Search This Blog

Thursday, September 26, 2013

TIMU ZA WIZARA YA HABARI ZAANZA KWA KUTOA VIPIGO SHIMIWI

Wachezaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa wamembeba Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Ole Sante Gabriel kusherehekea ushindi walioupata timu za kuvuta kamba za wizara hiy 
Mshambuliaji wa timu ya mpira wa pete Hadija Jaha akijiandaa kutoa pasi kwa mwenzake wakati walipokutana na timu ya Wizara ya Maji. Wizara ya Habari ilishinda kwa alama 19 kwa 15.

Kiungo wa timu ya mpira wa pete ya Wazara ya Habari Flora Mwakasala akijiandaa kutoa pasi kwa mshambuliaji wa timu hiyo Grace Kinga

Kiungo wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari Mbozi Katala akimtoka beki wa timu ya Wizara ya Maji wakati timu hizo zilipokutana katika mshindano ya SHIMIWI.Habari ilishindwa kwa 1-0.
Wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya Wanawake ya Wizara ya Habari wakiivuta timu ya Afrika Mashariki (haipo pichani) katika mchezo wa mashindano ya SHIMIWI Septemba 22.

Wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya Wanawake ya Wizara ya Habari wakiivuta timu ya Afrika Mashariki (haipo pichani) katika mchezo wa mashindano ya SHIMIWI Septemba 22.

Nahodha wa timu ya soka ya Wizara ya Habari Carlos Mlinda akiongoza wenzake kusalimiana na wachezaji wa timu ya Wizara ya Maji wakati walipokutana katika ya kwanza ya mashindano ya SHIMIWI.

Wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya Wanaume ya Wizara ya Habari wakiivuta timu ya Afrika Mashariki (haipo pichani) katika mchezo wa mashindano ya SHIMIWI Septemba 22.

Kikosi cha mpira wa miguu cha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. 
Kikosi cha mpira wa pete cha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

MAKALA: MRISHO NGASSA KUPEWA PASI ZA MGONGO YANGA?

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                 
NA BARAKA MBOLEMBOLE 
Miaka mitatu iliyopita wakati wa majira ya kiangazi, 2010 kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa aliihama klabu ya Yanga na kutua Azam FC kwa usajili ambao uliwagharimu Azam zaidi ya shillingI za Kitanzania 90 millioni. Ngassa alijiunga Yanga, Juni, 2007 na akatokea kuwa mchezaji kipenzi kwa makocha Dusan Kondic, na baadae Kostadin Papic. Katika siku zake za mwanzo klabuni Yanga, Ngassa hakuweza kupewa nafasi kubwa sana na aliyekuwa kocha wa kikosi hicho, Mserbia, Militun Micho, na ninakumbuka mchezo wake wa kwanza wa kimataifa alicheza kwa dakika zisizozidi 15 na kutolewa. Ilikuwa ni mapema mwezi februari , 2007 wakati Yanga ikicheza na na timu ya Petro Atletico ya nchini Angola.

Kocha, Micho alimpanga Ngassa katika kikosi cha kwanza ila baada ya robo saa kiungo huyo akaoneka kuzidiwa mambo mengi na wachezaji wa Atletico, na wakati wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Taifa, Micho akamuinua Mkenya, Bernad Mwalala na akaisaidia Yanga kutoka nyuma na kushinda mechi kwa mabao 3-2. Akiwa na kipaji cha kuchezea mpira na kuutambuka kama wafanyavyo Cristiano Ronaldo au Robinho De Souza, Ngassa alikuwa akihaha kila kona ya uwanja kutafuta mipira na kuichezesha timu. Aliweza kuwang’arisha wachezaji wa safu ya mashambulizi, kama Maurice Sunguti, Mwalala, Boniface Ambani na wengine ambao waliisadia Yanga kutwaa ubingwa katika misimu ya 2007/ 08 na kufanya tena hivyo katika msimu wa 2008/ 09 na baada ya kumaliza katika nafasi ya pili msimu wa 2009/ 10, kiungo huyo alijiunga na Azam kwa staili ya ‘ kuweka rekodi ya usajili nchini’.

Akicheza pembeni ya uwanja na kuingia katikati ya uwanja kwa kasi akiwa na mpira, kulimfanya Ngassa kuhesabika miongoni wa wachezaji bora wa nafasi ya kiungo wa mashambulizi, mtoaji mzuri wa pasi za mwisho, mpigaji mzuri wa krosi za mwisho akiwa katika spidi, baadae akaibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara, katika msimu wake wa kwanza akiwa na Azam FC. Alifunga mabao 16 katika michezo isiyozidi 25 katika msimu wa 2010/ 11, japo Azam ilimaliza katika nafasi ileile tu waliyokuwa wameishia msimu wa nyuma yake ( nafasi ya tatu), Ngassa kwa upande wake binafsi alikuwa na mafanikio makubwa. Alithibitisha thamani yake kwa vitendo. Alistahili kuwa mchezaji ghali wa ligi kuu ya Bara, wakati huo.

Katika msimu wake wa pili akiwa na timu ya Azam, mshambuliaji John Bocco akashinda tuzo ya mfungaji bora akiwa na mabao 16, huku Ngassa akimudu kufunga zaidi ya mabao sita kwa msimu mzima. Alitumia muda mwingi wa msimu wa 2011/ 12 akimchezesha Bocco na kumsaidia kufunga, lakini hakuwa Yule tena. Kiwango chake kilianza kushuka na akajikuta akipoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu ya Taifa na baadae akapoteza na namba katika klabu yake. Wakati wa michuano ya Kagame Cup, mara nyingi alikuwa akitokea benchi na alipokuja kuibusu jezi ya Yanga wakati wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya timu ya AS Vita, Ngassa akajikuta akivunja mahusiano yake na Azam. Tetesi zikadizi kuwa kiungo huyo alikuwa akiipenda zaidi Yanga na alikuwa akihitaji kurejea katika klabuhiyo ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.

