Search This Blog

Tuesday, April 24, 2012

ITS ALMOST DONE..... SIMBA YAKARIBIA BINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE 2012


WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC jioni hii wamejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuifunga Moro United ya Morogoro maba 3-0 na mechi ya wapinzani wao katika mbio za ubingwa,  Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ikivunjika timu hizo zikiwa zimefungana 1-1, Uwanja wa Azam, Chamazi.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Patrick Mutesa Mafisango, Haruna Moshi Shaaban 'Boban' na Felix Mumba Sunzu Jr.
Simba sasa imetimiza pointi 59, ambazo kutokana na matokeo ya leo ya sare ya 1-1 kati ya azam na Mtibwa, haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Lakini kujiweka salama, Simba itahitaji japo polnti moja katika mechi zake tatu zilizobaki. 
Mchezo kati ya Azam na Mtibwa ulivunjika wakati beki Salum Swedi amekwishaifungia bao Mtibwa na Mrisho Khalfan Ngassa ameifungia Azam FC. Mtibwa waligomea mechi hiyo wakipinga Azam kupewa penalti. Sasa Kamati ya Ligi Kuu itakutana kesho na kutoa uamuzi, lakini kuna uwezekano mkubwa Mtibwa ikatozwa faini na wapinzani wao kupewa ushindi.



Nafasi
TimuMPWDLGFGA+/-Pts
1 Simba SC25185242123059
2 Azam23155334112350
3 Young Africans24154538211749
4 Mtibwa Sugar2310583125635
5 Coastal Union24102122429-532
6 Kagera Sugar2471072525031
7 JKT Ruvu2471072530-531
8 Ruvu Shooting247982019130
9 JKT Oljoro237881620-429
10 Toto African2451182327-426
11 African Lyon2458112029-923
12 Villa Squad2465132643-1723
13 Moro United25310122744-1719
14 Polisi Dodoma2538141834-1617

Monday, April 23, 2012

MAGOLI 34 NA JINSI ALIVYOBADILISHA MSIMU WA ARSENAL: TATHIMINI YA MCHEZAJI BORA WA ENGLAND VAN PERSIE KUTOKA AUGUST 2011 - APRIL 2012

AUGUST
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
4(0)
1/1/2
2
6.25
Van Persie, na Arsenal in general, walianza msimu taratibu. Baada ya sare tasa katika mechi ya ufunguzi., baadae mdachi huyo akafunga goli muhimu la kusawazisha dhidi ya Udinese katika mechi ya play off ya champions league kabla ya kufunga goli la pili katika mechi ya aibu kwa upande wao waliyofungwa 8-2 naManchester United.
SEPTEMBER



SEPTEMBER

GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
4(0)
1/1/2
2
6.25
Arsenal waliendelea kucheza ovyo mwezi wote wa septmber, ushindi mwembamba dhidi ya Swansea na droo ngumu dhidi ya Dortmund zikifuatiwa na kufungwa na Blackburn huku Van Persie akifanikiwa kufunga goli 1 katika mechi dhidi ya wajerumani. Mambo yalianza kwenda vizuri baada ya kufunga goli mbili zilizoisadia Arsenal kushinda 3-0 dhidi Bolton.

OCTOBER

GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
5(0)
4/0/1
7
7.50
Mwezi October  Van Persie alifakuwa na urafiki mzuri na magoli ya wapinzani. Baada ya kufungwa na Tottenham, nahodha wa Arsenal alifunga mabao mawili ya ushindi ya Sunderland , akafunga mawili tena katik mechi dhidi ya Stoke kabla ya kufunga hat trick katika london derby dhidi ya Chelsea. 
NOVEMBER

GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
4(1)
3/2/0
5
7.50
Hali ya hewa ikawa ya baridi ulipofika mwezi November lakini mdachi huyu akazidi kuwa wa moto. Baada ya kufunga goli katika ushindi wa 3-0 dhidi ya West brom @Emirates, Van Persie akafunga katika mechi ya tano mfululizo akitupia bao mbili za ushindi dhidi ya Norwich City na Dortmund huku Gunners wakianza kuirudisha form yao iliyokuwa imepotea.
DECEMBER

GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
6(0)
4/1/1
4
7.08
Magoliyakizidi kumwagika kwa Van Persie katika kipindi cha sikukuu, akifunga dhidi ya Wigan, kabla ya kutia kambani dhidi ya Everton na Aston Villa. Akakosa bao katika mechi dhidi ya Wolves, na sasa akawa anahitaji hat trick dhid ya QPR ili kuifikia rekodi ya Alan Shearer  ya kufunga mabao mengi katikA KALENDA YA mwaka wa premier league, lakini akafunga goli moja.

JANUARY
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
4(0)
1/0/3
4
6.75
 Gunners walianza mwaka 2012 na vipigo vitatu mfululizo, Van Persie akifunga dhidi ya Swansea na Man United. Baada ya kumuangalia Henry akifunga katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Leeds, Mdachi huyu alikwenda kufunga penati mbili katika mechi ya raundi ya nne dhidi ya Aston Villa.

FEBRUARY
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
6(0)
3/1/2
4
6.75
Mwezi mbaya, walianza na sare ya 0-0 dhidi ya Bolton, kabla ya mambo kubadilika na kushinda 7-1 dhidi ya Blackburn huku Van Persie akifunga hat tick kabla hawajaenda San Siro na kufungwa magoli manne kwa nunge. Baadae wakaja wakatolewa katika FA Cup baada ya kufungwa 2-0 na Sunderland. Mechi iliyofuatiwa walianza kufungwa 2-0 na Spurs pale Emirates kabla ya Pesie kurudisha na kwenda hafl time wakiwa wamelingana. Kipindi cha pili Walcott akaibuka shujaa baada ya kufunga mengine na kuifanya timu yake iibuke na ushindi wa 5-2.


MARCH
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
6(0)
5/0/1
4
6.75
Ushindi dhid ya Spur uliamsha cheche za ushindi za Arsenal. Van Persie akafunga goli muhimu dhdi ya Liverpool. Gunners wakakaribia kuushangaza ulimwengu baada ya kuifunga AC Milan 3-0 katika mchezo wa pili wa UCL huku Van Persie akifunga goli penati. Nahodha huyo pia alifunga goli la ushindi dhidi ya Newcastle ingawa mwezi huo uliisha kwa kipigo dhidi ya QPR.




APRIL

GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
4(0)
2/1/1
1
6.7
Form ya the Dutchman hivi karibuni imekuwa ya kawaida sana, akifunga goli moja  mpaka sasa ndani ya mwezi huu wa nne  katika dhidi ya Wolves.




                                        JUMLA YA TATHIMINI YOTE YA MIEZI 10
 SEASON'S TOTAL THUS FAR
GAMES PLAYED(SUBSTITUTE)
GAMES WON/DRAWN/LOST
GOALS SCORED
AVERAGE GOAL.COM PLAYER RATING
43(2)
26/7/12
34
6.94

RONALDINHO GAUCHO ! HUYU MTU ANA BALAA

Zinedine Zidane - Footballs Greatest document

MSAADA TUTANI: IANDIKIE CAPTION HII PICHA

GARI LA CHEKA MAUGO ILI HAPA

 Msemaji wa Mpambano wa Ngumi kati ya Mada Maugo na Francis Cheka , Yasini Abdallah akionesha mkana na gari atakalopewa mshindi wa mpambano huo.picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/
Johannes Lugenge kushoto na Promota wa Mpambano wa Mada Maugo na Francsis Cheka, Lucas Rutainurrwa wakionesha mkana wa Ubingwa wa I.B.F Afrika na gari atakalochukua bingwa wa mchezo huo Dar es salaam.picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/


Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi gari watakalogombania  Mabondia Mada Maugo Na Francis Cheka  Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D

HATIMAYE YANGA YAOMBA RADHI KWA KUMPIGA MWAMUZI


MKUTANO MKUU WA MWAKA 2011 WA TFF
Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) wa 2011 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umefanyika kwa siku mbili (Aprili 21-22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront na kuhudhuriwa na wajumbe 104. Mkutano ulipokea taarifa, kufanya uamuzi katika masuala mbalimbali na mengine yaliyojitokeza kama ifuatavyo;

EL MAAMRY, NDOLANGA WATUNUKIWA URAIS WA HESHIMA
AGM ilipitisha pendekezo la kuwatunuku urais wa heshima wa TFF, Alhaji Said Hamad El Maamry na Muhidin Ahamadi Ndolanga lililowasilishwa na Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Rais wa TFF, Leodegar Tenga.

Alhaji El Maamry ambaye ni mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) alikuwa Mwenyekiti wa TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) kuanzia mwaka 1973 hadi 1986. Alhaji Ndolanga aliongoza FAT kuanzia mwaka 1993 hadi 2004.

BAJETI YA MWAKA 2012
Bajeti ya Mwaka 2012 ya sh. 7,246,628,650 kwa ajili ya matumizi ya TFF ilipitishwa. Kwa mwaka 2012 TFF inatarajia kukusanya sh. 7,572,991,433 kupitia vyanzo mbalimbali.

Vyanzo hivyo ni viingilio vya uwanjani vinavyotarajiwa kuingiza asilimia 22 ya mapato yote, udhamini (asilimia 74) na vyanzo vingine kama haki za matangazo ya televisheni, ada za ushiriki wa timu katika mashindano mbalimbali, misaada kutoka FIFA na CAF ambayo kwa pamoja vinatarajiwa kuingiza asilimia nne ya mapato yote.

KAMATI YA LIGI YA TFF
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaendelea na mchakato wa kupendekeza mifumo mitatu tofauti ya chombo kitakachosimamia/kuendesha Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ikieleza faida na athari za kila mfumo uliopendekezwa na baadaye kuwafanya mawasilisho (presentation) kwenye Kamati ya Utendaji.

Baada ya kuwasilisha mifumo hiyo kwa Kamati ya Utendaji, Kamati ya Ligi itapendekeza mfumo upi kati yao hiyo inaoona unafaa kabla ya kufanyika uamuzi wa mwisho.

Lengo la kuunda chombo maalumu cha kuendesha ligi ni kuongeza ufanishi katika uendeshaji wa VPL na FDL, na pia kuifanya Sekretarieti ya TFF kushughulikia zaidi shughuli za maendeleo.

UUZWAJI WA TIMU
Uuzaji wa timu linabaki kuwa suala la kisheria. Lakini TFF imeweka utaratibu ufuatao; lazima Mkutano Mkuu wa klabu husika uidhinishe uuzaji, na timu ikishauzwa inabaki katika mkoa husika.

MFUMO WA MASHINDANO
Kwa vile kuna tatizo la ligi mbalimbali kuwa fupi, hali inayosababisha baadhi ya wachezaji katika madaraja ya chini kucheza ligi zaidi ya moja katika msimu mmoja, mfumo wa ligi/mashindano utaangaliwa upya.

Mfumo uliopo sasa uliwekwa kwa ajili ya kuvutia uwekezaji katika mpira wa miguu ambapo mwekezaji anaweza kuanzisha timu, na ndani ya miaka mitatu ikacheza Ligi Kuu. Pili, ilikuwa ni kuondoa mlolongo mrefu wa ligi, na kuwafanya wanachama wa TFF (mikoa) nao kuendesha ligi zao mikoani.

Ijulikane kuwa ligi za mikoa (regional leagues) zinachezwa. Kwa sababu TFF inaendeshwa kwa mfumo wa shirikisho (federation), nia ni wanachama wa federation nao kuwa na majukumu ya kusimamia na kuendesha ligi, kwa vile TFF haiwezi kusimamia ligi zote.

MAREKEBISHO YA KATIBA
Mkutano Mkuu wa TFF umepitisha marekebisho ya Katiba katika maeneo mawili; moja ni kuanzisha Baraza la Wadhamini ambalo linatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua watatu na wasiozidi watano.

Marekebisho mengine ni kuongeza idadi ya kanda kutoka kumi na moja za sasa hadi 13. Marekebisho hayo yamefanyika kutokana na Serikali kuongeza mikoa mipya ya kijiografia.

Kanda mpya sasa zitakuwa Kagera/Geita, Arusha/Manyara, Kilimanjaro/Tanga, Katavi/Rukwa, Njombe/Ruvuma, Dodoma/Singida, Dar es Salaam, Shinyanga/Simiyu, Mwanza/Mara, Lindi/Mtwara, Kigoma/Tabora, Mbeya/Iringa na Pwani/Morogoro.

Ukiondoa mamlaka ya uteuzi aliyonayo Rais kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji huchaguliwa kwa kanda.

HESABU ZILIZOKAGULIWA
Mkutano Mkuu ulipitisha hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2010 (Audited Accounts) , na pia kuiteua kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya TAC Associates kuwa mkaguzi wa hesabu za TFF kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

YANGA YAOMBA RADHI MKUTANO MKUU
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambaye pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF akiwakilisha klabu za Mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Bhinda aliwaomba radhi wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kitendo cha wachezaji wake kumpiga mwamuzi Israel Nkongo kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu.

Pia alimuomba Rais wa TFF, Leodegar Tenga kutoa msamaha wa adhabu ya kulipa faini iliyotolewa na Kamati ya Ligi ya TFF kwa wachezaji wawili wa Yanga ambao mpaka sasa hawajalipa faini hiyo.

Rais Tenga alimshukuru Bhinda kwa ujasiri alioonesha wa kuomba radhi mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa kitendo kile. Aliongeza kuwa kwa vile yeye ni muumini wa kanuni, na adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni hawezi kutoa msamaha, hivyo wachezaji hao walipe faini hizo.

Pia Rais Tenga alisema binafsi haziingilia kamati za TFF katika uamuzi ambao zinafanya kwa vile zina watu waadilifu, na angekuwa yeye binafsi ndiye anayetoa adhabu, angetoa adhabu kali zaidi kwa vile vitendo vya kupiga waamuzi havikubaliki katika mchezo wa mpira wa miguu.

KANUNI ZA NIDHAMU, MAHAKAMA YA USULUHISHI
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Rais Tenga aliwaambia wajumbe kuwa Kanuni za Nidhamu (Disciplinary Code) za TFF na uundaji wa Mahakama ya Usuluhishi (Arbitration Tribunal) ya TFF ambacho ndicho kitakuwa chombo cha juu cha kutoa haki kwa masuala ya mpira wa miguu nchini vitakamilika mwaka huu.

Pia TFF itaendelea kutafuta wadhamini kwa ajili ya timu za Taifa za vijana na wanawake, itaendelea kuendesha semina na makongamano katika nyanja mbalimbali za mpira wa miguu, kutengeneza mtaala wa academy na kutengeneza mpango wa maendeleo (Comprehensive Plan) baada ya ule wa awali kumalizika mwaka huu.

MBWANA SAMATTA AREJEA UWANJANI, TP MAZEMBE IKIIFUNGA LUPOPO BAO 1:0



Van Persie atwaa tuzo ya mwanasoka bora wa kulipwa.

Naye beki wa kulia wa Totenham Hotspurs Kyle Walker alichaguliwa mwanasoka bora kijana akiwashinda Sergio Aguero na Danny Welbeck.

Premier League team of the year:

Joe Hart (Man City), Kyle Walker (Tottenham), Vincent Kompany (Man City), Fabricio Coloccini (Newcastle), Leighton Baines (Everton), David Silva (Man City), Yaya Toure (Man City), Gareth Bale (Tottenham), Scott Parker (Tottenham), Robin van Persie (Arsenal), Wayne Rooney (Man Utd).

Championship team:

 Kelvin Davis (Southampton), Nathaniel Clyne (Crystal Palace), James Tomkins (West Ham), Curtis Davies (Birmingham), Ian Harte (Reading), Adam Lallana (Southampton), Peter Whittingham (Cardiff), Mark Noble (West Ham), Matt Phillips (Blackpool), Rickie Lambert (Southampton), Jay Rodriguez (Burnley).

