINA. Hakuna lolote hapa ni kuogopa vipimo tu. Nilikuwa nampenda Ngasa kwa sasa hata kumsikia tu sitaki tena.

    ReplyDelete
  19. Huyu dogo asipojiangalia atajipotezea umaarufu wake bure.Tatizo ;la wachezaji wa kibongo hawatulii wakacheza mpira,wanalewa sifa mapema sana.Namshauri asiwe na papara atulie amalize mkataba wake ndo afanye michakato mingine.

    ReplyDelete
  20. hivi ninyi ni nani hadi mmsemee Ngasa, lini Ngasa akawaamulia mambo yenu hadi ninyi mjipe nafasi ya kumwamulia? mnaona pesa ndo kitu cha msingi sana katika maisha kiasi kwamba ndo kiwe kigezo pekee cha kufanyia maamuzi. Eti ooh anawaalibia watanzania...ingekuwa hivyo tusingekuwa na shida watz maana wanaofanya maamuzi wengekuwa wanatufikiria sisi.. Ngasa ni yeye na maisha yake kama ninyi mlivyo na maisha yenu.

    ReplyDelete
  21. Safi sana karibu nyumbani.

    ReplyDelete
  22. Kama maoni au ushauri wadau mmetoa vya kutosha ila ndio vile "unaweza kumswaga ng'ombe kwenda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji"

    TIME WILL TELL!!

    ReplyDelete
  23. Tuache kumhukumu Ngasa, hatujui kitu gani kimetokea. Katika hali ya kawaida, hatutegemei kama Ngasa ameamua kutokwenda Sudan bila sababu ya msingi. Kwanza Tanzania hatuna mamlaka za kusimamia maslahi/haki za wachezaji na mpira wetu bado wa ridhaa. Hivyo magumashi kibao.
    Habari zilipotka kwamba Ngasa anauzwa El Merreikh, Simba na Azam wakaanza kugombea hizo hela kabla hata hazijalipwa. Katika hali ya kawaida hiyo inaashiria nini? Msimu uliopita Yanga walitaka kumrudisha Ngassa kundini baada ya Azam kumtuhumu mambo kibao. Lakini Azam hao hao hawakuwa tayari kuona Ngasa anaenda Yanga, badala yake wakajifanya wamempeleka Simba kwa mkopo. Na tuliambiwa simba wamelipa Tsh 25M. Je, Ngasa aliridhika na hili?? Leo Azam walishakubali kumuuza Ngasa kwa El Mereikh, tunauhakika gani Ngasa aliridhia. Tunajua alikuwa Uganda kwenye Challenge Cup wakati haya mambi yanafanyika, kuna uhakika wowote kuwa alihusishwa? Kama hata Simba ambao wanamtumia Ngasa kwa mkopo hawakupewa taarifa, tunauhakika gani kama Ngasa alishiriki kikamilifu ktk mchakato wa kuuzwa kwake, hasa tukizingatia kwamba alikuwa katika Challenge Cup.
    Kama alikubali kwenda Sudan, alikubali vipi? Kwa mazungumzo ya kwenye simu au kimaandishi? Nani alikuwepo, mwanasheria, muwakilishi wa Ngasa etc.???
    Katika hili kuna maswali mengi kuliko majibu yanayotolewa kishabiki na wadau wengi hapa jamvini. Hata mleta habari hii kaileta kishabiki zaidi, ameifanya ionekane kuwa ya kweli wakati ni tetesi tu. ''Chanzo ni mtu aliyekaribu na Ngasa''. Huu ni udaku!!

    ReplyDelete
  24. Maisha popote, Huko mbele kuna niniiiiiiiiiiii? Ngasssa nakupa big up kwa ulichokifanya.

    Jamani kwani wewe ni chombo hadi uuzwe bila makubaliano? Faida ya Tamaa ya hela za vilabu kwa wachezaji wao ndiyo hiyo. Soka haliendi namna hiyo, wadau tujifunze

    ReplyDelete
  25. Ngassa ni Yanga Daima, Nampongeza sana

    ReplyDelete
  26. Uwezo mdogo wa kufikiri jumlisha elimu ndogo jibu utalipata. Hivi hata mzee Halfan Ngasa (baba yake) naye kashindwa kumshauri cha maana wakati fitina ya soka la bongo anazijua. Bongo mchezaji akicheza kwa muda mrefu miaka 5 isipokuwa wachache sana wanacheza zaidi ya miaka 28 kama madaraka selemani. Yale yale ya Tegete kuacha kumalizia majaribio nje kurudi mbio bongo kuwahi mechi ya simba na yanga matokeo yake mwakani tutacheza naye bonanza leaders akijiita veterani wakati hata miaka 30 hana. Ngasa na washauri wake wote wanatia huruma sana kuanzia majaribio Norway, Marekani, West ham duu dogo atakuja kuliaje miaka 5 ijayo kwani hatamuona mpambe yeyote kati waliomzunguka sasa.

    ReplyDelete
  27. Kwa hili Ngasa amepotoka...ila bado najiuliza hii sinema ni series ya ngapi maana stearling anatuchanganya!!! Au tuseme basi ina EPISODE nyingi?!

    ReplyDelete
  28. JAMANI SOTE HATUJUI SABABU NI NINI NGASA KUKATAA KWENDA SUDANI NADHANI TUNGEFANYA JUHUDI KUJUA SABABU NA SI KULAUMU TU, KAMA PESA NI KILA KITU HEBU WATOENI WAKE ZENU KWA WENYE PESA ILI MTATUE SHIDA ZENU, TAFUTENI SABABU KWA NGASA MWENYEWE.

    ReplyDelete