Vilabu vyote viwili vinajinasibu kwamba vipo katika muda wa mapito baada ya kubadilisha makocha, lakini ushindi wa 4-1 wa City dhidi ya majirani zao ulionyesha utofauti mkubwa uliopo baina ya vikosi vya klabu hizi mbili.
City wana ukamilifu kwenye idara, ubora wa ufundi, na matamanio ya dhati ya kurudisha ubingwa wa Premier League chini ya kocha mwenye ufundi mkubwa hasa kwenye mechi kubwa kama hizi.
MSIMAMO WA PREMIER LEAGUE | |||
TIMU 1. Arsenal 2. Tottenham 3. Man City 4. Chelsea ...................... 5. Liverpool 6. Everton 7. Southampton 8. Man Utd | MECHI 5 5 5 5 ........ 5 5 5 5 | GD 5 4 8 4 ........ 2 2 1 1 | Points 12 12 10 10 ........ 10 9 8 7 |
David Moyes alipewa ratiba ngumu - na hata akalalamika kuhusu ratiba hiyo ngumu - lakini mscotish huyu amepata pointi moja tu katika michezo yote mitatu tuliyocheza na timu kubwa zenye upinzani nasi katika ligi na kikosi chake kimecheza kwa kiwango cha kuridhisha kwenye mchezo mmoja tu wa ligi.
Ukiachana na mchezo wa kufungua ligi dhidi ya Swansea, United tumekuwa tukionekana kukosa ubora wa pamoja kama timu, huku safu yetu ya ulinzi ikiyumba hasa kwa viwango vya wachezaji wetu wenye umri mkubwa kiasi kama Rio Ferdinand na Patrice Evra.
Ujio wa Marouane Fellaini katika siku ya mwisho ya usajili ulikuwa muhimu sana, lakini United bado wana tatizo sana katika safu ya kiungo - hawana uimara wa kuweza kufananisha na safu ya kiungo cha Chelsea, City, Tottenham, na sasa hata Arsenal wanaoringia ujio wa 'The Master of Assists' Mesut Ozil na mkabaji Matheiu Flamini.
Kitu kingine cha kuhuzunisha ni upangaji wa kikosi wa kocha, inaonekana bado anafanya majaribio wakati wapinzani wetu wengine wanaogombea TOP 4 wakiwa wameanza vizuri ligi, pamoja na kwamba wamebadilisha makocha na wengine hata wakiwa wameuza wachezaji mategemeo katika msimu uliopita.
United sasa kwa bahati nzuri tuna mechi ambazo angalau unaweza kuziita nyepesi mpaka pale tutakapokutana na 'The inform Gunners' Arsenal November 10. Lakini angalau hizi mechi na timu ndogo tusifanye makosa au Moyes ajiandae kutuletea aibu ya kukosa ubingwa na kukosa hata kushiriki Champions League msimu unaokuja.
in the world there are twp teams only, one is MANCHESTER UNITED and the other is OTHERS, huyu anayempangia Moyes kikosi apange kwanza cha timu yake LOCAL na NATIONAL then afuate UNITED. wanajua wanachofanya na cc tutulie tu maana hatuna mchango wowote kwenye timu zaidi ya kupiga kelele inaposhinda na kushindwa, SAF hawezi kuwa kocha maisha yote, as doesd MAN UTD haiwezi kuwa bingwa miaka yote, times change and now its our time the transition is with us!
ReplyDeletealex alipigwa 6 na city mbona mlikaa kimya liverpool iliifunga utd 4 tena old traford mbona hamkusema mwachen jamaa afanye kaz ndo maana simba yanga kila siku mnatimua makocha
ReplyDeleteyan pale mcmu huu atachukua ubingwa ashle young kwa kujiangusha ila nyie wengine msubili mcmu ujao hata kombe la ligi hata la Fa hakuna kitu mcmu huu tim yetu ya man city iko imara alifungwa faghason 6 sembuse moyes tena siku ile ilibidi tupige hata 9 bas zeko aloizingua tukiamua tunawauzia
ReplyDeletena bado we are blues true color
ReplyDeleteOzil ndo jibu pia Van Persie maujuz aliyopewa na Prof Wenger yanaelekea kwisha.
ReplyDeletemsisahau Van Persie alikuwa winga yule Prof wenger nimjuzi sana.
Naunga mkono hoja
ReplyDeletembona SAF alipigwa 6 - 2 tena nyumbani na nimzoefu wa ligi hiyo tena sana kwa iyo ni suala la kumpa mda Moyes maana bado hajui jinsi ya kupambana na Derby kama izo ila kama ataitaji matokeo kama hayo na kuishia nafasi za Uropa ligi kwenye msimamo aendelee kuwapiga bench Nani,Kagawa Chicharito(kijana alie jaa magoli miguuni kwake) ila akiendeleza uingereza wake wa kumpanga Welbeck,Young na Valencia(sio mwingereza) wataumia na leo wanakutana na Liverpool ya Suarez, mimi nasubiri soka tu.
ReplyDeletei support u n kwel hatuwez kuwa mabingwa sku zote coz kila m2 anataka ubingwa but tusmlaum coz msimu bado mkubwa kumbuka alikokuwa arsenal mwaka jana na wakamaliza wa tano xo big up Moyes
ReplyDeletebado unamtazamo wa jicho moja kaka
ReplyDelete