UPEPO UMEBADILIKA: UNITED WAMEWEKA UBINGWA REHANI - DERBY KUAMUA BINGWA - FERGUSON ASEMA ITAKUWA MECHI YAKE MUHIMU KULIKO ZOTE KATIKA MAISHA YAKE.


Hatimaye zimebakia pointi 3 tu zinazowatenganisha mahasimu wawili katika kuelekea mwishoni mwa mbio za ubingwa wa ligi kuu ya England.  Jambo hili linaufanya mchezo wa jumatatu ijayo uwe mtamu zaidi katika historia ya upinzani kati ya Manchester United na Manchester City.

Kiukweli hivi sasa Roberto Mancini hawezi tena kujifanyisha kwamba City hawana nafasi ya kubeba taji na usiku huu muitaliano huyo atakuwa akigongesha glass na Stevn Pienaar huku akiwa na mawazo ya Manchester Derby jumatatu ijayo.

Siku zote ilikuwa ikionekana kwamba mchezo huu wa jumatatu ya tarehe 30 ndio utaamua ubingwa pamoja na mabadiliko ya mapishano ya pointi katika mbio hizi ambazo tangu mwanzoni mwa msimu zimekuwa zikiongozwa na vilabu hivi vya Manchester.

City wataenda katika mchezo huo pale Etihad Stadium wakijua kwamba ushindi wa mara 3 katika michezo yao ya mwisho utakuwa unatosha sana kuwafanya wawe mabingwa wa premier league kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 44. Wana wastani mzuri wa magoli dhidi ya majirani zao - tofauti ya magoli 6 - kwa maana watakuwa on top hata kama watafungana pointi na United mwishoni mwa msimu.

Haikuwa ikionekana mambo yatakuwa hivi wakati zikiwa zimebaki dakika 7 za kucheza pale Old Trafford leo jumapili na United wakiongoza 4-2 dhidi ya Everton. Kwa muda huo, Sir Alex Ferguson inawezekana alikuwa akifikiria namna ya kwenda kubeba ubingwa pale pale nyumbani kwa majirani zake wapiga kelele kama anavyowaita.

Lakini magoli mawili kutoka Nikica Jelavic na Pienaar yalibadilisha kila kitu, na mbio za ubingwa, matokeo yakawa 4-4 katika ubao wa matokeo mwishoni mwa mchezo na kuwarudisha City katika mbio hizo ambazo zilionekana zinakaribia kuisha.

Wakati City walipofungwa na Arsenal April 8, walikuwa nyuma kwa pointi 8 nyuma ya United huku ikiwa imebakia michezo 6 ya kucheza. Maswali yalielekezwa kwa Mancini na hatma yake wakati baadhi ya mashabiki wa United walitengeneza t-shirts za kusherekea ubingwa wa 20.

Wiki 6 kabla ya kuisha kwa msimu, kila mtu alidhani muda ulikuwa bado, lakini hakuna aliyefikiri wala kutegemea United wataachia mahasimu wao kurudi katika mbio za ubingwa kirahisi hivyo. City walicheza vizuri na kuutumia udhaifu na makosa ya United leo na kuwafunga Wolves na kubakisha pointi 3 kabla ya derby yao pale Etihad.

"Tumewapa City dhumuni la kupigana zaidi, hakuna mashaka juu ya hilo. Makosa yetu ya leo yameufanya mchezo wa Etihad kuwa derby muhimu zaidi katika maisha yangu hapa Old Trafford. Mechi itaamua kila kitu. Tumejitengenezea mazingira magumu wenyewe - lakini tutaenda pale kwao tukiwa tunajua tuna uwezo wa kupata matokeo mazuri dhidi yao." - Alikaririwa Ferguson leo baada ya mechi.

Ama kwa hakika sasa mambo yamegeuka, na derby ya manchester itakuwa vita kubwa kuliko zote ambazo timu hizi mbili zimewahi kupigana. City watamkosa kiungo wao na roho ya safu ya kiungo Yaya Toure ambaye leo amepata kadi ya njano ya tano hivyo ataukosa mchezo. Hii itakuwa derby itakayofanana na El Clasico ya jana.
Ukiachana na Derby - City wamebakisha mechi dhid ya Newcastle @Sports Direct Arena na watamaliza dhidi ya QPR pale Etihad Stadium. Huku United wenyewe wakiwa wamebakia na mchezo dhidi ya Swansea City pale Old Trafford na watamaliza ugenini  dhidi ya Sunderland.
 

Sunday, April 22, 2012

HATIMAYE NIZAR KHALFAN ATUA MSIMBAZI - KUANZA KUICHEZEA SIMBA MSIMU UJAO


KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliyekuwa anacheza soka ya kulipwa Marekani, amejiunga rasmi na `Mabingwa Watarajiwa’ wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, Simba.
Habari za kutoka ndani ya klabu hiyo ambazo zimeenea zinasema kuwa, usajili wa mchezaji huyo umefanikishwa na mmoja wa wafadhili wa zamani wa klabu hiyo, Azim Dewji.
Dewji mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia hilo, alikiri na kusema kuwa, aliombwa na uongozi wa Simba kufanikisha usajili wa mchezaji huyo na kwamba baada ya kufanikiwa, ameshamkabidhi Nizar kwa uongozi wa klabu.
“Kama Mwanasimba, nimetimiza wajibu wangu kama nilivyokuwa nimeombwa na uongozi. Nimeambiwa ataungana na wenzake kuanza mazoezi wakati wowote kuanzia Jumatatu (leo),” alisema na kuongeza kuwa, mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Moro United atakuwa na nafasi ya kuanza kuichezea Simba katika michuano ya kimataifa mwaka huu endapo itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Baada ya kuzing’oa ya Kiyovu ya Rwanda na Setif ya Algeria, wiki hii Simba itaishukia Al Ahly Shandy ya Sudan na kama ikifanikiwa kuvuka kiunzi hicho, itaingia katika raundi nyingine itakayoamua timu za kucheza Nane Bora Afrika.
Habari zaidi zinasema kuwa, Nizar leo atakabidhiwa rasmi jezi atakayoitumia akiwa Simba. Atakabidhiwa jezi hiyo siku moja kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Moro United unaotarajiwa kuanza saa kumi alasiri.
Mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hata hivyo hakuwa tayari kutajwa jina akisema si msemaji, alikiri kukamilika kwa taratibu za Nizar kutua Simba huku akiongeza kuwa, ataisaidia klabu hiyo katika michuano ya ligi na ile ya kimataifa kuanzia msimu ujao.
“Ni kweli, timu inazidi kuimarika. Kumpata staa wa kimataifa kama Nizar ni jambo la kujivunia, tunashukuru kwa juhudi zilizofanyika na hatimaye kumpata mchezaji huyu,” alisema.
Nizar ambaye Juni 21 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 24, kabla ya kutua Simba aliichezea Philadelphia Union ya Ligi Kuu ya Marekani aliyodumu nayo kwa miezi mitatu tu baada ya kujiunga nayo akitokea Vancouver Whitecaps. Alikuwa Vancouver tangu Agosti 22, mwaka 2009 akitokea Moro United.
Katika soka ya ushindani, nyota huyo aliibukia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2004 na baadaye akajiunga na Mtibwa Sugar kabla ya kutimkia Kuwait kuichezea Al Tadamon ya huko msimu wa 2007-2008. Kutoka Tadamon alikwenda Lebanon na kuichezea Tadamon Sour ya huko na mwaka 2009 aliichezea Moro United.
 
