Hizi ni fainali za 20 za kombe la dunia, zijue timu zilizowahi kutwaa ubingwa wa kombe la dunia pamoja na wafungaji wa michuano hiyo kuanzia mwaka 1930 mpaka 2010.
Mwaka 1930 fainali ziliandaliwa nchini Uruguay wakati mfungaji bora wa michuano hiyo alikuwa Muargentina Guillermo Stabile aliefunga magoli nane wakati bingwa wa kombe la dunia mwaka huo ilikuwa ni timu ya taifa ya Uruguay,.
Fainali za pili za dunia zilifanyika mwaka 1934 nchini Italy huku Old rich Nejedly akitwaa kiatu cha dhahabu na Italy walitawaa taji la ubingwa wa dunia.
Fainali za tatu zilifanyika mwaka 1938 nchini Ufaransa wakati Leonidas wa Brazil alitwaa kiatu cha ufungaji bora Italy walitetea taji la kombe la dunia.
Fainali za nne zilifanyika nchini Brazil mwaka 1950 , mfungaji bora alikuwa mbrazil Admir aliefunga magoli 8, wakati mabingwa walikuwa ni nchi ya Uruguay.
Fainali za tano zilifanyika mwaka 1954 nchini Switzerland mfungaji bora alikuwa Sandor Kocsis wa Hungary aliefunga magoli 11, kwa mara ya kwanza Ujerumani Magharibi walitwaa kombe la dunia.
Fainali za sita zilifanyika mwaka 1958 nchini Sweden, mfungaji bora alikuwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Just Fontaine aliefunga magoli 13, wakati Brazil walikuwa mabingwa kwa mara ya kwanza.
Fainali za saba zilifanyika mwaka 1962 nchini Chile, wafungaji bora walikuwa Drazan Jerkovic wa Czesk, Florian Albert wa Hungary, Garrincha wa Brazil, leonel Sanchez wa Chile, Valentin Ivanov wa Russia, na Vava wa Brazil wote walifunga magoli manne kila mmoja, wakatI Brazil walifanikiwa kutwaa taji la dunia kwa mara ya pili.
Fainali za nane zilifayika mwaka 1966 nchini England, mfungaji bora alikuwa ni mreno Eusebio ambaye alifunga magoli 9, huku England kwa mara ya kwanza wakatwaa taji hilo la dunia.
Fainali za tisa zilifanyika nchini Mexico mwaka 1970, mfungaji bora alikuwa ni Gerd Muller alifunga magoli 10, na timu ya taifa ya Brazil ama Selcao walitwaa taji la dunia.
Fainali za kumi zilifanyika mwaka 1974 nchini Ujerumani Magharibi, mfungaji bora Grzegorz Lato wa Poland aliefunga magoli saba, kwa mara ya pili Ujerumani Magharibi walitwaa kombe la dunia.
Fainali za kumi na moja zilifanyika nchini Argentina mwaka 1978, Mario Kempes wa Argentina alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga magoli sita, pia Argentina walitwaa taji hilo la dunia kwa mara ya kwanza.
Fainali za kumi na mbili zilifanyika mwaka 1982 nchini Hispania , mfungaji bora alikuwa Paulo Rossi aliefunga magoli sita na na timu ya taifa ya Italy maarufu kama Azuri walitwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya pili.
Fainali za kumi na tatu zilifanyika mwaka 1986, nchini Mexico, mfungaji bora alikuwa Gary Lineker wa England baada ya kufunga magoli sita, na Argentina walitwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya pili.
Fainali za kumi na nne zilifanyika nchini Italy, mwaka 1990, mfungaji bora alikuwa Salvatore Schillaci wa Italy aliefunga magoli sita, na timu ya Ujerumani Magharibi wakatwaa ubingwa.
Fainali za kumi na tano zilifanyika nchini Marekani mwaka 1994, wafungaji bora walikuwa Hrist Stoichkov, Oleg Salenko wa Russia baada ya kufunga magoli sita, kila mmoja, na Brazil walifanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia.
Fainali za kumi na sita zilifanyika nchini Ufaransa mwaka 1998, mfungaji bora alikuwa Davor Suker alitwaa kiatu cha ufungaji bora, na timu ya taifa ya Ufaransa ilitwaa ubingwa wa Dunia.
Fainali za kumi na saba ziliandaliwa na nchi mbili za bara la Asia, kwenye nchi za Korea Kusini na Japan mfungaji bora alikuwa ni Ronaldo de Lima wa Brazil aliefunga magoli nane, wakati Brazil walifanikiwa kutwaa taji la dunia kwa mara ya tano.
Fainali za kumi na nane ziliandaliwa nchini Ujerumani mwaka 2006, mfungaji bora wa michuano hiyo alikuwa Miroslav Klose baada ya kufunga magoli matano, huku Italy wakitwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya nne.
Fainali za kumi na tisa ziliandaliwa nchini Afrika Kusini mwaka 2010, wafungaji bora walikuwa Diego Forhan wa Uruguay, Thomas Muller wa Ujerumani, Wesley Sneider wa Uholanzi, na David Villa wa Hispania, bingwa wa alikuwa timu ya taifa ya Hispania maarufu kama La Roja.
No comments:
Post a Comment