Azam ikamuuza kwa mkopo kwa timu ya Simba, ingawa mchezaji mwenyewe hakuonesha kuvutiwa na maamuzi hayo. Baadae akasaini mkataba rasmi na timu ya Simba na kupewa million 45 na baadhi ya vitu vya thamini huku pia mshahara wake ukiwa wa kiwango kizuri. Msimu huu, Ngassa amesajiliwa na Yanga, huku akiwa na mkataba wa mwaka zaidi na timu ya Simba. TFF, Shirikisho la Soka nchini, lilimuizinisha Ngassa kuwa mchezaji wa Yanga na kuitaka timu hiyo kuilipa Simba, 45 millioni ili kupata huduma ya Ngassa. Pia mchezaji huyo alifungiwa kucheza katika michezo sita ya mwanzo ya msimu huu, na akaambiwa kuwa ataruhusiwa kucheza endapo pesa hiyo italipwa. Mchezo wa mwisho katika kuitumikia adhabu hiyo ulikuwa ni ule wa kichapo kutoka kwa Azm FC, wikiendi iliyopita. Na Yanga wamesema watamtumia kiungo huyo katika mchezo ujao dhidi ya Ruvu Shootings siku ya Jumamosi hii.

NI USAJILI MPYA NA WA GHARAMA 
Ngassa alipoondoka Yanga kwa mara ya kwanza, timu hiyo ilikuwa chini ya mwenyekiti Iman Madega, na uamuzi wake huo wa kujiunga na Azam ulivunja mahusiano kati yake na baadhi ya watu ndani ya Yanga na baadae akaambiwa kuwa ‘ Ni mchezaji wa laki moja’ ambaye hakuwa na thamani yoyote ile kwa Yanga. Nafikiri uamuzi wa Ngassa kusaini Azam ulikuja kama kisasi baada ya timu hiyo kumzuia kujiunga na timu moja ya nchini Norway ambayo ilimtaka kwa ada ya kiasi cha dola za kimarekani laki mbili. Yanga walionekana kuathirika sana katika nafasi hiyo ambayo ndiyo inayowapata ubingwa kwa miaka mingi sasa. Ngassa alijiunga na Yanga kumpokea aliyekuwa winga Said Maulid ‘ SMG’, ambaye alihitisha miaka yake saba ya uchezaji klabuni hapo mwaka 2007 na kutimkia nchini Angola kucheza soka la kulipwa kwa muda wa misimu sita. Kuondoka kwa SMG kulitoa nafasi ya Ngassa kuwa ‘ injini ya timu’ na marta zote alikuwa mchezaji muhimu wakati Yanga ikitwaa m,ataji ya ligi kuu mfululizo.

Ngassa hakuwa na ushindani mkubwa sana wa kugombea namba katika kikosi na hata timu ilipojikuta ikisajili wachezaji 11 wa kigeni wakati Fulani timu ikiwa chini ya Kondic bado kiungo huyo aliendelea kuchomoza katika kikosi cha kwanza. Alipokwenda Azam akajikuta akirundikiwa rundo la wachezaji wa nafasi yake nap engine kuinuka kiuchezaji kwa Hamis Mcha kulipoteza Ngassa. Wakati Ngassa akiwa ametumia misimu mitatu nje ya Yanga, akizurura katika klabu za Azam na Simba, HAKUWAHI kushinda taji lolote lile zaidi yua tuzo ya ufungaji bora. Kwa muda wote huo Yanga imetwaa ubingwa mara mbili na Yanga imefanikiwa kushinda mataji mawili, 2010/ 11 na msimu uliopita. Saimo Msuva ametokea kuwa mchezaji bora wa kiungo wa pembeni hasa baada ya kufanya mambo maklubwa msimu ulipita.

Kuna tofauti katika uchezaji wa Msuva na Ngassa, wakati wote wakiwa na uwezo mdogo wa kuzuia, wanaweza kuwa na kasi sawa nap engine Msuva akawa juu kidogo ya Ngasaa kwa kuwa Ngassa amekuwa akicheza ‘ kifadha’ katika miaka miwili iliyopita. Msuva ni kijana hasa kama ilivyo kwa Ngassa ila Msuva anaonekana kuwa na uchu zaidi wa mafanikio kuliko kiungo mwenzake huyo ambaye alianza kucheza ligi kuu mwaka 2006. Inasemekana kuna jengwe kutoka ndani ya wachezaji wenyewe wa Yanga, hawapendi kuona namna Ngassa anavyothaminiwa kupewa kitita kikubwa. Wakati soka letu likipigiwa kelele kuingia katika mfumo wa kulipwa sifikirii kama kuna haja ya mchezaji kuchukia au kumuonea wivu mchezaji mwenzake kwa kuwa tu analipwa kiasi kikubwa cha pesa. Mshahara wa Felix Sunzu ulikuwa ni tatizo kubwa kwa klabu. Kuna wachezaji ambao waluiona million 5.5 alizokuwa akilipwa kwa mwezi ni nyingi sana na hakutakiwa kuwa analipwa kiasi hicho kutokana na huduma aliyokuwa akiitoa uwanjani. Mkataba ni makubaliano ya pande mbili, hivyo mimi sioni tatizo kama kunakuwa na wachezaji wanatumia majina na uwezo wao kuchuma vitita vikubwa vya pesa.

Sitapenda kuona Ngassa akipigiwa pasi za ‘ mgongo’ na wachezaji wenzake wa Yanga, sitapenda kuona vita ya kurushia maneno kutoka kwa baadhi ya wachezaji wenyewe kwa wenyewe kwani hiyo ni tabia mbaya. Kila mtu atakula kutokana na urefu wa kamba yake mwenyewe. Msimchukie Ngassa kwa kuingiza kiasi kikubwa cha pesa, shirikianeni kuipaisha klabu yenu. Ngassa, Msuva, Said Bahanunzi, hawa watauana katika winga ya kulia, kushoto yupo ‘ pass master’ Haruna Niyonzima. Jamani msimpigie Ngassa pasi za mgongoni msaidieni na atawaidieni pia. Hata naye aliwahi kuitwa ' mchezaji wa bei rahisi' 0714 08 43 08

Wednesday, September 25, 2013

MOYES: KIPIGO KAMA CHA MAN CITY KINAWEZA KUIRUDIA - TIMU IPO KATIKA MAPITO"

Kocha wa Manchester United David Moyes amewaonya mashabiki wa mabingwa wa ligi kuu ya England kwamba anahitaji kuimarisha kikosi chake na kwamba kipigo cha Jumapili ambapo walichapwa 4-1 na Manchester City huenda isiwe ndio mwisho wa matokeo kama hayo.
"Kutatokea siku kama ile ya Jumapili na huenda tukakabiliwa na matokeo zaidi kama hayo kwa sababu tuko katika kipindi cha mpito," aliwaaambia waandishi habari kabla ya pambano la Jumaatano la kombe la Capital One dhidi ya Liverpool.

"Tulihitaji wachezaji wawili watatu hivi ambao wangeweza kuingia moja kwa moja katika timu. Lakini hayo yatatokea, kweli huenda itabidi nikabiliane na vipigo vichache zaidi. Bado tunakabiliwa na kazi pevu ya kuwasajili wachezaji sio tu watakaojumuishwa na kikosi chetu lakini wenye uwezo wa kuingia moja kwa moja katika timu," aliongeza kusema Moyes katika msimu wake wa kwanza katyika a Old Trafford baada ya kushikikilia nafasi iliyoachwa na Alex Ferguson.
Manchester United iliwakosa wachezaji kadhaa mastaa wakati wa kipindi kilichopita cha usajili na hata kulikua na tetesi za juhudi za dakika ya mwisho za kuipiku Real Madrid ili kumsajili Gareth Bale ambae kuuzwa kwake kutoka Tottenham Hotspur kulivunja rekodi kama mchezaji ghali kupita wote duniani.
Juhudi za kuwasajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona, Ander Herrera kutoka Athletic Bilbao na Fabio Coentrao kutoka Real Madrid ziliambulia patupu.
Leighton Baines aliamua kubaki Everton wakati Thiago Alcantara aliamua kuihama Barcelona na kujiunga na Bayern Munich.
Moyes badala yake alikimbilia kumsajili mchezaji wa kiungo wa Ubelgiji Marouane Fellaini, kutoka klabu yake ya zamani Everton, kwa dola millioni ($43.96 ) dakika chache tu kabla ya kufungwa dirisha la usajili.

WACHEZAJI NDIO CHANZO CHA DI CANIO KUFUKUZWA SUNDERLAND


Inaaminika wachezaji wa Sunderland walilalamika kwa mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Margaret Byrne kuhusu kocha Paolo Di Canio kabla ya kupigwa kalamu.

Di Canio aliitisha mkutano wa timu nzima siku ya Jumapili ambao inasemekana ulikumbwa na majibizano makali kufuatia timu hiyo kushindwa mabao 3-0 na West Bromwich Albion.

Baadae wachezaji waandamizi walimwambia Byrne kwamba hali imekua isioweza kuvumilika kwa sababu ya tuhuma kali na matusi ya Mtaliana huyo dhidi ya kikosi cha timu hiyo.

Kikosi hicho ambacho hujulikana kama 'The Black Cats' wameambulia pointi moja tu kutoka mechi tano za ligi ya Premier League katika msimu huu.

Aliyekua kocha wa Chelsea na West Brom Roberto Di Matteo ndiye anayetabiriwa na wengi kuteuliwa kuwa kocha mpya na wengine wanaotajwa ni Gus Poyet, Tony Pulis na Alex McLeish.

Kocha msaidizi Kevin Ball ameteuliwa kuwa kaimu kocha kwa hivi sasa.

Di Canio ameshinda mechi 3 tu kati ya 13 baada ya kufukuzwa kwa Martin O'Neill mnamo mwezi wa Machi.

Tuesday, September 24, 2013

MAONI YA SHABIKI WA MAN UNITED: MOYES ASIRUDIE MAKOSA AU TUJIANDAE NA AIBU YA KUKOSA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU UJAO

Nilinyanyuka kwenye kochi la nyumbani kwangu nikiwa mzito na kwenda kulala moja kwa moja ikiwa ni mapema sana kuliko kawaida yangu. Hii ilikuwa baada ya kuangalia timu yangu niipendayo ikadhalilishwa katika dimba la Etihad usiku wa jumapili ya wiki iliyopita. Nilijiuliza swali moja tu hivi ni kweli hata kuna ushindani mkubwa msimu huu kama inavyosemekana baina ya vilabu viwili vya jiji la Manchester.

