Search This Blog

Friday, December 14, 2012

MOPAO KOFFI OLIMIDE AHAIDI SHOW YA KUFA MTU LEADERS KESHO - KIRUMBA JUMAPILI


Mwanamuziki kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akitia saini moja ya bango lenye kampeni inayowatahadharisha madereva wa magari kunywa pombe kupindukia,ikiwa ni hatari kwa afya na usalama wao kwa ujumla,pichani kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Steve Gannon akishuhudia tukio hilo,aidha katika tukio hilo Wanahabari mbalimbali walishuhudia tukio hilo ndani ya hotel ya Serena Inn mapema leo mchana.Koffi Olomide na skwadi lake la Quartie Latin wametua jana jijini Dar kwa ajili ya maonesho yao mawili yatakayofanyika jijini Dar ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni siku ya jumamosi na jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM-Kirumba siku ya jumapili kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Tusker Lager.
 Bango alilotia wino Koffi Olomide.
 Koffi Olomide akitoa vionjo vya moja ya wimbo wake mbele ya wanahabari,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi Mwiyombela akinogesha
Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akiuzumguza mbele ya Wanahabari mapema leo ndani ya hotel ya Serena Inn,kuhusiana na onesho la Mwanamuziki kutoka DRC-Congo,Koffi Olomide linalotarajiwa kufanyika kesho jumamosi kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
 Baadhi ya wafanyakazi wa SBL wakifurahia jambo  
 Mkurugenzi wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi Mwiyombela akiwakaribisha wageni mbalimbali wakiwemo wanahabari kwenye mkutano uliohusu onesho la Mwanamuziki Koffi Olomide,ambalo limedhaminiwa na kampuni ya SBL kupitia kinywaji chake cha Tusker.
 Mwanamuziki kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akifafanua jambo mapema leo alipokuwa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani),ndani ya hotel ya Serena kuhusiana na onesho lake atakalolifanya hapo kesho ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Koffi amewaomba washabiki na wapenzi wake waje wajionee kazi kubwa atakayokuwa akiifanya jukwaani akiwa na vipaji vipya kabisa katika tasnia ya muziki wa dansi nchini Congo.
 Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Steve Gannon  akimkaribisha Koffi Olomide (hayupo pichani) na pia aliwataka mashabiki na wapenzi wa mwanamuziki huyo wajitokeze kwa wingi na kushuhudia tukio hilo adhimu hapo kesho.

 Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwashukuru Wadhamini wa onesho la Koffi Olomide pamoja na Wanahabari kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kuhakikisha jamii inapata taarifa mbalimbali kuhusiana na ujio wa mwanamuziki huyo pamoja na onesho lenyewe.
 Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akisalimiana mkono na Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga pichani shoto akiwa ameambata na mgeni wake Koffi Olomide sambamba na Mkurugenzi wa SBL,Steve Gannon wakiwasili ndani ya ukumbi wa mikutano,Serena Hotel kwa ajili ya kuzungumza na Wanahabari kuhusiana na onesho litakalofanyika kesho kwenye viwannja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Picha na Michuzijr.Blogspot.com.

WAKENYA KUCHEZESHA MECHI YA STARS, ZAMBIA




Mwamuzi Sylvester Kirwa kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kirwa anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range. Waamuzi hao wasaidizi ambao vilevile watatoka Kenya pia wanatambuliwa na FIFA.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini hoteli ya Tansoma, na inafanya mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.

SPORTS XTRA& BAR WADHAMINI KOZI YA WAAMUZI WA SOKA MKOA WA DAR ES SALAAM!

Alex Luambano akimkabidhi mratibu wa kozi ya waamuzi wa soka mkoa wa Dar Es Salaam mwamuzi Hashim Ramadhani, Chama cha waamuzi cha manispaa ya Kinondoni ( KIFRA ) Kimeandaa kozi ya kuwaongezea ujuzi waaamuzi wa mpira wa miguu wa mkoa wa Dar Es Salaam inayotaraji kufanyika hivi karibuni huko Bagamoyo.
Kitengo cha michezo cha CLOUDS MEDIA GROUP kimetoa udhamini wa SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI MOJA.