SOURCE:http://bongostaz.blogspot.com/

MANCHESTER UNITED WAUWEKA UBINGWA WAO REHANI - WATOKA SARE NA EVERTON HUKU ROONEY AKIMFIKIA GEORGE BEST


Manchester United vs Everton 4:4 HIGHLIGHTS by maidb7abc

YANGA YAIFUNGA POLISI MABAO 3-1

 Mchezaji wa Yanga Haruna Niyonzima akikokota mpira mbele ya beki wa timu ya Polisi Dodoma Idd Ramadhan wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Vodacom unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, mpaka sasa ni kipindi cha pili na yanga imefanikiwa kuongoza katika vipindi vyote baada ya kupata magoli matatu  kupitia kwa wachezaji wake Davis Mwape magoli mawili  na Idrisa R.Senga goli moja na sasa inaongoza 3-0 dhidi ya Polisi Dodoma  .
 Wachezaji wa Yanga na Polisi Dodoma wakipeana mikono kama ishara ya kusalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Leo mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa uchache katika uwanja wa taifa, huenda hii inatokana na mwenendo wa timu hiyo katika michezo yake ya hivi karibun, ambapo imepoteza matumaini ya kuchukua ubungwa na hata nafasi ya pili, Yanga ndiyo walikuwa mabingwa watetezi wa kombe la  ligi kuu ya Vodacom walilochukua mwaka jana.
 
MABAO YA YANGA KWENYE MCHEZO WA LEO YAMEFUNGWA NA DAVIS MWAPE ( 2 ) NA IDRISSA RASHID.

NIZAR KHALFAN ATUA SIMBA SC


Nizar alipokuwa Marekani


KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliyekuwa anacheza soka ya kulipwa Marekani, amejiunga rasmi na `Mabingwa Watarajiwa’ wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, Simba.
Habari za kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa, usajili wa mchezaji huyo umefanikishwa na mmoja wa wafadhili wa zamani wa klabu hiyo, Azim Dewji.
Dewji mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia hilo, alikiri na kusema kuwa, aliombwa na uongozi wa Simba kufanikisha usajili wa mchezaji huyo na kwamba baada ya kufanikiwa, ameshamkabidhi Nizar kwa uongozi wa klabu.
“Kama Mwanasimba, nimetimiza wajibu wangu kama nilivyokuwa nimeombwa na uongozi. Nimeambiwa ataungana na wenzake kuanza mazoezi wakati wowote kuanzia Jumatatu (leo),” alisema na kuongeza kuwa, mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Moro United atakuwa na nafasi ya kuanza kuichezea Simba katika michuano ya kimataifa mwaka huu endapo itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Baada ya kuzing’oa ya Kiyovu ya Rwanda na Setif ya Algeria, wiki hii Simba itaishukia Al Ahly Shandy ya Sudan na kama ikifanikiwa kuvuka kiunzi hicho, itaingia katika raundi nyingine itakayoamua timu za kucheza Nane Bora Afrika.
Habari zaidi zinasema kuwa, Nizar leo atakabidhiwa rasmi jezi atakayoitumia akiwa Simba. Atakabidhiwa jezi hiyo siku moja kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Moro United unaotarajiwa kuanza saa kumi alasiri.
Mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hata hivyo hakuwa tayari kutajwa jina akisema si msemaji, alikiri kukamilika kwa taratibu za Nizar kutua Simba huku akiongeza kuwa, ataisaidia klabu hiyo katika michuano ya ligi na ile ya kimataifa kuanzia msimu ujao.
“Ni kweli, timu inazidi kuimarika. Kumpata staa wa kimataifa kama Nizar ni jambo la kujivunia, tunashukuru kwa juhudi zilizofanyika na hatimaye kumpata mchezaji huyu,” alisema.
Nizar ambaye Juni 21 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 24, kabla ya kutua Simba aliichezea Philadelphia Union ya Ligi Kuu ya Marekani aliyodumu nayo kwa miezi mitatu tu baada ya kujiunga nayo akitokea Vancouver Whitecaps. Alikuwa Vancouver tangu Agosti 22, mwaka 2009 akitokea Moro United.
Katika soka ya ushindani, nyota huyo aliibukia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2004 na baadaye akajiunga na Mtibwa Sugar kabla ya kutimkia Kuwait kuichezea Al Tadamon ya huko msimu wa 2007-2008. Kutoka Tadamon alikwenda Lebanon na kuichezea Tadamon Sour ya huko na mwaka 2009 aliichezea Moro United.