Search This Blog
Tuesday, July 3, 2012
BALOTELLI ATEGEMEA KUPATA MTOTO NA MPENZI WAKE WA ZAMANI
Raffaella Fico mrembo mwanamitindo wa Italia mwenye umri wa miaka 24, anategemea kupata mtoto na Mchezaji wa Timu ya taifa ya italia na Manchester city Mario Balotelli “super Mario”, Raffaella ametoa taarifa kuwa amegundua ni mja mzito mwezi wa tano mara baada ya penzi la wawili hao kuvunjika mara baada ya kumtuhumu balotelli kuwa na wapenzi wengi. Raffaella aliwahi na mahusiano na Mchezaji Cristiano Ronaldo
Raffaella amewaambia waandishi wa habari kuwa Mario amekuwa excited na habari za kuwa baba na inawezekana wakabatana for the sake of their child
Source:Darbase magazine
SPAIN WAREJEA NYUMBANI - WAPOKEA KIFALME NA MAELFU YA WAHISPANIA WAKIONGOZWA NA MFALME
Timu ya taifa ya Spain leo hii imerejea nyumbani kwao na kupokea na melfu ya wananchi wa nchi wakiongozwa familia ya mfalme wa nchi hiyo.
STRIKER MPYA WA SIMBA ABDALLAH JUMA APIGA GOLI 2 MNYAMA AKIMTAFUNA MAFUNZO
Siku moja baada ya kutoka sare na klabu ya Express ya Uganda, mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Simba imeanza vyema michuano ya kombe la Urafiki huko Zanzibar baada ya kuwagonga wala urojo klabu ya Mafunzo kwa mabao mawili kwa moja.
Alikuwa ni kinda jipya la klabu hiyo lilosajiliwa kutoka klabu ya Ruvu Shooting aliyefunga mabao ote mawili katika dakika ya 27 na 44, huku pasi za mwisho zote zikitolewa na kiungo mpya wa timu hiyo Kanu Mbivayanga raia wa DRC Congo.
Kwenye dakika ya 80 Mafunzo walikuja juu na kufanikiwa kufunga bao la kufutia machozi lilofungwa Jaku Joma
Simba; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah/Paul Ngalema, Lino Masombo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Danny Mrwanda/Mwinyi Kazimoto, Mussa Mudde/Salim Kinje, Abdallah Juma/Uhuru Suleiman, Kanu Mbivayanga/Haroun Othman na Kiggi Makassy.
Mafunzo: Suleiman Janabi, Hajji Abdi, Ally Juma, Yussuf Makame, Said Mussa, Juma Othman, Abdulrahim Mohamed, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Ismail Khamis, Juma Jaku na Ally Othman.
Monday, July 2, 2012
YUSUSPH MANJI ASHINDA PINGAMIZI ALILOWEKEWA - KUENDELEA KUGOMBEA UENYEKITI YANGA
MVAMIZI: ANGALIA NAMNA WACHEZAJI WA REAL MADRID WALIVYOMTIMUA JAVIER MARTINEZ WAKATI KUPIGA PICHA
| Wakati Spain walipokuwa wamekabidhiwa kombe lao la Euro wachezaji wa Barcelona na Real Madrid walianza kuchukua kombe na kuanza kupiga nalo picha kwa kila kundi la wachezaji wa timu hizo mbili kupiga picha ya pamoja na kombe. Walianza Barceona ambao wao ndio wengi kwenye kikosi cha Spain wakapiga picha na kombe kisha wakawabidhi wa Real Madrid - wakiongozwa na nahodha Iker Casillas, Raul Albiol, Arbeloa, Xabi Alonso na Sergio Ramos walijipanga kupiga picha na kombe na ghafla akaibuka Javier Martinez wa Atletico Madrid na kujipanga nao - kwa utani mchezaji mwingine akisaidiana na Sergio Ramos wakamtoa kwenye sehemu ya kupiga picha hiyo maalum kwa wachezaji wanaochezea Madrid. |
PELE AWAONGOZA WATU MILLIONI 16 - KUVUNJA REKODI YA TWITTER DUNIANI
Mtandao wa kijamii wa Twitter umesema watumiaji wa mtandao huo walikuwa wakituma tweets zaidi ya 15,000 kwa sekunde wakati Spain walipofunga goli la nne kwenye mchezo wa Jumapili wa fainali ya Euro - ikiwa ni rekodi mpya inayohusiana na michezo katika mtandao huo wa kijamii.