Vilabu vyote viwili vinajinasibu kwamba vipo katika muda wa mapito baada ya kubadilisha makocha, lakini ushindi wa 4-1 wa City dhidi ya majirani zao ulionyesha utofauti mkubwa uliopo baina ya vikosi vya klabu hizi mbili.

City wana ukamilifu kwenye idara, ubora wa ufundi, na matamanio ya dhati ya kurudisha ubingwa wa Premier League chini ya kocha mwenye ufundi mkubwa hasa kwenye mechi kubwa kama hizi. 


MSIMAMO WA PREMIER LEAGUE 
TIMU

1. Arsenal
2. Tottenham
3. Man City
4. Chelsea
......................
5. Liverpool
6. Everton
7. Southampton
8. Man Utd

MECHI
5
5
5
5
........
5
5
5
5

GD

5
4
8
4
........
2
2
1
1
Points

12
12
10
10
........
10
9
8
7
Katika michezo mitano ya ligi ambayo tayari Man United tumeshacheza, inaonekana wazi inabidi tubadilike sana au tusihau kuhusu ubingwa na kuweka kipaumbele katika kumaliza ndani ya TOP 4.

David Moyes alipewa ratiba ngumu - na hata akalalamika kuhusu ratiba hiyo ngumu - lakini mscotish huyu amepata pointi moja tu katika michezo yote mitatu tuliyocheza na timu kubwa zenye upinzani nasi katika ligi na kikosi chake kimecheza kwa kiwango cha kuridhisha kwenye mchezo mmoja tu wa ligi. 


Ukiachana na mchezo wa kufungua ligi dhidi ya Swansea, United tumekuwa tukionekana kukosa ubora wa pamoja kama timu, huku safu yetu ya ulinzi ikiyumba hasa kwa viwango vya wachezaji wetu wenye umri mkubwa kiasi kama Rio Ferdinand na Patrice Evra.

Ujio wa Marouane Fellaini katika siku ya mwisho ya usajili ulikuwa muhimu sana, lakini United bado wana tatizo sana katika safu ya kiungo - hawana uimara wa kuweza kufananisha na safu ya kiungo cha Chelsea, City, Tottenham, na sasa hata Arsenal wanaoringia ujio wa 'The Master of Assists' Mesut Ozil na mkabaji Matheiu Flamini.

Kitu kingine cha kuhuzunisha ni upangaji wa kikosi wa kocha, inaonekana bado anafanya majaribio wakati wapinzani wetu wengine wanaogombea TOP 4 wakiwa wameanza vizuri ligi, pamoja na kwamba wamebadilisha makocha na wengine hata wakiwa wameuza wachezaji mategemeo katika msimu uliopita.

United sasa kwa bahati nzuri tuna mechi ambazo angalau unaweza kuziita nyepesi mpaka pale tutakapokutana na 'The inform Gunners'  Arsenal November 10. Lakini angalau hizi mechi na timu ndogo tusifanye makosa au Moyes ajiandae kutuletea aibu ya kukosa ubingwa na kukosa hata kushiriki Champions League msimu unaokuja.

TAMBWE AMIS, NA MABAO MENGINE 78 KATIKA MICHEZO KATIKA MECHI 35, - STEPHEN KESHI KUCHUKUA MIKOBA YA STEWART HALL AZAM??

Na Baraka Mbolembole 
Uliona namna Yanga ilivyouliwa na Azam FC? Uliona mabao ya kuvutia katika mchezo wa Simba na Mbeya City? Umesikia matokeo ya timu ya Rhino Rangers? Umemuona Hamis Tambwe? Na vipi kuhusu kipaji cha ufungaji cha Didier Kavumbagu? Tunahitaji nini zaidi ya mbinu za makocha na uaminifu wa wachezaji na viongozi kwa makocha wao?

Mabao manne yaliyofungwa na mshambuliaji, Hamis Tambwe yanaweza kuwa ' topiki' baada ya kupita miaka miwili pasipo kufungwa kwa ' hat-trick' katika ligi kuu Tanzania Bara, raia huyo wa Burundi alifunga wakati timu yake ya Simba, ikiifunga timu ya Mgambo JKT, mabao 6-0 na akafunga tena mara mbili katika sare ya 2-2 siku ya jumamosi

Raundi ya tano ya ligi kuu ilimalizika wikiendi iliyopita, na kutoa mabao 18 katika michezo 35 ambayo imeshapigwa hadi sasa. Mechi baina ya Azam FC na Yanga, ndiyo Iiyotoa mabao mengi zaidi ( matano) katika mechi za raundi hiyo, ambayo ilishuhudia pia vinara Simba SC wakivutwa shati katika uwanja wa Taifa na Mbeya City, sarte iliyozalisha mabao manne ya ‘ video’ kutoka kwa washambuliaji Hamis Tambe ( Simba), Paul Nongwa na Richard Peter ( City).

Ligi imekuwa ngumu kweli kweli, na uwepo wa udhamini wa ziada ya AZAM TV, na fursa ya kujiongezea wadhamini kwa kadri timu zinavyoweza kuwashawishi wawekezaji, kumeendelea kutoa mwanga kidogo kuwa huenda msimu huu ukawa ni moja ya misimu bora kwa baadhi ya timu nap engine kutoa ‘ bingwa wa ukweli’. Sijui ni kitu gani kitakachotokea upande wa Yanga endapo watajikuta katika wakati mgumu tena siku ya jumatano hii watakapocheza na Ruvu Shootings katika mchezo wa raundi ya sita, kama watapoteza kwa mara nyingine pointi itakuwa ni jambo zuri kwa Shootings, ambayo imekuwa ni moja kati ya timu zenye safu nzuri ya ulinzi.

