Search This Blog

Monday, March 3, 2014

MJADALA: SIMBA YA 2003 VS YANGA 2014 - TIMU IPI INA KIKOSI KIKALI - NA JE YANGA WATAWEZA KUWAVUA UBINGWA WAARABU KAMA SIMBA MWAKA 2003

Juma Kaseja, Athuman Machupa, Boniface Pawasa, Ulimboka Mwakwinge, Selemani Matola, Alex Massawe, Victor Costa, Ramadhani Wasso, Yusuph Macho, Said Sued - Hiki ndio kikosi cha Simba kilichoivua ubingwa Zamalek nyumbani kwao mwaka 2003.

Deaogratius Dida Munishi, Simon Msuva, Hamis Kiiza, Oscar, Kelvin Yondan, Emmanuel Okwi. Niyonzima Haruna, Mbuyu Twite, Nadir Haroub Cannavaro, Domayo, Mrisho Ngassa. - Hiki ndio kikosi cha Yanga cha mwaka 2014 ambacho nacho kimewapiga waarabu 1-0 nyumbani kama ilivyofanya Simba mwaka 2003. 

Je unadhani kipi ni kikosi kikali na Je Yanga itaweka rekodi kama ya Simba  kumtoa Al Ahly ambaye ni bingwa mtetezi wa Champions league?

14 comments:

  1. Yanga bado sana! Huwezi fananisha na wachezaji wa zaman ambao hawakati tamaa,wachezaji wetu wa ss hivi wanalewa sifa mapema,yanga inatakiwa ijipange sana kule cairo,kwa ninavyowajua al ahly walivyocheza juzi sivyo watakavyocheza cairo.walijitahidi yanga kucheza kwa nguvu na ushirikiano lkn waarabu wao hawakutumia nguvu zaid ya kucheza nyuma,sijaona bado yanga ya juzi uifananishe na simba ya kina seleman matola.ili kuamin maneno yangu tusubiri tarehe tisa.

    ReplyDelete
  2. Ulinganishaji wako siyo sahihi, kwani Simba ya 2003 haikumtoa Al Ahly, bali Zamalek, ingawa Zamalek alikuwa bingwa mtetezi kama ilivyo kwa Al Ahly ya sasa!

    ReplyDelete
  3. Hahahahaha simba ya mwaka 2003 ilikuwa bora sana kuliko yanga hii, na kipindi hicho asilimia 99.9 ya wachezaji wa simba walikuwa wazawa kasoro ramadhan waswa.

    ReplyDelete
  4. kikosi kile cha Simba ya 2003 kilikuwa na baadhi ya wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu kama Kaseja,Wasso,Pawasa,Costa,Matola,Garrincha,Ulimboka,Machupa na Gabriel.Hawa pia walikuwemo kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichofika fainali ya Kombe la Chalenji mwaka 2002 kule Mwanza na kufungwa na Kenya 3-2.Pengine upo mlingano na kikosi cha sasa cha Yanga chenye Twite,Yondani,Domayo,Niyonzima,Ngassa,Kiiza,Okwi.Simba ile ilikwenda Cairo na kufungwa bao 1-0 na Zamalek ndani ya dakika 90 lakini ikafanikiwa kushinda katika mikwaju ya penati.Tofauti kubwa baina ya vikosi hivi ni iwapo mechi ya Yanga na Ahly itaamuliwa kwa penati kwani nina wasiwasi na uwezo wa kufunga penati wa wachezaji wa Yanga.Kiiza ndiye mfungaji wa uhakika wa penati lakini wanaobakia kama Canavaro,Niyonzima,Ngassa,Okwi na Msuva sio wafungaji wa mara kwa mara wa penati.Simba ile ilikuwa na watu wa uhakika inapofika penati kama vile Saidi Sued,Wasso,Christopher Alex,Matola,Bethuel,Pawasa,Costa,Ulimboka na Machupa

    ReplyDelete
  5. Waandishi KANJANJA!!!!

    ReplyDelete
  6. Kwani yanga inacheza na Zamaleki? Acha post za kuwachanganya watu. Juzi yanga iliposhinda kina maestro badala ya kuongelea mechi wakasema Yanga ina kazi ngumu Misri sa walitaka ifungwe ndo ikawe rahisi? Mwaka 2003 wachezaji hawakuwa na exposure kama hawa wa sasa hivi. Wachezaji hawa wamechezaji na wachezaji makubwa duniani timu ya Brazil ambayo wiki 2 kabla ya WOZA, kina etoo, Drogba, domayo kakabana na Yaya toure kwa maoni yangu best midfield in the World kwa sasa. Internationl Footbal is all about exposure and experience

    ReplyDelete
    Replies
    1. Alichofanya mwandishi n kulinganisha, simba alicheza na zamalek aliekua bingwa mtetez. The same na yanga anaecheza na bingwa mtetez pia. Wakat mwngine tuwe waelewa. Kwa mfano the mail wanapowalinganisha bayern ya sasa na barca ya guardiola, wanatambua pia tofaut za mda na changamoto baina ya bayern ya sasa na barca ya guardiola! Kulinganisha n kitu kizuri. Kinaweza kuijeng yanga. Wachezaji watataka wafikie na kupita mafanikio ya simba ya kipind kile. Na hyo inaonyesha jins gan watu walivyo na iman na yanga hii kuliko kipind chochote kile... Yanga hii imekamilika kuliko tim yoyote ile ya kitanzania tangu simba ile ya 2003, kuanzia makipa, beki, katikati na fowad hatar. Naamin yanga watafika mbali sana na wataanza kwa kuwatoa al ahly!

      Delete
  7. Ahly iliyofungwa 1-0 juzi ndiyo hiyo hiyo itakayocheza Cairo na mfumo wao wa uchezaji utabadilika kidogo kwa kushambulia zaidi ili wapate mabao mengi ya mapema.Kumbuka kwamba hata Yanga nao watatumia mfumo wa kujilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza ambayo kwa namna kikosi chao kilivyo wataumudu kwa kiwango cha juu mfumo huo kwa kuwatumia strikers wenye kasi Msuva,Ngassa na Okwi,Kwa hakika huu ni mwaka wa Yanga kuwatoa Ahly kwani Ahlyt imeanza kipindi cha mpito baada ya kuondokewa na wazoefu na kupisha damu changa kama ilivyokuwa kwa Zamalek wakati inatolewa na Simba mwaka 2003.Ikumbukwe kwamba baada ya kutolewa na Simba Zamalek ilipotea kwa karibu miaka sita kwenye soka la ngazi ya afrika,huku mwaka uliofuata Simba hiyo hiyo ikatolewa katika raundi ya kwanza na Zanaco ya ZambiaHii inaonyesha kwamba siku za Zamalek zilikuwa zimefika na timu yoyote ingeweza kuwaondoa mashindanoni na bahati hiyo ikawadondokea simba

    ReplyDelete
  8. Kweli sasa nimeamini wanao wagombanisha mashabiki wa Simba na Yanga ni waandishi kama ww dauda......
    endelea usichoke utafanikiwaa

    ReplyDelete
  9. Tukiweka unazi na ushabiki pembeni,Simba ile ilikuwa bora sana kuanzia beki hadi striker,tulinganishe comb ya Yondani na Cannavaro na ya Pawasa na Costa,jamani tusikufuru jamani

    ReplyDelete
  10. Proffesionalism, mzee huku mtaa umedharika sana watu wanakuita KIHIYO,KANJANJA etc. kwa nini usiende kufanya kazi ulosomea.

    ReplyDelete
  11. Mpira Ni mchezo WA makosa na surprise so chochote knaweza tokea tusubir tu

    ReplyDelete
  12. chanel gan itarusha mechi hyo jaman?

    ReplyDelete