Ule usiku Champions league unarudi tena leo katika hatua ya robo fainali ya michuano. Dunia ya mashabiki wa soka itaelekeza macho na masikio katika viwanja vya Old Trafford na Camp Nou katika michezo kati ya Manchester United vs Bayern Munich na FC Barcelona vs Atletico Madrid.
Manchester United vs Bayern Munich
Draw yoyote ambayo Manchester United wangepata isingekuwa rahisi. Pamoja na kuwatoa Olympiakos kwenye kwenye hatua ya mtoano, ni ngumu kuamini kuwa united iko imara kuleta upinzani kwenye timu kubwa na ni fair kusema ndio weakest side (timu dhaifu) still in the competition. Draw against timu nyingine ambayo ingeleta hope kidogo kwa united ingeweza kuwa Borussia Dortmund, japo nao si timu ya kubeza lakini walau united wangejipa matumaini kidogo ya kuingia nusu fainali especially wangepangiwa second leg Old Trafford.
Instead, wamepata draw ambayo mashabiki wa united watakubaliana na mimi nikisema ni worst draw for long time dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich huku first leg ikifanyika Old Trafford.
Ni vizuri kuwa positive ukizingatia kwenye football maamuzi ni dakika 90, lakini pressure kubwa ipo kwa David Moyes na kikosi chake huku Bayern wakiwa favourite.
United wana historia nzuri kiasi na Bayern, ukikumbuka ushindi wa mwaka 1999 ambapo United waliwafunga Bayern na kutwaa ubingwa wa ulaya thanks to super sub Ole Gunnar Solskjaer na Teddy Sheringham.
TAKWIMU
Manchester United wana rekodi ya kushinda mechi 6 za mwisho walizocheza na timu kutoka Bundesliga na rekodi yao ya kiujumla dhidi ya timu za kijerumani wanapocheza Old Trafford - wameshinda mara 8, safe 3 na wamepoteza mechi 2. Rekodi yao ya ugenini na nyumbani ipo hivi ushindi mechi 14, sare 7 na kufungwa 6.
Bayern wanasaka ushindi wa tano mfululizo katika ardhi ya UK. Msimu huu walishinda 3-1 dhidi ya Man City katika makundi na wakaifunga 2-0 Arsenal katika hatua ya 16 bora. Msimu uliopita, walishinda 301 dhidi ya Arsenal katika hatua ya 16 bora kabla ya kurudi England katika dimba la Wembley kuwamaliza wajerumani wenzao 2-1 katika Fainali ya UCL.
Rekodi ya Bayern dhidi ya timu za kiingereza ipo hivi W16 D15 L12.
Bayern hawajapoteza mechi msimu huu - Je United itavunja mwiko huu?
Barcelona vs Atletico Madrid
Barca wameingia kwenye Champions League wakiwa ni moja ya interesting team. Ila kwa performance yao ilivyo mwaka huu, ni ngumu kusema moja kwa moja kuwa ni favourite, japokuwa chochote kinaweza kutokea ukichukua reference mwaka 2009 na 2011.
Baada ya kuwatoa Man City kwenye raundi iliyopita, timu ambayo Barca walikuwa wakiihofia zaidi kukutana nayo ni Bayern Munich, wamepata draw against Atletico Madrid timu ambayo inaonesha kuwasumbua zaidi Barca recently na sasa wanachuana vikali kwenye top position ya La liga wa msimu huu, Atletico hawajapoteza mechi yoyote dhidi ya Barca (wamepata draw tatu) hali ambayo inawapa extra confidence kwa maana wanaweza ku progress to semi finals kama watapata draw mbili ambazo zitawa favour na away goals, pia wachezaji hatari wa Atletico kama Diego Costa na Koke wanaongeza confidence kuwa watashinda dhidi ya Barcelona.
Lakini ikumbukwe kwamba hapa tunaongelea Barca, bingwa mara 3 kombe hili, pia wana kikosi imara na chenye uzoefu wa kufanya lolote lile ndani ya dk 90, hapa bila shaka huwezi kuacha kulitaja jina la Lionel Messi ambaye ana rekodi ya kuifunga Atletico Madrid magoli mengi kuliko timu nyingine yeyote.
TAKWIMU
FC Barcelona wana rekodi ya kushinda mara 4 na kufungwa mara 5 katika mechi 9 dhidi ya timu za Hispania katika michuano ya UEFA. Pia walipoteza fainali ya mwaka 2006 ya UEFA Super Cup kwa kipigo cha 3-0 kwa Sevilla FC in Monaco.
Atlético hawajawahi kufika kwenye hatua hii katika michuano ya UCL tang msimu wa 1996/97 walipofungwa na AFC Ajax. Rekodi ya Atletico katika robo fainali ni ushindi wa me chi 3 na wamefungwa mara 2 kutoka katika robo fainali 5.
No comments:
Post a Comment