63 – Wastani mzuri magoli ya kufunga wa timu ya taifa ya Marekani kutoka mwaka1950 mpaka 1990 – ni wastani wa magoli 2.7 kwa mchezo.
62 – kipigo kikubwa ambacho timu ya taifa ya Marekani imewahi kukipata ni magoli 7 kwa 1 kutoka kwa timu ya taifa ya Italy mwaka 1934 .
61 – Eddie Pope ni beki mahiri wa marekani aliecheza michezo mingi ya kombe la dunia , amecheza michezo 9.
60 –kombe la Dunia la mwaka 2014 , marekani itaanza kampeni yake kwa kucheza na Ghana, taifa ambalo lililowatoa kwenye hatua ya 16 bora kwenye kombe la Dunia lililopita.
59 – Canada imewahi kufuzu kombe la Dunia mara moja (1986).
58 – Sweden waliandaa kombe la Dunia la mwaka1958, na walipoteza mchezo wa fainali mbele ya Brazil.
57 – Luis Monti ni mchezaji pekee aliyecheza timu mbili tofauti kwenye kombe la Dunia alicheza dhidi ya Argentina (mwaka 1930) na Italy (mwaka 1934).
56 – mataifa manne tu ya Ulaya ndio yalioshiriki kombe la Dunia la kwanza mataifa hayo ni (Yugoslavia, Romania, Ufaransa na Ubelgiji ).
55 –Mfaransa Zinedine Zidane alipewa kadi nyekundu kwenye kombe la Dunia la mwaka 2006 baada ya kumpiga kichwa mlinzi wa Italy Marco Matterazzi.
54 – Uholanzi ni moja ya timu bora ya kombe la Dunia ambayo haijawahi kutwaa taji la Dunia, wamefungwa kwenye fainali tatu. (1974, 1978, 2010).
53 – watu bilioni 3.2 Duniani kote waliangalia kombe la Dunia miaka mine iliyopita , ni karibu ya nusu ya wakazi wote wanaoishi kwenye sayari ya Dunia.
52 – Afrika Kusini ndio taifa la kwanza la Afrika kuandaa kombe la Dunia mwaka 2010.
51 –goli la 500 la kombe la dunia lilifungwa mwaka 1950 lililofungwa na mscotland Robert Collins kwenye mchezo ambao Paraguay walishinda 3-2.
50 – Uruguay walitwaaa taji la kombe la Dunia mwaka 1950. Ni fainali pekee zilizotumia mfumo wa robin.
49- mpira rasmi utakaotumika kwenye michuano ya mwaka 2014 umetengenezwa na Adidas unaitwa Brazuca.
48 – uwanja wa Maracana upo katika mji wa Rio de Janeiro uliingiza watazamaji 79,000 mwaka 1950. Kwa sasa unaingiza idadi ya watu 200,000.
47 – kutokana na michuano ya kombe la dunia nchini Brazil, wananchi wa Brazil watapewa mapumziko ya mwezi mmoja .
46 – kombe la Dunia la mwaka 2010 lilishuhudia magoli 145 yakifungwa kwenye michezo 64 ni wastani wa magoli 2.3.
45 – “All in One Rhythm” ndio kauli mbiu rasmi ya kombe la dunia la mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment