Bondia Alibaba Ramadhani akijifua katika Gym ya Luis iliyopo KCMC kwa ajili ya pambano lake la kesho katika ukumbi wa YMCA dhidi ya Bondia Roy Mbunda kutoka Ruvuma. |
Bondia Alibaba Ramadhan akiwa katika mazoezi makali chini ya kocha wake Pascaly Bruno. |
Bondia Alibaba akizungumza na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini kuhusiana na pambano hilo. |
Na Dixon Busagaga,Moshi
BONDIA, Alibaba Ramadhani kutoka mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro
anatarajia kupanda ulingoni Aprili 5, mwaka huu, kupambana na Bondia
Roy Mbunda wa Ruvuna katika mpambano wa uzito wa kati wa kilo 76
(supermiddle).
Ali baba mwenbye rekodi nzuri ya kushinda mapambano 9 na kupoteza 9
kati ya mapambano 18 alizoingia jukwaani likiwemo lile la uzito huo
huo kati yake na Japhet Kaseba, anaingia katika mpambano huo akiwa na
matarajio ya kuinua mchezo wa ngumi mkoani Kilimanajro.
Naye Bondia Mbunda kutoka Ruvuma anaingia katika mchezo huo akiwa na
rekodi safi ya kushinda michezo 12, akipoteza mapambano matano huku
mmoja akitoka sare katika michezo aliyoingia ulingoni.
Akizungumza na Tanzania Daima, Promota wa mpambano huo, Henry George
"Tyson" wa Green Hills Promortion, alisema mpambano huo utafanyika
katika ukumbi wa YMCA na kwamba maandalizi yote yameshakamilika huku
akiongeza kuwa mabopndia hao wanatarajiwa kupima uzito ijumaa ya
Aprili 4 katika ukumbi wa Zumba kuanzia saa nne asubuhi.
"Mpambano wetu utafanyika katika ukumbi wa YMCA, tunatarajia mabondia
wetu, Alibaba na Mbunda wapime uzito siku ya ijumaa pale Zumbaland,"
alisema Tyson.
Wakati huo huo chama cha ngumi mkoani Kilimanjaro (KBA), kimepata
viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika jana katika ukumbi wa YMCA,
ulioko mjini Moshi, mkoani hapo ambapo Elikunda Kipopo alichaguliwa
kuwa mwenyekiti mpya.
Wengine waliochaguliwa katika kamati tendaji walikuwa ni Hamidu
Nyangasa (mwenyekiti msaidizi), Shambe Sagafu (Katibu), Mfaume Bakari
(Katibu msaidizi) Halifa Kiwango (mweka hazina), Aloyce Msila
(mwakilishi wa vilabu) na Emanuel Mushi akichaguliwa kuwa mwenyekiti
wa kamati ya waamuzi.
Wajumbe wa kamati tendaji wa chama hicho, waliochaguliwa na jumla ya
wajumbe 12 wa mkutano huo wa uchaguzi, ulioendeshwa na Mwenyekiti wa
uchaguzi, Shambe Sagafu, ni Felix Babu, Hafidh Mussa na Felix Msele
huku Promota Henry George akitangazwa rasmi kuwa Mjumbe wa heshima wa
mchezo wa Ngumi mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment