Search This Blog

Tuesday, April 24, 2012

ITS ALMOST DONE..... SIMBA YAKARIBIA BINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE 2012


WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC jioni hii wamejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuifunga Moro United ya Morogoro maba 3-0 na mechi ya wapinzani wao katika mbio za ubingwa,  Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ikivunjika timu hizo zikiwa zimefungana 1-1, Uwanja wa Azam, Chamazi.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Patrick Mutesa Mafisango, Haruna Moshi Shaaban 'Boban' na Felix Mumba Sunzu Jr.
Simba sasa imetimiza pointi 59, ambazo kutokana na matokeo ya leo ya sare ya 1-1 kati ya azam na Mtibwa, haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Lakini kujiweka salama, Simba itahitaji japo polnti moja katika mechi zake tatu zilizobaki. 
Mchezo kati ya Azam na Mtibwa ulivunjika wakati beki Salum Swedi amekwishaifungia bao Mtibwa na Mrisho Khalfan Ngassa ameifungia Azam FC. Mtibwa waligomea mechi hiyo wakipinga Azam kupewa penalti. Sasa Kamati ya Ligi Kuu itakutana kesho na kutoa uamuzi, lakini kuna uwezekano mkubwa Mtibwa ikatozwa faini na wapinzani wao kupewa ushindi.



Nafasi
TimuMPWDLGFGA+/-Pts
1 Simba SC25185242123059
2 Azam23155334112350
3 Young Africans24154538211749
4 Mtibwa Sugar2310583125635
5 Coastal Union24102122429-532
6 Kagera Sugar2471072525031
7 JKT Ruvu2471072530-531
8 Ruvu Shooting247982019130
9 JKT Oljoro237881620-429
10 Toto African2451182327-426
11 African Lyon2458112029-923
12 Villa Squad2465132643-1723
13 Moro United25310122744-1719
14 Polisi Dodoma2538141834-1617

3 comments:

  1. Kichwa cha habari umerekebisha kutoka kile cha jana, Thats good! But contents bado kaka, Simba wamebakiza mechi tatu kivipi kaka?

    ReplyDelete
  2. Kaka hao YANGA wamepata point 49 lini? wanaubavu huo? baada kumfunga Polisi dom (Kibonde) wana point 46. Badili kaka wanatamba huku

    ReplyDelete
  3. Kaka Shafii, inasikitisha kuona kila siku mechi zinazoingia dosari ni dhidi ya AZAM? Nadhani hiyo inaashiria kuwa hiyo ni kashfa ya upangaji matokeo hivyo ifike wakati TFF wachunguze kupitia kamati zake na ikibainika ni kweli AZAM anahusika sheria ichukue mkondo wake dhidi ya waamuzi wliohusika pamoja na timu husika ikiwemo kushushwa daraja kama JUVENTUS walivyofanyiwa pale Italy.YANGA Vs AZAM,POLISI Vs AZAM na AZAM Vs MTIBWA SUGAR,Cha kusikitisha TFF wame "relax" na huo mwenendo!!!

    Ni maoni tu,
    Edger,Iringa.

    ReplyDelete