Twitter wanasema kwamba traffic ya tweets duniani kote ilifikia mpaka 15,358 kwa sekunde wakati wa goli la nne lilipofungwa mjini Kiev, ambapo Spain walishinda kwa goli 4-0. Twitter pia wamesema kwa usiku wa jana tweets millioni 16.5 zilitumwa kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Katika watu walio-tweet mmoja wao alikuwa Pele, mchezaji mstaafu wa Brazil. Aliwapongeza Spain na kusema anategemea makubwa kwenye fainali za kombe la dunia 2014.
Twitter wanasema kwamba traffic ya tweets duniani kote ilifikia mpaka 15,358 kwa sekunde wakati wa goli la nne lilipofungwa mjini Kiev, ambapo Spain walishinda kwa goli 4-0. Twitter pia wamesema kwa usiku wa jana tweets millioni 16.5 zilitumwa kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Katika watu walio-tweet mmoja wao alikuwa Pele, mchezaji mstaafu wa Brazil. Aliwapongeza Spain na kusema anategemea makubwa kwenye fainali za kombe la dunia 2014.
HIVI NDIVYO SPAIN WALIVYOANZA NA KUMALIZA EURO WAKITWAA UBINGWA
Kutoka kuitwa wacheza soka wasio na mafanikio mpaka kuja kuandika jina lao kwenye vitabu vya historia kwa kushinda mataji matatu makubwa mfululizo baada kuwafunga Italy na kuweza kutetea ubingwa wao ulaya - hawa ndio Spain.
Wakiwa wameshinda kombe moja tu la kimataifa kwenye historia ya soka kabla ya mwaka 2008, La Roja saa wanayo matatu kwa mfululizo kufuatiwa kushinda Euro 2008, World Cup 2010 - lakini tofauti na miaka minne iliyopita nchini Austria na Switzerland, Spain ya safari hii ilikumbana na mawazo tofauti kutoka kwa wadau juu ya staili yao ya uchezaji lakini mwisho wa siku waliwanyamazisha jana usiku baada ya kuchukua ubingwa wa Euro 2012.
Wakicheza bila mshambuliaji halisi kwenye mechi dhidi ya Italy, Croatia na Ureno, Spain walionekana kupata taabu kidogo lakini wakicheza dhidi ya Ireland, France na baada kuwamalizia na kuwatia aibu waitaliano kwenye fainali - La Roja wamethibitisha kwamba hizi ni zama zao.
Ebu tuangalie safari yao kutoka mwanzo mpaka mwisho wa michuano ya Euro 2012 ilivyokuwa kwa picha.
Watoto wa Del Bosque wakiwa wamepumzika baada ya mazoezi ya siku ya kwanza kuelekea kwenye Euro
Cesc Mwokozi: Fabregas aliiokoa Spain kwa kufunga goli la kusawazisha dhidi Italy kwenye makundi
Torres akifunga goli lake la kwanza la mashindano dhidi ya Ireland
DAVID VS GOLIATH: Silva akifunga goli kwenye msitu wa mabeki wa Ireland
JESUS: NAVAS AKIFUNGA BAO LA USHINDI DHIDI CROATIA
Shujaa wa karne | Alonso akishangilia goli la kwanza kwenye mechi ya 100 kuichezea La Roja dhidi ya France.
Xabi Alonso akifunga bao la pili na ushindi kwa Spain dhidi ya France kwenye robo fainali
Wewe tena | Busquets na Ronaldo wakikumbushia upinzani wa vilabu vyao kwenye level ya kimataifa.
Iker akiokoa | Casillas akiokoa penati ya kwanza ya Portugal kwenye nusu fainali.
Cesc Fabregas akifunga penati ya ushindi dhidi ya Ureno
KIPUTE KIKIANZA
Maestro kazini| Xavi akiwafanyia balaa waitaliano kwa kuiongoza meli ya La Roja dhidi ya Azzur.
Jolly Jordi akafunga bao la pili
Game over | Kutoka kwa Thiago Motta kuliwafanya Italy wacheze na watuu 10 - Spain hapo ndipo wakamaliza mchezo.
Goli la tatu kwa Torres | El Nino akifunga bao la tatu kwenye Euro na kupata tuzo ya kiatu cha dhahabu
KIPA BORA | Casillas akishangilia ushindi wa kihistoria kwa nchi yake.
Filimbi ya mwisho | Benchi la La Roja likishangilia baada ya filimbi ya mwisho kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Italy.
Wafalme Kiev | Casillas akiwa amebeba kombe la Henri Delaunay baada ya Spain kushinda Euro 2012
SPAIN WATOA WACHZAJI 10 KWENYE KIKOSI CHA MASHINDANO CHA UEFA - MFUNGAJ BORA TORRES ATEMWA - INIESTA AIBUKA MCHEZAJI BORA WA MASHINDANO
Shirikisho la soka la bara la ulaya UEFA limemtangaza kiungo wa Spain Andres Iniesta kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Euro 2012.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 alianza kwenye mechi zote sita za Euro na akucheza kama kiungo mshambuliaji na kuiwezesha timu yake ya La Roja kubeba ndoo jana usiku.
Iniesta ambaye alichaguliwa na watu 11 wa jopo la ufundi la UEFA, alitoa assist moja katika dakika dakika 551 alizocheza kwenye Euro 2012.
Pia yupo kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa UEFA wa michuano hiyo, ambacho pia kimebeba wachezaji 10 wa Spain na wanne wa Italy.
Cha kushangaza zaidi mfungaji bora wa mashindano Fernando Torres hayupo kwenye kikosi, kucheza dakika 189 kukionekana kuwa sababu kubwa, Mario Balotelli, Cesc Fabregas, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na David Silva ndio wanaounda safu ya ushambuliaji.
HIKI NDIO KIKOSI CHA MICHUANO HIYO KILICHOCHAGULIWA NA UEFA
Goalkeepers: Gianluigi Buffon (Italy), Iker Casillas (Spain), Manuel Neuer (Germany)
Defenders: Gerard Pique (Spain), Fabio Coentrao (Portugal), Philipp Lahm (Germany), Pepe (Portugal), Sergio Ramos (Spain), Jordi Alba (Spain)
Midfielders: Daniele De Rossi (Italy), Steven Gerrard (England), Xavi (Spain), Andres Iniesta (Spain), Sami Khedira (Germany), Sergio Busquets (Spain), Mesut Ozil (Germany), Andrea Pirlo (Italy), Xabi Alonso (Spain)
Attackers: Mario Balotelli (Italy), Cesc Fabregas (Spain), Cristiano Ronaldo (Portugal), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), David Silva (Spain).
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 alianza kwenye mechi zote sita za Euro na akucheza kama kiungo mshambuliaji na kuiwezesha timu yake ya La Roja kubeba ndoo jana usiku.
Iniesta ambaye alichaguliwa na watu 11 wa jopo la ufundi la UEFA, alitoa assist moja katika dakika dakika 551 alizocheza kwenye Euro 2012.
Pia yupo kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa UEFA wa michuano hiyo, ambacho pia kimebeba wachezaji 10 wa Spain na wanne wa Italy.
Cha kushangaza zaidi mfungaji bora wa mashindano Fernando Torres hayupo kwenye kikosi, kucheza dakika 189 kukionekana kuwa sababu kubwa, Mario Balotelli, Cesc Fabregas, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na David Silva ndio wanaounda safu ya ushambuliaji.
HIKI NDIO KIKOSI CHA MICHUANO HIYO KILICHOCHAGULIWA NA UEFA
Goalkeepers: Gianluigi Buffon (Italy), Iker Casillas (Spain), Manuel Neuer (Germany)
Defenders: Gerard Pique (Spain), Fabio Coentrao (Portugal), Philipp Lahm (Germany), Pepe (Portugal), Sergio Ramos (Spain), Jordi Alba (Spain)
Midfielders: Daniele De Rossi (Italy), Steven Gerrard (England), Xavi (Spain), Andres Iniesta (Spain), Sami Khedira (Germany), Sergio Busquets (Spain), Mesut Ozil (Germany), Andrea Pirlo (Italy), Xabi Alonso (Spain)
Attackers: Mario Balotelli (Italy), Cesc Fabregas (Spain), Cristiano Ronaldo (Portugal), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), David Silva (Spain).
