Search This Blog

Monday, April 7, 2014

EXCLUSIVE: TAARIFA RASMI YA ETOILE DU SAHEL KUHUSU MGOGORO WAO NA OKWI - NA KWANINI WANAMDAI FIDIA YA ZAIDI YA BILLIONI 1.

Klabu ya Etoile Du Sahel imetoa taarifa rasmi kuhusu sakata lake na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi anayekipiga katika klabu ya Yanga.

Mtandao huu umefanikiwa kupata barua rasmi ya Etoile kwenda FIFA wakimshtaki rasmi Okwi kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na hivyo kutaka walipwe fidia.

Katika barua hiyo Etoile wanaeleza: "Mwanzoni kabisa alipoanza kuitumikia klabu, hatukuona tabia yoyote isiyoridhisha kutoka kwake, alishiriki kwenye baadhi ya mechi rasmi za mashindano na timu ya wakubwa na nyingine kadhaa kikosi cha U23, alilipwa mishahara yake pamoja na bonasi kulingana na makubaliano ya mkataba, sheria na kanuni za FIFA na shirikisho la soka la Tunisia. 

"Baadae tukagundua mabadiliko kwenye tabia yake, ilikuwa mwanzoni mwa mwezi May 2013, tulianza kuona utoro mazoezini bila sababu za msingi na mchango wake kwenye timu ukaanza kushuka kwa kiasi kikubwa pamoja na kuwa mmoja wa wachezaji tegemeo waliokuwa wamefuzu vigezo vyote kushiriki katika mechi zinazoandaliwa na CAF.

"Sababu pekee aliyokuwa akisema inamfanya agome kuitumikia klabu vizuri ni madai ya bonasi pamoja na kwamba hakuwa amecheza mechi ambazo alikuwa anadai hizo bonasi. Kwa mujibu wa sheria na kanuni za shirikisho la soka la Tunisia ni kwamba bonasi na zawadi nyingine hutolewa kulingana na namba ya mechi ambazo mchezaji amecheza na mechi za mashindano alizoshiriki.

"Muda mfupi baadae tulipokea mualiko wake kutoka Shirikisho la soka la Uganda kwa ajili ya kwenda kushiriki michuano ya kufuzu kombe la dunia 2014 dhidi ya Liberia na Angola, michezo iliyopangwa kufanyika tarehe 8 na 15 June 2013. Lakini Okwi aliondoka klabuni bila ruhusa kutoka kwa klabu au kiongozi yoyote. 
"Tulifanya mawasiliano na shirikisho la soka la Tunisia, Uganda na mchezaji mwenyewe ili aweze kurudi klabuni lakini akakataa muda wote.
"Tarehe 12, July 2013, tuliwasiliana FUFA katika kusisitiza mchezaji arejee kwa sababu bado alikuwa na mkataba na klabu. Tunaamini mchezaji alikuwa akidanganywa na baadhi ya watu ili avunje mkataba na klabu katika bila kufuata sheria. Kitendo cha kuchelewa kwa mshahara hakimpi mamlaka ya kuvunja mkataba kisheria.
"Ukosefu huu wa nidhamu wa mchezaji ulitufanya tuanze mchakato wa kudai fidia na hivyo tunawaandikia FIFA kuomba msaada wao.

*Ukosefu wa nidhamu na kutojua majukumu yake kwa mchezaji kumesababisha hasara kubwa za kifedha kwa klabu na hili limetufanya kuomba usaidizi kutoka FIFA kuhusu yafuatayo:

  -Kutokana na kwamba  Emmanuel Anorld Okwi amevunja mkataba yeye mwenyewe na klabu yetu bila kuwa na sababu inayotosha kumpa haki ya kuvunja mkataba kisheria.
 -Tunawaomba FIFA wampe mchezaji amri ya kulipa fidia kutokana hasara na aibu ya kimichezo aliyoingizia klabu: 

    i. Two hundreds fifty seven thousands-one forty t two US.Dollars(247,142 USD) kama fidia ya as a compensation of prorata of the value of his transfer (cf pj n.6)
    ii. Ten thousands US dollars ( 10,000US D) for the period of May 2013 to June 2013( salaries and prizes)
    iii. One hundred eighty thousands US Dollars (180,000 US D) for the period of July 2013 to June 2016 ( salaries till the end of his contract).
    iv.Four hundreds eighty thousands US Dollars( 480,000) for the period of July 2013 to June 2016( prizes of the year 2015)
   v.Charges for location of five hundreds US Dollars per months( 38months x500 US D= 19.000US D)
   Costs for air plane tickets of one thousands US Dollars par months ( (1000US D x12= 12,000USD)
   vi. Costs for hiring car of seven hundred US D per month ( 700 US D x38= 26,000 USD)
   vii. Salaries and prizes /bonuses already received by the player of fifty thousands US dollars( 50,000USD)
   viii. Financial and sportive prejudice( for rupture/breaking legal the contract during the protectedperiod and indemnity of his formation at Etoile Sportive du Sahel) estimated value is three hhundreds thousands US dollars ( 300,000  US D)
 This make the total amount to be paid by the player = One million three hundred twelve thuousands seven hundreds forty two US Dollars( 1,312,742 US D)."

Hivi ndivyo inavyosomeka sehemu ya barua ya Etoile kwenda FIFA kuhusiana na madai yao dhidi ya Okwi. Watunisia hao ambao bado wanadaiwa na Simba kiasi cha dola laki tatu, wameomba walipwe fidia ya dola millioni 1.3 ambayo inaweza kuwa na thamani ya billioni na nusu za kitanzania.

6 comments:

  1. utaacha lini haya mambo wewe hayakuhusu kwanini unaangaika nayo tumekuchoka na hii story ya okwi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwan..kuna kosa gani..jamaa kuandika kama haikuhusu sio lazima kusoma..

      Delete
  2. Ndio maana wachezaj wetu hawafiki mbali kwa kutojua majukumu yao na umuhimu wa mikataba na impacts zake!

    ReplyDelete
  3. Asipomtaja Ojai anahisi nyrnyelle wanamtrmbelea

    ReplyDelete
  4. Kwa maana hiyo Issue ya Okwi bado ni mbichi,nakumbuka Shaffih ulitoa angalizo katika moja ya Article zako ingawa ilipata upinzani kutoka kwa mashabiki wa Yanga.Nafikiri kuna sababu ya kuwasikiliza watu wenye uzoefu katika uchambuzi wa masuala ya soka.

    Abraham J. Mcharo

    ReplyDelete
  5. Hao jamaa wa Etoile wala hawana time na Okwi,ni huku bongo ndio bado Shafii anafuatilia kwa sababu anaona aibu jinsi alivyopotosha watu na mwisho Okwi akacheza Yanga.Itachukua muda mpaka akubali ukweli kwamba alichemsha

    ReplyDelete