Masaa 24 baada ya vyombo vya habari vya Uingereza kuripoti kwamba kiungo wa Bayern Munich Toni Kroos yupo tayari kuhamia Manchester United kutoka Munich katika kipindi cha usajili kijacho, leo hii wakala wa mchezaji huyo amezungumza na kuweka wazi kuhusu taarifa hizo.
Bild, gazeti la Ujerumani, limeripoti kwamba wakala wa Kroos, Volker Struth ametoa taarifa ambayo itawavuja moyo washabiki wengi wa United. Struth aliiambia Bild:
"Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukisikia kuhusu hizi tetesi na tukaamua kukaa kimya. Lakini mpaka sasa naamini Toni atabaki Allianz Arena mpaka 2015."
Kroos ana mkataba na Bayern mpaka 2015, lakini mapaka sasa amegoma kuongeza mkataba mpya na Bayern. Anaripotiwa kulipwa €86,000 kwa wiki, na amekuwa akiripotiwa kutaka mara mbili ya fedha anayolipwa sasa ili aendelee kubaki klabu hapo.
No comments:
Post a Comment