'' Sisi kama idara tumekuwa mbele kupigania maendeleo ya michezo hapa nchini hasa mchezo wa soka kwaiyo walipokuja waamuzi kuomba tuwasaidie kufanikisha kozi yao tukaona ni jambo la msingi,basi kama idara tukawachangia sehemu ya bajeti kiasi cha shilingi 1,000,000/= alisema Alex Luambano mmoja wa watangazi wa vipindi vya michezo vya SPORTS XTRA na SPORTS BAR.

TUSKER CARNIVALS CELEBRATIONS FEATURING KOFFI OLOMIDE!


* GIVING THE CONSUMERS A VALUABLE GOOD TIME*

13th December 2012, Dar es Salaam – With two great perfomances this weekend featuring the best Congolese musician Kofi Olomide better known as “Le Grand Mopao”, the Tusker carnival kicks off with style this weekend.

Kofi Olomide scheduled to arrive anytime now will have his first performance in Dar Es Salaam leaders club on the 15th December and thereafter will head to Mwanza Kirumba stadium on the 16th December 2012 for yet another thrilling performance.

Fans, especially those that truly enjoy the ‘BOLINGO’ themed dances and moves are now more eager than ever to find out what the sensational and stylish, Kofi brings to the stage this time around.

“It is a great honour for us to bring people together with great performances such as these ones. We know how unique Kofi Olomide is and loved by many.  To bring out even bigger and greater bond, with our consumers we have organised Tusker carnivals to trail out to four major towns.  The first two will be Dar Es Salaam and Mwanza, which will be graced by Kofi.  We also have Moshi and Mbeya, these two which are scheduled in the next week will feature our top local bands and musicians,” Said Maurice Njowoka, Brand manager, Tusker.

The entrance set for leaders club this Saturday is at Tshs.10,000 for those who will join the carnival in the morning hours and those who come in the evening will be charged Tshs.15,000.

“We urge Kofi fans and our Tusker consumers as well as those who delight to the band music to show up in large numbers as there will lots for all of them”, he continued.

 About Tusker Lager
Tusker is an enduring brand full of vitality that unites people, one full of progressive spirit and modernity.  A beer brewed since 1922 with enhanced quality over the years.  A beer grounded in its roots just like the people of Africa giving people the belief and optimism of a brighter future.  Tusker is a medium strength beer enjoyed easily among friends.

 Please remember to drink responsibly, strictly 18+

For more information:, contact the Corporate Relations Director, Ms. Nandi Mwiyombella  nandi@serengetibrew.com

MKOA WA KILIMANJARO NAO WAUPINGA WARAKA WA TFF!

Koffi Olomide atua jijini Dar tayari kwa onesho lake la Jumamosi

Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku huu mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),tayari kwa onesho lake litakalofanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,onesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio chake kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini.Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga
Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Koffi Olomide mara baada ya kuwasili usiku huu  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar.Koffi alitanabaisha kuwa yeye amekuja nchini Tanzania kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa ndani ya kundi lake la Quartier Latin.

KIKOSI BORA CHA DUNIA 2012: VAN PERSIE, YAYA TOURE NJE - LA LIGA YATAWALA

Katika tuzo za ubora zinazotolewa na jarida la World Soccer pia imetajwa timu bora ya dunia iliyochaguliwa na wachambuzi wa soka na wasomaji wa jarida.

Pamoja na kuwa katika kiwango bora kwa mwaka huu mfungaji bora wa EPL msimu uliopita Robin Van Persie na kiungo bora aliyeiongoza Manchester City kutwaa kombe la EPL baada ya kipindi kirefu sana - muafrika Yaya Toure hawamo katika kikosi hicho.

Hii ndio kikosi kamili cha wachezaji bora wa dunia 2012.
  

LEO MESSI AANZA KUKUSANYA TUZO: ATAJWA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA - ZAMBIA YATISHA TUZO ZA JARIDA LA WORLD SOCCER


Lionel Messi amechaguliwa na jarida la World Soccer kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2012. Mchezaji huyo wa  Barcelona na Argentina alikusanya kura mara mbili ya alizopata mpinzani wake Cristiano Ronaldo aliyeshika nafasi ya pili na mchezaji mwenzie wa Barca Andres Iniesta akshika nafasi ya tatu.