KIMWAGA AMUOKOA KOCHA STEWART HALL 
Kinda wa Azam, Joseph Kamwaga aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Brian Omony aliweza kuchomoza katika soka la Tanzania baada ya kutumia vizuri pasi aliyopewa kwa mtindo wa ‘ counter attack’’ na kisha kuwapita walinzi, Kelvin Yondan na Mbuyu Twite na kuwapa ushindi wa kwanza timu yake katika michezo mitano iliyopita.
 Kabla ya mchezo huo, wachezaji wa Azam waliahidi mbele ya uongozi wao wa juu kuwa wataifunga Yanga, lakini kocha Stewart Hall ambaye alitoa machozi baada ya kumalizika kwa mchezo huo anaweza kuitwa ‘shujaa aliyekuwa ametengwa’. Baadhi ya wachezaji muhimu wa Azam waliondolewa katika kikosi cha kwanza na wapo ambao hawakujumuishwa kabisa katika mchezo huo. 
Na yote hiyo ilikuja baada ya Stewart kuhisi hawapo tayari kutetea kibarua chake kwa kuisadia timu kupata ushindi. Habari ambazo nimezipata ni kwamba Stewart, ‘hawivi chungu kimoja’ na baadhi ya viongozi wa juu wa klabu. Hivyo anaandaliwa matokeo ya kufukuzwa, wakati Nigeria itakapokuwa ikicheza na Ethiopia katika michezo ya kuzufu kwa fainali za kombe la dunia, baadae mwezi ujao na kufuzu pengine ndiyo Stewart atatulia, ila endapo Nigeria itatolewa basi hatakuwa na kibarua. Azam si wana pesa bwanaa., Stephen Keshi alikuwa atue klabuni hapo mara baada ya Boris Bunjak kutimuliwa oktoba mwaka jana, akatoa masharti ya kuja na msaidizi wake, Azam wakamwambia atasaidiana na Kally Ongalla, dili likafa na Keshi akatwaa taji la mataifa ya Afrika, mapema mwaka huu akiwa kocha wa Nigeria.

Azam wanahisi tayari wanahitaji kitu kikubwa zaidi ya nafasi wanayoipata, kumaliza nafasi ya pili mara mbili mfululizo, kumaliza nafasi ya tatu mara mbili mfululizo, baada ya kunusurika kushuka daraja katika msimu wao wa kwanza, Azam wanajiona wapo tayari kuwa mabingwa wa ligi kuu mbele ya timu za Simba na Yanga. Wakati mwingine pesa inaweza kununua kila kitu, lakini ushindi wa mataji hauji kirahisi. Ni kweli baada ya misimu sita tangu Azam ianzishwe wanastahili kutwaa ubingwa mbele ya Simba au Yanga?. Wapo katika mwendo mzuri na navyofahamu mimi lengo la awali la mmiliki ni baada ya miaka kumi ya kujijenga ndiyo wanaweza kutwaa ubingwa. Lakini wanataka kusimamisha saa, ila wanasahau kuwa muda hausimami daima.

Tayari timu hiyo imenolewa na makocha, Neidor Dos Santos, Itamor Amourin, Bunjak, na sasa Stewart achana na wale wazawa kama Habib Kondo, Silvester Marshi, huku Stewart aliondolewa na kurudishwa tena baadae. Ni idadi kubwa sana ya makocha kwa timu kama Azam, ndani ya miaka sita kuwa na mipango ya makocha wengi hivyo bila shaka kuna lengo la ziada ambalo Azam wanalo na si lile la kujiimarisha kwanza huku wakitoa changamoto ya kuwania mataji na Simba na Yanga, na kama ikitokea kutwaa ubingwa hilo liwe jambo lisilotarajiwa. Pesa wanayo, na pengine ndiyo sababu ya yote hayo, kutokea, pengine wanaweza kuwa tayari wamewatumia zaidi ya wachezaji 40- 50 wa kigeni tangu kuanzishwa kwake na hakuna aliyemaliza mkataba wake zaidi ya Ibrahim Shikanda ambaye amekuwa mmoja wa makocha wasaidizi klabuni hapo kwa sasa. 

Ila bado wachezaji Fulani Fulani wa Kitanzania wamebaki kuwa muhimu zaidi, ukichunguza wachezaji kama John Bocco, Salum Abubakary, Himid Mao, Wazir Salum, kipa Aishi Mwinula, wamekuwa wakifanya vizuri muda wote ni msingi wa timu yao na pengine ni kutokana na uaminifu wa vijana hao kwa walimu wao waliopita na waliyenaye sasa umekuwa ukiwapatia mafanikio, na, kuisadia timu yao.

Kwa soka la Tanzania hata kama mchezaji ataanza kucheza ligi kuu ya Tanzania akiwa na miaka 17 baada ya misimu mitatu anaitwa ‘ Mzee’, Salum anacheza msimu wake wa sita wa ligi kuu akiwa katika kikosi cha kwanza cha Azam, Himid baada ya kumaliza masomo mwaka uliopita naye amejikita katika kikosi cha kwanza kwa sasa, Bocco ‘hagusiki’ kikosini mwao, na wakati nyota hawa wakikua kiumri na kimchezo, wakiimarika kimbinu na kiufundi baada ya kupata bahati ya kufundishwa na walimu wa kigeni tangu wakiwa yosso, Azam wenyewe waaingia katika mipango ya kuivuruga timu. Kuna kundi makundi, kwa muda sasa wachezaji wamekuwa wakimkubali Stewart, na uongozi umekuwa ukimuona Muingereza huyo si mtu wa kuwafikisha wanakotaka kufika.

