Jana usiku Manchester Utd na Borrusia Dortmund zilifanikiwa kufuzu hatua ya robo ya fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
Mabao matatu ya mshambuliaji Robin Van Persie yaliisaidia Manchester Utd kuifunga Olympiakos ya Ugiriki MABAO 3-0 na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 3-2.
Huko nchini Ujerumani pamoja na Dortmund kufungwa nyumbani kwenye uwanja wa Signal Iduna Park mabao 2-1 na Zenit St Petersburg ya nchini Urusi,ilifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa jumla ya mabao 5-3.
mabao ya Zenit hapo jana usiku yalifungwa na mshambuliaji raia wa Brazil Hulk kwa shuti kali na lingine lilifungwa na Salomon Rondon wakati lile la Dortmund lilifungwa na kiungo mkongwe Sebastian Kehl.
Sehemu ya mashabiki wa Dortmund hapo jana.......
Mshambuliaji Hulk akishangilia bao lake hapo jana........
Hii ni faulo aliyochezewa Robin Van Persie na kuipatia Man Utd mkwaju wa penati...penati hiyo ilifungwa na Van Persie
wachezaji wa Dortmund wakijumuika na mwenzao Sebastien Kehl kushangilia bao lake....
Van Persie akifunga bao lake la tatu kwenye mchezo wa jana na kuipatia Man Utd ushindi wa mabao 3-0.
Mshambuliaji Salomon Rondon akiifungia timu yake ya Zenit bao la pili kwa kichwa cha kuchumpa...kwenye mchezo huo Zenit ilishinda mabao 2-1..
David Moyes akifurahia ushindi wa timu yake.....
Kocha wa Dortmund Jurgen Kloop akishangilia na wachezaji wake kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA Champions League hapo jana usiku....
No comments:
Post a Comment