Hii ni mara ya tatu Messi anashinda tuzo hii, akiwa ameshinda mwakak 2009 na 2011. Akiungana na Mbrazil Ronaldo aliyshinda mara tatu na yeye.

Pia kocha wa Spain Vicente Del Bosque amechaguliwa kuwa kocha wa dunia kwa 2012 kutokana na mafanikio aliyoipa timu ya taifa ya nchi hiyo.





Kwa mara ya kwanza katika miaka 30 ya utoaji wa tuzo hizo - mwakak huu kura za mashabiki zimechangwa na jopo maalum la wachambuzi wa soka kisha ndio majibu ya kuamua wanaostahili tuzo kutolewa.
 
Pia katika hali nyingine timu ya Taifa ya Zambia imepigiwa kura kuwa timu bora ya taifa iliyoshika nafasi ya pili nyuma ya Spain.


2012 World Player of the Year
1 Lionel Messi (Barcelona & Argentina) 47.33%
2 Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Portugal) 19.01
3 Andres Iniesta (Barcelona & Spain) 9.77
4 Andrea Pirlo (Juventus & Italy) 6.10
5 Radamel Falcao (Atletico Madrid & Colombia) 5.95
6 Neymar (Santos & Brazil) 3.60
7 Iker Casillas (Real Madrid & Spain) 2.30
8 Xavi (Barcelona & Spain) 1.78
9 Didier Drogba (Chelsea/Shanghai Shenhua & Ivory Coast) 1.77
10 Eden Hazard (Lille/Chelsea & Belgium) 0.37

2012 World Manager of the Year
1 Vicente Del Bosque (Spain) 28.49
2 Jose Mourinho (Real Madrid) 12.27
3 Roberto Di Matteo (Chelsea) 12.05
4 Jurgen Klopp (Borussia Dortmund) 10.33
5 Diego Simeone (Atletico Madrid) 7.19
6 Herve Renard (Zambia) 6.83
7 Marcelo Bielsa (Athletic Bilbao) 5.74
8 Tite (Corinthians) 4.67
9 Pep Guardiola (Barcelona) 2.72
10 Luis Tena (Mexico Olympic) 2.63

2012 World Team of the Year
1 Spain 47.36
2 Zambia 8.52
3 Chelsea 7.84
4 Juventus 7.36
5 Atletico Madrid 4.89
6 Borussia Dortmund 4.25
7 Corinthians 4.23
8 Universidad de Chile 4.00
9 Barcelona 3.63
10 Montpellier 2.90

Namna kura zilizopigwa na wasomaji
Player
Lionel Messi 40.13 %
Cristiano Ronaldo 18.94
Radamel Falcao 10.99
Andrea Pirlo 9.48
Neymar 7.20
Andres Iniesta 6.82
Xavi 2.65
Didier Drogba 2.63
Eden Hazard 0.76
Yaya Toure 0.38

Manager

Del Bosque 21.54
Jose Mourinho 15.45
Roberto Di Matteo  11.38
Marcelo Bielsa 10.57
Jurgen Klopp 9.77
Tite 9.35
Diego Simeone 8.94
Herve Renard 7.31
Rene Girard 4.06
Luis Tena 1.63

Team

Spain 32.00
Juventus 12.00
Zambia 9.78
Chelsea 9.33
Atletico Madrid 8.88
Corinthians 8.45
Universidad 8.00
Borussia Dortmund 5.78
Montpellier 4.00
Mexico Olympic 1.78

Panel votes
Player
Lionel Messi 54.54%
Cristiano Ronaldo 19.09
Andres Iniesta 12.73
Iker Casillas 4.54
Andrea Pirlo 2.73
Mohamed Aboutrika 0.91
Sergio Ramos 0.91
Radamel Falcao 0.91
Didier Drogba 0.91
Juan Mata 0.91
Zlatan Ibrahimovic 0.91
Xavi 0.91