Chozi la Stewart katika uwanja wa Taifa baada ya kinda, Kimagwa kufunga bao la kushtukiza, lilikuwa na maana kwamba kuna wachezaji wamemsaliti, ni kwa mtazamo wangu zaidi lakini naweza kuwa sahihi na wengine pia. Kuna wachezaji wameingia katika ‘ mkumbo’ wa baadhi ya viongozi kwa kumsariti Stewart ili timu ifungwe, kisha afukuzwe. Nao wanaoneka kukubali hilo kwa kuwa keshi ndiye anaweza kuwa mbvadala wa Stewart. Sijui kwa nini ila wakati, ligi kuu yetu ikizalisha soka safi, timu zenye ushindani, makocha wenye mbinu nzuri, pengine tunahitaji udhamini wa lazima, ‘Uaminifu katika kila idara ndani ya klabu’ Bado tunahitaji kuona Simba na Yanga zikifungwa, Simba na Yanga zikiruhusu mabao ya kulazimishwa, tunahitaji kuona zaidi uwepo wa timu katika kujilinda na kushambulia, kuona ‘hat- trick’ zaidi kutoka kwa Tambwe, na kuona Yanga wakishika tena katika eneo lao na timu pinzani kupewa penati. Mohammed Kampira,

Hemed Morocco, Mbwana Makatta, Juma Mwambusi, Jackson Mayanja, Mecky Mexime, Charles Mkwasa, Jumanne Chale, na wengineo TUKIWATEGEMEA kutuletea nyota wengine wapya katika soka la Tanzania. Nasikia Yusuph Manji, aliocheza kale ka mchezo ketu….. Aaah, eti Manji alebeti Yanga inafungwa…. Yanga wakifungwa mji unatulia, kama United tu, wapenzi wa soka Dar walikuwa na wikendi mbovu. Liverpool, Simba, Yanga , Manchester United waliharibu . Mechi, 35, Mabao 78, Tamwe kinara wa mabao, tayari tunayo ‘ hat’ trick’, mabeki fungeni viatu. 0714 08 43 08

Monday, September 23, 2013

FIESTA SHINYANGA NOMA SANAAAAA!

 Anajiita Mzee wa Mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake kwa shangwe huku mayowe yakitawala kila kona ya uwanja wa Kambarage usiku huu ndani wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea kurindima usiku huu.
 Mtoto wa Mama Said a.k.a Chege akiimba kwa hisia jukwaani.
Msanii wa Bongofleva Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake.
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoko akiimba jukwaani usiku huu sambamba na madensa wake (hawapo pichani). 
Tamasha la Serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku huu.

Mashabiki wake wanamuita Kinga Zilla kutoka Sala Sala,lakini pia jina la Godzilla limemuongeza umaarufu kwa mashabiki wake kutokana na umahiri wake wa kushusha mistari ya hip hop mikavu mikavu,kama aonekavyo jukwaani akiwaimbisha mashabiki wake ndani ya uwanja wa Kambarage usiku huu.
  Baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga,ambapo tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kufanyika.
Mwanadada Linah akiimba sambamba na shabiki wake jukwaani usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea ndani ya uwanja wa Kambarage,mkoani Shinyanga usiku.
 Baadhi ya Wadau wakubwa na wadhamini wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2013,kutoka kampuni ya Serengeti Breweries,Octavian,Bahati pamoja na mdau wao,wakiwa katika picha ya pozi usiku huu ndani ya uwanja wa Kambarage,mkoani Shinyanga
 Mwanadada ambaye kwa sasa ameonekana akifanya vyema kwenye jukwaa la Serengeti fiesta 2013,Neylee akiwaimbisha mashaniki wake (hawapo pichani). 
 Anajiita Jita Man kutoka jijini Mwanza akitumbuiza jukwaani usiku huu.

Dj Zero kutoka Clouds FM akiburuza mangoma usiku huu.
 Mwanadada Shilole na madensa wake wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Kambarage.mkoani Shinyanga. 
 Masbabiki kibao waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,usiku wakifuatilia na kushangweka vilivyo mbele ya jukwaa la fiesta.
 mashabiki wakifuatilia
 Kutoka Wanaume TMK,wakiongozwa Mh Temba na Chege kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa kambarage mjini Shinyanga.
 Weusi wakitumbuiza jukwaani usiku huu.
 Shabiki akifurahi jamboo.
Kundi la Wanaume TMK-Halisi likiongozwa na Sir Juma Nature wakilishambulia jukwaa la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Kambaraje,mjini Shinyanga.



PAMBANO LA AZAM, YANGA LAINGIZA MIL 138/-


Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Azam na Yanga lililochezwa jana (Septemba 22 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 138,188,000.

Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 33 la VPL msimu wa 2013/2014 lililomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 walikuwa 24,020.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 33,065,409.1 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 21,079,525.42.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 16,812,919.89, tiketi sh. 5,022,342, gharama za mechi sh. 10,087,751.93, Kamati ya Ligi sh. 10,087,751.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,043,875.97 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,923,014.64.

Mechi iliyopita ya VPL kwenye uwanja huo kati ya Simba na Mbeya City iliingiza sh. 123,971,000.

MECHI YA TOTO, POLISI DOM KUPIGWA J2
Mechi namba 12 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Toto Africans na Polisi Dodoma iliyokuwa ichezwe Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza imesogezwa mbele kwa siku moja.

Timu hizo za kundi C sasa zitapambana Jumapili (Septemba 29 mwaka huu) kwenye uwanja huo huo ili kupisha mechi namba 10 kati ya Pamba na Stand United FC ya Shinyanga itakayochezwa Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu).

