Search This Blog

Friday, March 14, 2014

MKALI NANI: NANI MWENYE UWEZO ZAIDI KATI EDIBILY LUNYAMILA NA MRISHO NGASSA.


9 comments:

  1. kwa wa kwanza lunyamila wa pili mapunda wa tatu said maulidi wa nne ndio ngasa

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. Lunyamila next level kaka,i wish tupate wachezaji wengine kama kina lunya co awa wakisifiwa kidogo wanaongeza mke mwingine

      Delete
  3. Kwa kweli Mpaka sasa sijaona mfano wa lunyamila. Jamaa alikuwa fundi hasa! Ni kipaji cha asili kama marehemu kizota

    ReplyDelete
  4. Lunyamila na Ngassa wamecheza soka katika vipindi tofauti na katika mifumo tofauti ya ushambuliaji,ufungaji na ukabaji,hivyo ni vigumu kuwapima kwa fair assessment.Sana sana tutaambulia kutaja tofauti zao na sio ubora wa mmoja dhidi ya mwingine.Kwa mfano Lunyamila alikuwa anatumia mguu mmoja tu wa kushoto na alikuwa anacheza nafasi moja tu ya winga wa kushoto na hakuwa na kasi sana lakini silaha yake ilikuwa miliki kubwa ya mpira,maamuzi sahihi na ufundi wa hali ya juu wa kuuchezea mpira lakini kwa malengo katika enzi ambapo hakukuwa na mifumo mingi ya ukabaji na ushambuliaji kama ilivyo sasa.Ngassa anatumia miguu yote miwili na anacheza nafasi zote za ushambuliaji,ana kasi lakini hana ufundi mkubwa wa kuuchezea mpira kwa malengo katika zama ambazo kuna mifumo mingi ya ukabaji,ushambuliaji na ufungaji.Wote wawili wana uwezo mkubwa wa kufunga mabao.Kwa maoni yangu Lunyamila angeweza kucheza soka Ulaya katika madaraja ya juu katika ligui kubwa kitu ambacho hakiwezekani kwa Ngassa

    ReplyDelete
  5. Ngasa si muuza sura tu

    ReplyDelete
  6. Wachezaji kama lunyamila hupatikana mara mojamoja katika vizazi vya nchi mojamoja.Mfano; Argentina walichua kipindi kirefu tangu Maradona mpaka Mesi,COMEROON wamechukua muda pia toka kwa Rojamila mpaka kwa ET'O.Hii nisawa na Ngasa na LUNYA.

    ReplyDelete
  7. Wote ni wafupi. Wote ni vipenzi wa yanga kwa nyakati tofauti.wote wamewahi kuhama yanga kwenda timu nyingine kisha kurudi yanga.wote wameishachezea simba.wote wamechezea timu ya taifa wakiwa wachezaji wa kutegemewa. Wote wamejaribu soka la kulipwa na kushindwa majaribio mmoja chile mwingine England.kwa ujumla mabadiliko ya soka duniani kila mmoja anabebwa na zama zake.

    ReplyDelete
  8. kaka luminyama ni kitu kingine kabisaaaaa usipime,soka la sasa ni ucheck bob kina Ngassa ni mauzo tu na si kazi wala kipaji wanaendekeza umaarufu na kusahau kama kuna watanzania wanatizama soka. olwaz luminyama bro

    ReplyDelete