Search This Blog

Monday, July 2, 2012

HIVI NDIVYO SPAIN WALIVYOANZA NA KUMALIZA EURO WAKITWAA UBINGWA



Kutoka kuitwa wacheza soka wasio na mafanikio mpaka kuja kuandika jina lao kwenye vitabu vya historia kwa kushinda mataji matatu makubwa mfululizo baada kuwafunga Italy na kuweza kutetea ubingwa wao ulaya - hawa ndio Spain.

Wakiwa wameshinda kombe moja tu la kimataifa kwenye historia ya soka kabla ya mwaka 2008, La Roja saa wanayo matatu kwa mfululizo kufuatiwa kushinda Euro 2008, World Cup 2010 - lakini tofauti na miaka minne iliyopita nchini Austria na Switzerland, Spain ya safari hii ilikumbana na mawazo tofauti kutoka kwa wadau juu ya staili yao ya uchezaji lakini mwisho wa siku waliwanyamazisha jana usiku baada ya kuchukua ubingwa wa Euro 2012.

Wakicheza bila mshambuliaji halisi kwenye mechi dhidi ya Italy, Croatia na Ureno, Spain walionekana kupata taabu kidogo lakini wakicheza dhidi ya Ireland, France na baada kuwamalizia na kuwatia aibu waitaliano kwenye fainali - La Roja wamethibitisha kwamba hizi ni zama zao.

Ebu tuangalie safari yao kutoka mwanzo mpaka mwisho wa michuano ya Euro 2012 ilivyokuwa kwa picha.



Watoto wa Del Bosque wakiwa wamepumzika baada ya mazoezi ya siku ya kwanza kuelekea kwenye Euro

Goli pekee alilofungwa Casillas kwenye dakika 90 kwenye Euro 2012

Cesc Mwokozi: Fabregas aliiokoa Spain kwa kufunga goli la kusawazisha dhidi Italy kwenye makundi

Torres akifunga goli lake la kwanza la mashindano dhidi ya Ireland

DAVID VS GOLIATH: Silva akifunga goli kwenye msitu wa mabeki wa Ireland



JESUS: NAVAS AKIFUNGA BAO LA USHINDI DHIDI CROATIA

Shujaa wa karne | Alonso akishangilia goli la kwanza kwenye mechi ya 100 kuichezea La Roja dhidi ya France.

Xabi Alonso akifunga bao la pili na ushindi kwa Spain dhidi ya France kwenye robo fainali

Wewe tena |
Busquets na Ronaldo wakikumbushia upinzani wa vilabu vyao kwenye level ya kimataifa.


Iker akiokoa | Casillas akiokoa penati ya kwanza ya Portugal kwenye nusu fainali.


Cesc Fabregas akifunga penati ya ushindi dhidi ya Ureno


KIPUTE KIKIANZA 
 Silva akiwatungua waitaliano baada ya pasi safi kutoka kwa Fabregas.

Maestro kazini|
Xavi akiwafanyia balaa waitaliano kwa kuiongoza meli ya La Roja dhidi ya Azzur.

Jolly Jordi akafunga bao la pili

Game over |
Kutoka kwa Thiago Motta kuliwafanya Italy wacheze na watuu 10 - Spain hapo ndipo wakamaliza mchezo.

Goli la tatu kwa Torres |
El Nino akifunga bao la tatu kwenye Euro na kupata tuzo ya kiatu cha dhahabu

KIPA BORA |
Casillas akishangilia ushindi wa kihistoria kwa nchi yake.

Filimbi ya mwisho |
Benchi la La Roja likishangilia baada ya filimbi ya mwisho kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Italy.
Top of the world | Cesc, Xabi & Co. walitengeneza history baada ya kushinda taji kubwa la tatu mfululizo

Wafalme Kiev | Casillas akiwa amebeba kombe la Henri Delaunay baada ya Spain kushinda Euro 2012

No comments:

Post a Comment