Mechi nyingine za kundi hilo zitakazochezwa Jumamosi ni Mwadui na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) wakati Kanembwa JKT na Polisi Mara zitacheza kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

SEMINA YA KAMATA FURSA ILIVYOFANA SHINYANGA

 
 Mbuge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Wa Nishati na Madini,Mh Steven Masele akizungumza na sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Mh Steven amewataka vijana wa Shinyanga kuwa na moyo wa kujituma na kuzifanyia kazi ipasavyo fursa wanazokumbana nazo bila kukata tamaa,ameeleza kuwa hivu karibuni mkoa huo,unatarajia kufungua viwanda kadhaa,ambapo anaamini kuanzia fursa ya kupata ajira kwa vijana itaongezeka.
 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Maxmalipo,Bernard Munubi akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twendzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.
 sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center. 
 Mkurugezi  wa Vipindi na Uzalishaji Kutoka Clouds Media Groug,Ruge Mutahaba akizungumza sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Ruge pia amefunga semina hiyo ya fursa kwa vijana mapema loe mchana,ambayo imekuwa ikiandaliwa na kampuni ya Clouds Media,Semina hiyo imefanyika  ndani ya mikoa takribani zadi ya kumi  ikiwemo   Kigoma,Singida,Tabora,Mtwara,Morogoro,Dodoma,Mbeya,Iringa,Bukoba na sasa ndani ya mkoa wa Shinyanga.

 sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.  
 Wengine tena ndio hivyo teena,fursaaa fursaaaaa. 
 Sehemu ya meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.
 Wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini.

 Mtangazaji wa Clouds FM,Shaffih Dauda akitoa mada ya fursa ndani ya michezo na changamoto zake,lakini pia namna ya kukabiliana nazo kiasi hata kupata mafanikio kwa namna moja ama nyingine,
Mwakalilishi kutoka TPSF,Jane Gonsalves akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twendzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali ya ujasiliamali kwa vijana ikiwa ni sehemu pia kujiongezea kipato,semina hiyo imefanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center. 

Baadhi wakazi wa mkoa wa Shinnyanga wakifuatila mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,semina hiyo imefanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Picha na Michuzijr wa MICHUZI MEDIA GROUP-SHINYANGA.

VIDEO: HATIMAYE MARIO BALOTELLI AKOSA PENATI - PEPE REINA NDIO KIBOKO YAKE


Baloreina by sr54r

VIDEO: OZIL NA RAMSEY WAZIDI KUING'ARISHA ARSENAL - GUNNERS WAKISHINDA 3-1 DHIDI YA STOKE CITY

VIDEO: MAN CITY YAIDHALILISHA MAN UNITED KWA KUICHABANGA 4-1

Sunday, September 22, 2013

LIVE SCORE: YANGA SC 2 - 3 AZAM - FULL TIME




FULL TIME AZAM 3-2 YANGA

DK 90: Gooo Joseph Kimwaga anaipatia Azam bao la 3.

DK 80: Timu zinashambuliana kwa zamu

DK 69 Kipre Tchetche anapiga penati na kuisawazishia Azam.

DK 68 Azam wanapata penati baada ya Kelvin Yondan kuunawa mpira.

Dakika ya 66, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili

Azam FC 1 - 2 Young Africans
Dakika ya 60, Azam FC 1 - 1 Young AfricansAnaingia Hamis Kiiza kuchukua nafasi ya Jerson Tegete


DK 50: Didier Kavumbagu anaisawazishia Yanga

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Azam FC 1 - 0 Young Africans

Dk 45 HALF TIME! Azam 1-0 Yanga

Dk 43 Mbuyu Twite anapiga shuti kali kuelekea lango la Azam lakini mpira unagonga mwamba na kutoka nje.

Dk 41 Kipre Balou anamchezea rafu Simon Msuva wa Yanga.

Dk 37 YELLOW CARD: Jockins Atudo wa Azam anaonyeshwa kadi ya njano kwa kuchelewa kupiga mpira uliokufa.


Dk 35 Tegete anakosa bao akiwa peke yake katika lango la Azam

DK 30: Azam FC 1 - 0 Yanga

DK Yanga wanakosa bao la wazi baada ya mpira uliopigwa na Kavumbagu kugonga mwamba.

Dk 5 Azam inalishambulia zaidi lango la Yanga.

Dk 1 GOOO...! Azam inapata bao la kwanza mfungaji John Bocco. AZAM 1-0 YANGA

Mpira umeanza hapa uwanja wa Taifa

Azam line up: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Waziri Salum, David Mwantika, Jockins Atudo, Himid Mao, Farid Musa, Kipre Balou, John Bocco, Humphrey Mieno na Brian Umony


Yanga:  Ali Mustapha, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Athuman Idd, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Jerry Tegete na  Haruna Niyonzima

AZAM FC VS YANGA: WACHEZAJI WAKIRI KUVURUNDA NA WAAHIDI USHINDI LEO DHIDI YA YANGA


Wachezaji wa Azam FC kwa pamoja wameahidi ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa, Azam FC ikiwa nyumbani.

Ahadi hiyo ilitolewa na wachezaji mbele ya viongozi wao (Makocha Kaly Ongala na Ibrahim Shikanda, Mwenye kiti Said Muhammad, Katibu Mkuu Nassor Idrissa na Mratibu wa timu hiyo Patrick Kahemele) kwenye kikao cha pamoja kati ya wachezaji na viongozi kutathmini mwenendo wa timu hiyo baada ya mechi nne za mwanzo za ligi kuu.

Wachezaji wa Azam FC wakiongozwa na John Bocco, Jabir Aziz na Salum Abubakar, walisema matokeo ya sare nyingi walizopata katika mechi zilizopita hayatokani na matatizo ya huduma isipokuwa ni mitihani ya kawaida kwenye soka ambapo timu inaweza kucheza vizuri nab ado ikashindwa kupata matokeo. Wachezaji wameahidi kuongeza nguvu kwa kuanzia mechi ya leo ili kupata matokeo ya ushindi badala ya sare.

Wachezaji kwa pamoja walionesha masikitiko yao kwa matokeo yaliyopita na kuahidi kuongeza kujituma kwenye mazoezi na mechi ili kurudisha makali yaliyoifanya Azam FC kuwa timu ya kuogopwa.

Azam FC itashuka uwanjani leo kukwaana na Yanga SC ambapo katika mechi nne zilizopita Azam FC imeambulia kipigo toka kwa Yanga. Lakini timu zote mbili zinashuka uwanjani zikiwa na matokeo ya kufanana na idadi sawa ya pointi baada ya kucheza michezo minne kila moja, kusinda mmoja na kutoka sare michezo mitatu hivyo kuwa na pointi sita.

Azam FC leo itamkosa Agrey Morris Ambrose ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita dhidi ya Ashanti United na nafasi yake itajazwa na David Mwantika.

SOURCE: AZAM FC WEBSITE

MAKALA: VITA YA FELLAINI DHID YA YAYA TOURE ITACHANGIA SANA MATOKEO YA MWISHO YA MANCHESTER DERBY LEO HII


Mbio za usajili wa kiungo wa kati katika klabu ya Manchester United zilileta vituko na maneneo mengi sana katika dirisha la 

Cesc Fabregas alikuwa chaguo la kwanza lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo ilivyoonekana wazi asingeweza kuondoka Barca. Kiungo wa Athletic Bilbao Ander Herrera alikuwa kiungo mwingine aliyetakiwa kama ilivyokuwa kwa Luka Modric. Na wakati Arsene Wenger akivunja kibubu na kulipa kiasi cha £42.5million kwa ajili ya Mezut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili, David Moyes akarudi kwenye klabu yake ya zamani na kumsajili mchezaji wa Everton Marouane Fellaini kwa ada ya uhamisho wa £27.5m – usajili ambao umemfanya mchezaji wa zamani wa United Teddy Sheringham kusema kwamba klabu yake ya zamani imemsajili mtu asiye sahihi. 

Wakati ikiwa bado mapema sana, kiwango cha United katika mchezo wa Champions League dhidi ya Bayer Leverkusen, ambao  Fellaini alianza, unaonyesha kwamba Moyes alimpata mchezaji ambaye alikuwa anatakiwa na kuliliwa sana Old Trafford.

Mchezaji ambaye hatofautiani sana na kiungo wa Manchester City Yaya Toure. Na Moyes akiwa anajiandaa na derby yake ya kwanza leo hii, upande mwekundu wa jiji la Manchester unaweza ukawa umempata mtu sahihi waliyekuwa wakimhitaji kwenye kiungo ambaye anaongeza uimara wa safu ya kiungo kama ilivyo kwa Yaya Toure kwa City.

Ni kweli, Fellaini anaweza akawa hana kipaji cha Ozil au jicho la pasi nzuri kama Fabregas, lakini mbelgiji huyu ameongeza kitu kikubwa katika safu ya kiungo ya United, dhidi ya Bayer wachezaji kama Robin van Persie, Wayne Rooney, Antonio Valencia na Shinji Kagawa, walipata uhuru mkubwa wa kucheza wakiwa na ulinzi mzuri wa Fellaini na ndio maana waliweza kuleta madhara makubwa kwa wapinzani wao. 

Kitu kama hicho ndicho Toure anachokifanikisha kwa timu ya City - kuwafanya washambuliaji wacheze kwa uhuru chini ya ulinzi wake.
Kama ilivyoonekana katika ya Crystal Palace na Bayer Leverkusen - Moyes atakuwa akimtumia zaidi Fellaini katika kiungo cha kuziua pembeni ya Micheal Carrick. 
Kule City, Toure, amekuwa akitumika kwa namna mbili kama kiungo wa juu na muda mwingine akicheza chini zaidi, kwa sasa akiwa anashirikiana na kiungo aliyesajiliwa kwa £30million Fernandinho.

SIFA ZAO ZA KIMWILI


UREFUUZITO
Yaya Toure189cm90kg
Marouane Fellaini194cm95kg


Kiukweli kabisa katika dunia ya soka hivi sasa ni wachezaji wachache wanaweza kucheza anavyocheza kiungo wa Ivory Coast, akitumia zaidi nguvu, akili katika kuitawala safu yote ya kiungo. 
Moyes atakuwa akiomba na kutumaini Fellaini, kiungo mkabaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo katika kipindi cha miaka sita, ataweza kucheza kama anavyocheza Toure katika safu ya kiungo ya United. 
Akiwa Fellaini atacheza kama alivyocheza usiku wa Jumanne, basi vita ya safu ya kiungo baina yake na Toure itachangia sana katika matokeo ya mwisho ya mchezo huo unaopigwa katika dimba la City of Manchester Stadium jumapili ya leo.
TAKWIMU ZA FELLAINI VS YAYA TOURE MSIMU ULIOPITA


VIDEO: OSCAR NA OBI WAIPA CHELSEA USHINDI WA 2-0 DHIDI YA FULHAM