Matumaini ya Uholanzi katika kombe la dunia yameanza kupotea siku ya jumatatu jana baada ya kutoka kwa taarifa kwamba Kevin Strootman ataikosa michuano hiyo.
Strootman alipata majeruhi ya goti kwenye mguu wake wa kushoto katika dakika ya 7 ya mchezo wa Roma vs Napoli ambao uliisha kwa Roma kupoteza katika mfululizo wa michezo ya Seria A.
Alirudi uwanjani lakini baadae ikabidi atolewe baada ya kuonekana hatoweza kabisa kuendelea kucheza.
Mchezaji huyo wa zamani wa PSV amekuwa mmoja ya vuingo bora kabisa barani ulaya msimu, na alikuwa mmoja ya wachezaji tegemeo wa kocha Louis van Gaal katika kikosi kitakachoenda Brazil.
Ripoti kutoka Uholanzi zinasema kwamba Strootman atakuwa nje ya dimba kwa miezi tisa kwa tatizo hilo la goti.
Holland wamepangwa kwenye kundi la kifo pamoja na Spain, Chile na Australia.
No comments:
Post a Comment