Manager

Vincente Del Bosque 35.45
Roberto Di Matteo 12.73
Jurgen Klopp 10.90
Jose Mourinho 9.09
Herve Renard 6.36
Diego Simeone 5.45
Pep Guardiola 5.45
Antonio Conte 3.64
Luis Tena 3.64
Roberto Mancini 1.81
Cesare Prandelli 1.81
Alex Ferguson 0.91
Rene Girard 0.91
Jorge Sampaoli 0.91
Theo Bucker 0.91
Marcelo Bielsa 0.91

Team

Spain 62.73
Zambia 7.27
Barcelona 7.27
Chelsea 6.36
Real Madrid 5.45
Borussia Dortmund 2.73
Juventus 2.73
Montpellier 1.81
Al Ahly 0.91
Manchester United 0.91
Atletico Madrid 0.91
Bayern Munich 0.91
Manchester City 0.91

AZAM SAFARINI LEO KWENDA CONGO - HII NDIO LISTI YA WACHEZAJI WANAOSAFIRI NA TIMU

 
Wachezaji wa Azam FC wanaosafiri leo kuelekea Kinshasa DRC ni
HERMAN/KIPRE TCHETCHE
RASHID/ABDALLAH SEIF
MICHAEL/KIPRE BOLOU
PAZI/ZAHORO IDDI
WANDWI/JACKSON
NDEULE/MALIKA PHILIP
MWAMBUNGU/UHURU SELEMANI
MTAKI/OMARI MSAFIRI
STIMA/JABIR AZIZ
MWAIPOPO/IBRAHIM
MWAIKIMBA/GAUDENCE
SADALA/ABDI KASSIM
KAKOLAKI/LUCKSON
NUHU/SAMIH
MWADINI/ALLY MWADINI
MKAMI/HIMID MAO
MWANTIKA/DAVID JOHN
OMAR/WAZIRI SALUM
JOCKINS/ATUDO
HUMPHREY/MIENO

VIONGOZI
IDRISSA/NASSOR
MAPWISA/ABUBAKAR
ONGALA/KALIMANGONGA
GOMES/PAULO
ABUBAKAR/IDDI
NZAWILA/YUSUPH
HALL/STEWART JOHN
SAID/JEMEDARY

Thursday, December 13, 2012

ujio wa koffi Olimide


OFFICIAL: MILOVAN APIGWA CHINI SIMBA - HUYU NDIO KOCHA MPYA - ZISOME SIFA NA TAKWIMU ZAK




Klabu ya ya Simba SC jana ilitangaza rasmi kwamba imevunja mkataba na kocha Mserbia Milovan Cirkovic na kutangza kumleta kocha mpya kutoka nchini Ufaransa Patrick Liewig.

Akizungumza jana na waandishi wa habari afisa habari a Simba Ezekiel Kamwaga alisema wameamua kumchukua Liewig kwa sababu ni kocha anayendana na falasafa ya Simba na hali ya soka la Tanzania lilivyo sasa.

Kocha huyo ambaye amewahi kuvifundisha vilabu vingi katika ulimwengu wa soka vikiwemo PSG ya Ufaransa alipokuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo huku akihusika zaidi na academy ya timu hiyo, Club African ya Tunisia pamoja moja klabu kubwa barani Afrika ya ASEC Mimosas ya Cote d'Ivoire.

Liewig ambaye ni mtalaam aliyebobea katika soka la vijana anategemewa kutua Tanzania ndani ya kipindi cha wiki mbili mpaka tatu zijazo kupisha msimu wa sikukuu ya krisimasi.  

HUU NDIO WASIFU WA KOCHA MPYA WA SIMBA 
 

HUKU WATU WAKIZIDI KUIPINGA REKODI YAKE: LEO MESSI APIGA NYINGINE MBILI NA KUTIMIZA MABAO 88 NDANI YA MWAKA 1



Cordoba vs Barcelona 0:2 GOALS HIGHLIGHTS by UCL2410

KALI YA LEO: CLAUDIO RANIERI ATISHIA KUWAUA WACHEZAJI WA MAONACO BAADA YA KUFUNGWA


Aibu ya kipigo cha 3-0 dhidi ya Caen imeifanya Monaco kushuka hadi nafasi ya pili katika ligi ya daraja la kwanza nchini Ufaransa na sasa meneja Claudio Ranieri ametangaza kwamba ikiwa wachezaji wake hawatoshinda mechi ijayo, atawaua. Kwa sababu ipi ni njia nzuri ya kuwatia hamasa ya kufanya wachezaji wanaopewa kila kitu lakini wanashindwa kufanya vizuri zaidi ya kuwatishia maisha yao?
Kutoka Reuters:
"Nina hasira sana. Kinguvu tulikuwa wapili kwa ubora na haya ndio matokeo. Nataka kushinda. Inatupasa kushinda vinginevyo nitakuja kuwaua hawa wachezaji," kocha wa zamani wa Chelsea na Juventus, ambaye alijiunga na Monaco mwezi watano, aliuambia mkutano wa waandishi wa habari siku ya jumatano.
"Timu tunazokutana nazo zinajituma kwa asilimia mia, na wakati sie tukiwa hatufanyi hivyo ni vigumu kushinda."
Hii ndio labda njia sahihi ambayo Arsene Wenger inabidi ajaribu kuitumia.

UCHAGUZI WA DRFA: KASONGO MWENYEKITI MPYA - DAUDA NA TEMBELE CHALIII

Uchaguzi wa chama cha mpira jijini Dar es Salaam DRFA umefanyika leo mchana na matokeo yapo kama ifuatavyo: Mwenyekiti ni Almas Kasongo amepata kura 11, akifuatiwa na mpinzani wake Evans Aveva amepata kura 7.                     Makamu m/kiti: Mede Ramadhani ambaye alipata kura 11 na kumfunika vibaya Ally Mayai alyepata kura 3.                                   Mjumbe mkutano mkuu - Muhsin Said aliwashinda wapinzani kwa kura 10, akafuatiwa na Shufaa Jumanne aliyepata 6, huku Shaffih Dauda akiambulia kura 2.                                             Uwakilishi wa vilabu ulienda kwa Benny Kisaka aliyebeba kura 14, na kumzidi mpinzani wake Philemon Ntahilaji aliyepata kura 4.                                                                                                     Katibu Mkuu akachaguliwa kuwa Msanifu Kondo.

















Wednesday, December 12, 2012

MWINYI KAZIMOTO KUCHUKUA NAFASI YA MRISHO NGASSA EL MERREIKH

Baada ya mchezaji Mrisho Ngassa kuingia mitini huku taarifa za kuaminika kutoka kwa vyanzo vilivyo karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga vikisema - Mrisho amekubali kimsingi kujiunga na mabingwa wa Afrika mashariki na kati baada ya mkopo wake utakapoisha katika klabu ya Simba, hivyo dili lake la kujiunga na El Merreikh kuota mbawa - leo hii kuna taarifa kutoka klabu ya Simba kwamba El Merreikh wameonesha nia ya kumtaka nyota Mwinyi Kazimoto kama mbadala wa Haruna Niyonzima ambaye walikuwa wakimtaka lakini ameamua kubaki kwenye klabu yake.

Akizungumza na mtandao chanzo cha habari kutoka Simba kinasema kwamba, kumefanyika mazungumzo ya mwanzo tu na El Merreikh wameonekana kuvutiwa na Mwinyi kwa kuwa walikuwa wanatafuta kiungo baada ya Niyonzima kukubali kuendelea kuichezea Yanga.

"Simba tupo tayari kumuuza Mwinyi Kazimoto kwa sababu klabu yetu inaamini katika kutoa nafasi kwa wachezaji kujiendeleza zaidi. Mazungumzo yanaendelea na kama kila kitu kikiwa sawa basi hivi karibuni Mwinyi atakuwa mchezaji mpya wa El Merreikh."

VIPIMO VYA AFYA, BANGI, UTOTO NA MAPENZI YA YANGA - MAONI YA WASHABIKI KUHUSU SAKATA LA YANGA