TWIGA STARS WAKANA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA USAGAJI
Uongozi wa Twiga Stars umekana kuwepo vitendo vyovyote vya kinyume na maadili kwa wachezaji wa timu hiyo ambayo hivi karibuni ilitolewa kwenye mechi za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC).
Wakizungumza na waandishi wa habari leo (Julai 2 mwaka huu), Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa wamesema hakuna vitendo vya aina hiyo.
Mkwasa amesema alikaririwa vibaya kuhusu suala hilo wakati akiwa kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Star Tv kutokana na swali alilokuwa ameulizwa kuhusiana na vitendo hivyo.
“Ukifuatilia mahojiano yangu na Star Tv mimi sikusema kuwa kuna vitendo hivyo. Tatizo nadhani lilianzia kwa magazeti yaliyonukuu kupitia Star Tv, na wala kujiuzulu kwangu hakukuhusiana na hilo, nimewajibika kama kocha kutokana na kutolewa na Ethiopia,” amesema Mkwasa.
Naye Furaha Francis amesisitiza kuwa hakuna vitu vya aina hiyo katika timu hiyo, na kama kuna mtu ana ushahidi na hilo ni bora akauonesha badala ya kuzungumzia uvumi kuliko ukweli.
“Ukweli ni kwamba si sisi na wachezaji tu ambao hatukufurahishwa kutolewa na Ethiopia, wapo Watanzania wengi ambao hawakufurahishwa na matokeo yale. Twiga Stars si timu ya kudumu, haikai na wachezaji kwa muda wote, kila mchezaji ana timu yake.
HABARI NZURI KWA WANAYANGA: NIYONZIMA AREJEA JANGWANI MAZOEZINI LEO
Kiungo wa Kimataifa raia wa Rwanda,Haruna Niyonzima Fabregas amerejea jana usiku na kujiunga na Kikosi cha Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Young Africans Sport Club (YANGA) katika mazoezi yanayotarajiwa kuanza leo jioni saa kumi katika uwanja wa Kaunda Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na tovuti ya klabu www.youngafricans.co.tz kiungo huyo amesema kuchelewa kwake kulitokana na matatizo binafsi yaliyokuwa yamemkuta wakati akiwa nchini kwao na kusababisha kuchelewa kujiunga na Kikosi chake.
Haruna amewataka wachezaji wenzake kurejesha heshima kwa mara nyingine kwa kutwaa kombe la Kagame katika michuano inayotarajiwa kuanza Julai 14 Mwaka huu, huku Yanga ikiwa ndiyo Mabingwa watetezi wa michuano hiyo.
Niyonzima amesema tangu alipokuwa mapunziko alikuwa akifuatilia kwa karibu juu ya Klabu yake ya Yanga hasa katika zoezi la usajiri unaoendelea na kupongeza usajili huo kutokana na baadhi ya wachezaji anaowafahamu kusajiriwa katika kikosi hicho.
Yanga itaanza kutupa karata yake dhidi ya Atletico ya Burundi ambapo mechi hiyo ndiyo itakayokuwa ni pekee wakati wa ufunguzi itachezwa katika uwanja wa Taifa,Jijini Dar es Salaam huku Simba ikaanza kampeni siku inayofuata.
SIMBA WASHINDWA KUWATAFUNA WANYONGE WA YANGA TAIFA
![]() |
| Hatari langoni mwa Express |
![]() |
| Abdallah Juma kulia akilitia misukosuko lango la Express |
![]() |
| Krosi ya Uhuru, jamaa kanawa refa kapeta |
![]() |
| Benchi la Simba SC |
Source: bongostaz.blogspot.com
Subscribe to:
Posts (Atom)



















