Na Baraka Mpenja, Dar
Es salaam
VINARA wa ligi kuu
soka Tanzania bara, Azam fc wanaingia kwenye mechi muhimu leo hii dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Mabatini
Mlandizi Mkoani Pwani.
Mechi hii ilitakiwa
kuchezwa jana, lakini iliahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha katika mji
wa Mlandizi na kuufanya uwanja wa Mabatini kujaa maji mithiri ya bwawa.
Azam fc wanaingia
katika mchezo wa leo wakiwa na `presha` ya kutafuta matokeo kwa jinsi yoyote
ile kwasababu ushindi wa mabao 2-1 walioupata mabingwa watetezi, Young Africans
jana uwanjanja wa Taifa dhidiya Kagera Sugar unawatishia amani katika mbio zao
za kutwaa ubingwa.
Sasa Azam wana pointi
53 pointi moja mbele ya Yanga, lakini wao wana mchezo wa leo mkononi.
Endapo wana
Lambalamba watashinda mechi hii, basi watakuwa wanahitaji pointi tatu pekee
katika michezo miwili itakayosalia dhidi ya Mbeya City na JKT Ruvu.
Ushindi utawafanya
Azam wafikishe pointi 56 kileleni na wakishinda mechi nyingine watafikisha
pointi 59 ambazo hazitaweza kufikiwa na Yanga hata kama watashinda mechi zote.
Yanga anahitaji
kutetea ubingwa wao, hivyo ni watumwa kwa Azam fc kwasababu wanahitaji kushinda
mechi zote na kuwaombea dua mbaya Azam fc katika mechi zao.
Baada ya mechi ya
jana, Yanga watakabiliana na JKT Oljoro mwishoni mwa wiki katika dimba la CCM
Shk. Amri Abeid jijini Arusha, na kibarua chao cha mwisho ni dhidi ya Simba
uwanja wa Taifa.
Mechi ya Azam fc leo
hii itakuwa ngumu kutokana na mazingira ya aina tofauti.
Ruvu Shooting
wanahitaji heshima mbele ya Azam fc ambao mpaka sasa hawajapoteza mchezo leo.
Hata kama Shooting
hawahitaji ubingwa wala nafasi pili na tatu, watapambana kuhakikisha wanafanya
vizuri na kuweka rekodi ya kumtandika kocha Joseph Marius Omog kwa mara ya
kwanza tangu aanze kazi ya kuinoa klabu hiyo katika michuano ya ligi kuu.
Hata hivyo, Shooting
wanatakiwa kujipanga vizuri kutokana na kikosi cha Azam fc kuwa katika morali
kubwa ya kutwaa ubingwa wao.
Kama vijana wa Omog
watafanikiwa kutwaa ubingwa, Azam fc wataandika historia mpya katika maisha yao
ya soka, kwasababu ndio yatakuwa mafanikio makubwa zaidi kwasasa.
Kutwaa ubingwa wa
kombe la Mapinduzi mara mbili zio ishu kwa Azam fc, ila ubingwa wa michuano
mikubwa ya ligi kuu ndio ndoto yao pekee msimu huu.
Hawahitaji nafasi ya
pili kwasababu wameshaipta zaidi ya misimu miwili, kwahiyo wao wanapambana
kutafuta ubingwa tu.
Kwa mazingira haya ya
Azam fc, Ruvu Shooting wanatakiwa kujipanga vizuri kuwazuia watu hawa wenye nia
ya dhati kusaka pointi tatu muhimu.
Haitakuwa kazi
nyepese kukabilina na kikosi cha Azam fc chenye mchangayiko wa wachezaji wenye
uzoefu na wakongwe.
Japokuwa watakosa
hudumza za Sami Haji Nuhu, Bryson Raphael, Joseph Kimwaga na baadhi ya
wachezaji wengine wenye majeruhi ya muda mrefu, bado Azam wana wachezaji
wengine wanaoweza kuamua matokeo siku ya leo.
Mlinda mlango
Chipukiza Aishi Manula anaweza kuanza leo hii langoni, huku beki wa kulia
akisimama mkongwe Erasto Nyoni.
Beki wa kushoto bila
shaka atasimama bwana mdogo Gadiel Michael, beki namba nne David Mwantika huku kitasa
akila Agrey Moris.
Omog anaweza
kumuanzisha Michael Bolou katika nafasi ya kiungo wa Ulinzi, wakati winga wa
kulia Himid Mao anaweza kuanza.
Namba 8 kwa asilimia
zote Salum Abubakar ataanza kwasababu hana mpinzani katika kikosi hicho, labda
kama akikumbwa na majeruhi.
Mshambuliaji wa kati,
Gaudence Mwaikimba anaweza kuanza, huku nahodha John Bocco `Adebayor` akicheza
namba kumi.
Winga wa kushoto
anaweza kuanza Kipre Herman Tchetche anaweza kuanza tofauti na mechi za nyuma.
Kwanini Omog anaweza
kuwatumia washambuliaji watatu kwa wakati mmoja?, sababu kubwa ni kutafuta mabao
kwani ushindi pekee ndio matokeo ya maana kwake.
Watalazimika
kushambulia kwa wakati wote ili kupata mabao ya mapema na kuibuka na pointi
tatu muhimu.
Pia wapo wachezaji
wengine wanaoweza kutokea benchi ambao ni Mwadini Ally, Said Morad, Jabir Aziz, Brian Umony, Kelvin Friday, Mudathir Yahya, na Khamis Mcha.
Kwa aina hii ya wachezaji wa Azam fc wanaotarajia
kucheza leo, Ruvu Shooting watahitaji kutumia akili za ziada kuwazuia wasipate
ushindi.
azam washafungwa kabla mpira kuanza leo lazma azam afungwe akitaka asitake bado mtoto mdogo wakuibabaisha yanga africa tim bora tanzania
ReplyDeleteAzam ndiye mpya,mliharibu timu yenu kwa kuwasajili Okwi na Ngassa na faida yake ni kukosa ubingwa
ReplyDelete