MTANZANIA Jackline Sakili ameibuka mshindi wa mbio za km 21 Half Marathon kwa wanawake na kufuta uteja kwa wanariadha wa Tanzania katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika jana katika Chuo cha Ushirika mjini Moshi.
Jackline aliibuka mshindi baada ya kutumia saa 1:12:43 na kujinyakulia Sh milioni 2 huku Mkenya Cynhia Tonett akishika nafasi ya pili kwa kutumia saa 1:14:33 na kujinyakulia Sh milioni 1 wakati nafasi ya tatu ilikwenda kwa Naomi Maiyo aliyetumia saa 1:17:47 na kuzawadiwa Sh 500,000.
Mshindi wa nne alikuwa Nancy Kakwea (Kenya), nafasi ya tano Magreth Karie (Kenya), nafasi ya sita ni Joyce Kandie (Kenya) na nafasi ya saba ni Mary Chemweno.
Kwa upande wa Half Marathon Wanaume nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Lagat Alfers wa Kenya aliyetumia saa 1:02:34 na kujinyakulia Sh milini 2 huku nafasi ya pili ikienda kwa Silah Kippkemboi wa Kenya aliyetumia saa 1:03:04 na kujinyakulia Sh milioni 1 wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Keneth Kandie (Kenya) aliyetumia saa 1:03:20, nafasi ya nne ilikwenda kwa Charles Ogari (Kenya) aliyetumia saa 1:03:25, wa tano ni Alfonce Felix (Tanzania) aliyetumia saa 1:03:27, wa sita Samwel Kariuki (Kenya) aliyetumia saa 1:03:36, wa saba Steven Onjari (Kenya) aliyetumia saa 1:03:39, wa nane Joseph Tophili (Tanzania) aliyetumia 1:03:40, wa tisa Silas Chaboit (Kenya) aliyetumia saa 1:03:45 na wa kumi Felix Kandie (Kenya) aliyetumia saa 1:04:10.
Kwa upande wa km 42 Full Marathon Wanaume David Ruto (Kenya) aliibuka mshindi baada ya kutumia saa 2:16:04 na kunyakua Sh milioni 4, wakati nafasi ya pili ilikwenda kwa Julius Kilimo (Kenya) aliyetumia saa 2:16:17 na kuzawadiwa Sh milioni 2 huku nafasi ya tatu ilikwenda kwa Victor Serem (Kenya) aliyetumia saa 2:16:32 na kuzawadiwa Sh milini 1.
Nafasi ya nne ni Maina Theori (Kenya) aliyetumia saa 2:17:01, nafasi ya tano ni Ezekiel Kimtai (Kenya) aliyetumia saa 2:17:04, nafasi ya sita ni Barnabas Kiptum (Kenya) aliyetumia saa 2:17:57, nafasi ya saba ni Wyclif Biwot (Kenya) aliyetumia saa 2:18:09, nafasi ya nane ni Alex Bartilot (Kenya) aliyetumia saa 2:18:26, nafasi ya tisa ni Daud Lwabe (Tanzania) aliyetumia saa 2:18:34 na nafasi ya kumi ni Wesley Kihegego (Kenya) aliyetumia saa 2:18:41.
Kwa upande wa km 42 Full Marathon Wanawake, Frida Ledepa (Kenya) aliibuka mshindi baada ya kutumia saa 2:40:11 na kujinyakulia Sh milioni 4 huku Joan Rutich (Kenya) akishika nafasi ya pili kwa kutumia saa 2:42:46 na kuzawadiwa Sh milini 2 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Jackline Kithia (Kenya) aliyetumia saa 2:55:19 na kujizolea Sh milioni 1.
Kwa upande wa wanaume km 5 Vodacom Fun Run mshindi ni Fabian Nelson (Tanzania) aliyezawadiwa Sh 500, 000, wa pili Wilbad Peter (Tanzania) aliyezawadiwa Sh 350,000 na wa tatu ni Basil John (Tanzania) aliyepata Sh 200, 000.
Kwa upande wa wanawake km 5 Vodacom Fun Run mshindi ni Natalia Elisante (Tanzania) aliyezoa Sh 500, 000, wa pili Rosalia Fabiano (Tanzania) aliyezawadiwa Sh 350, 000 na wa tatu Aisha Juma (Tanzania) aliyezoa Sh 200, 000.
Kwa upande wa km 10 Gapco Wheel Chair Wanawake mshindi ni Joyce Joseph (Tanzania), wa pili Linda Macha (Tanzania) na wa tatu Hadija Bakari (Tanzania).
Mgeni rasmi Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara, aliwashukuru wadhamini Kilimanjaro Premium Lager kwa kuendeleza mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment