Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Ufundi.
Uteuzi huo umefanya na Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi, Madadi alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Ufundi aliyekuwepo kumaliza mkataba wake Desemba 31 mwaka jana.
Madadi mwenye leseni A ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni kocha mwenye uzoezi wa zaidi ya miaka 30 ambapo alianza kufundisha mpira wa miguu mwaka 1980 katika klabu ya Maji SC ya Lindi.
Ana elimu ya sekondari aliyoipata katika shule ya Chidya na diploma ya ukocha wa mpira wa miguu aliyoipata nchini Ujerumani. Pia ni Mkufunzi wa makocha wa CAF, na alijiunga na TFF mwaka 2006 akiwa Ofisa Maendeleo.
Alikuwa Kocha wa Taifa Stars mwaka 2000. Mbali ya Maji SC, amewahi kufundisha timu za Nyota Nyekundu, Ushirika ya Moshi, Simba, Shangani ya Zanzibar, Malindi ya Zanzibar, Cardif ya Mtwara na Kariakoo ya Lindi.
Pia amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Ninakumbuka Madadi alikuwa kocha mkuu wa Simba SC ilipotwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1992 kule Zanzibar akitumia fomesheni ya 4-4-2 akiwa na viungo wanne: Ramadhani Maufi "Lenny" na Hussein Masha katikati na Michael Paul "Nylon" na George Lucas"Gazza" pembeni.Pengine anaweza kutusaidia katika nafasi ya sasa kutokana na elimu yake na uzoefu alioupata katika kazi ya ukocha na pia kuwepo katika idara ya ufundi TFF kwa muda mrefu.Aidha Madadi ni mtu msikivu na asiye na makuu.Ushauri wangu kwake ni kwamba awe karibu na makocha,awe karibu na wadau wa soka na aandae utaratibu wa kupata maoni ya wadau wa soka wasio makomandoo,awe karibu na mahali soka linakoanzia yaani mtaani,atafute kiungo kati ya TFF na soka la mtaani bila kupitia FA za mikoa ambazo zimejaa wanasiasa,ili kuhakikisha mpira unachezwa grassroots.Mwisho,namshauri asiwe YESMAN,kwani wako watu watataka kumpangia kazi nje ya utaratibu wa kawaida,hawa ni kamati ya ufundi ya TFF,Rais wa TFF na makomandoo walioko karibu na viongozi wa juu wa tff Hata kama wameamua kumpa kazi hiyo kwa ajili ya maslahi yao binafsi,asiwe mwoga akabiliane nao kitaalam ili wasimwingilie kwenye kazi yake
ReplyDeleteHuyu alikuwa kibaraka wa Kambi ya Malinzi na alitumika sana kuwahujumu uongozi uliopita wa TFF.Hongera Matandika kwa kumsaidia home boy wako
ReplyDeleteTayari ameshaonyesha udhaifu mkubwa kwa kukubali utaratibu wa 'wang'amuzi uchwara wa vipaji kututeulia wachezaji wa timu ya taifa kutoka mchangani kupitia mechi za bonanza ili watupeleke AFCON 2015/Hapa ametekeleza ushauri wa wapambe wa Malinzi na wachambuzi uchwara wa soka ambao si wa kitaalamu bali ni wa kisiasa na kijiweni zaidi
ReplyDelete