Search This Blog

Thursday, April 3, 2014

MAKALA: JE EVRA ANAWEZA KUFUATA NYAYO ZA PHILIPH LAHM KUHAMIA KWENYE KIUNGO?

Kuwaondoa wachezaji watatu wakongwe mwishoni mwa msimu  (Nemanja Vidic, Rio Ferdinand na Patrice Evra) inaweza kuleta balaa kwa Manchester United. Wakati Ferdinand na Vidic wamekuwa wakiandamwa na majeruhi hasa kwa upande wa Ferdinand, Evra, kwa kutokuwa na majeruhi na consistency aliyonayo, bado ni chaguo la kwanza katika kikosi cha kwanza. Je ni kweli beki wa pembeni ambaye ni mzuri sana katika kushambulia na mwenye uzoefu mkubwa wa kucheza na kuongoza wenzie hana mahala kwa kwenda pindi anapopoteza kasi kidogo? Lakini kiwango cha Philip Lahm kinaonyesha hali tofauti.

Evra na Lahm tunawafananisha vipi? Katika uzuiaji, Evra amefanikiwa kwa asilimia 50 zaidi katika tackling kuliko Lahm msimu huu, kafanya interceptions asilimia 30% zaidi ya Lahm. Ingawa Lahm amefanikiwa zaidi katika upigaji wa pasi, lakini pia Evra ameokoa mara 5 zaidi ya nahodha wa Bayern, katika kuangalia tofauti yao kulingana na majukumu ya nafasi wanazocheza. Katika ushambuliaji - Evra amefanikiwa kufanya driblling zaidi ya Lahm ingawa anazidiwa kwenye key passes.
  

Ingawa takwimu hazifanani kutoka na nafasi tofauti wanazocheza, wachezaji wote wawili walikuwa bora kabisa kwenye nafasi zao wakati walipokuwa kwenye viwango vyao vya juu kabisa na wote wana uwiano mzuri wa kushambulia na kuzuia. Wakati Lahm anaweza kuwa katika kupiga pasi, Evra na nguvu zaidi hewani, na kasi na uwezo kufanya dribbling zaidi.

Je ni namna gani Evra anaweza kufiti katika kiungo? Katika mfumo wa 4-1-4-1? Hapana, lakini katika mfumo wa 4 2 3 1 kwa pamoja na Michael Carrick, Darren Fletcher au Maruoane Fellaini. Hahitaji kuwa  Paul Scholes kupiga mipira mirefu kutoka kona moja ya uwanja mpaka nyingine, au kuwa kama Roy Keane katika ukabaji lakini hatokuwa na ulazima kufanya tackles dhidi ya mawinga wenye kasi. Kasi yake, ubunifu, stamina, aggression, uzoefu ni sifa nzuri zinazohitajika kwa kiungo yoyote, Man Utd wanahitaji sana mtu mwenye sifa hizo. 

Kama tulivyoona usiku wa Jumanne, United wanaweza wasihitaji sana kuangalia mbali kupata mtu wa kuvaa viatu vya Evra. Katika mechi iliyopewa jina la utani  David vs.Goliath, kiwango cha Buttner’ kilimtuliza Arjen Robben kwa kiasi fulani, uizingatia uzoefu wake wa mechi kubwa kama zile Buttner alijitahidi sana. Ingawa mechi moja inaweza isiwe kipimo (unakumbuka ya Macheda 2009) lakini bado anastahili pongezi kwa jitihada zake na anastahili kupewa nafasi ili aonyeshe uwezo kama ataweza kurithi nafasi ya Evra kwa kuwa na consistency.

Kwa upande mwingine Evra anaweza kuleta ubunifu kwenye kiungo pembeni ya Fletcher, Carrick auana nguvu hewani, mzuri kwenye tacklin, na uzoefu, stamina na mzuri katika kuhamasisha timu. Pia kwa upande mwingine United wanaweza kumuacha Evra aondoke na kuendeleza kujaza listi ya wachezaji wa kusajili......kumchezesha Evra kati inaweza kuwa plan nzuri, inaweza pia isikubali kama ilivyokubali kwa Lahm, lakini Moyes hana cha kupoteza. 

No comments:

Post a Comment