Familia ya Glazer sasa wapo radhi sasa kupokea wazo la kubadilisha kocha, ingawa mpaka sasa bado wanampa sapoti Moyes, lakini wiki ijayo inasemekana mambo yanaweza kubadilika. United kesho inabidi ifanye kila liwezekanalo kubadilisha matokeo ya 2-0 dhidi ya Olympiakos katika Champions League, baada ya hapo wataenda kupambana na timu ngumu ya West Ham United halafu siku chache baadae wanakutana na mahasimu wao Manchester City.
Wakati endapo wataweza kufuzu kucheza robo fainali ya Champions League kutaleta ahueni kwa Moyes, matokeo mabaya ya kutolewa na kuelekea mechi zingine ambazo kama hatopata matokeo mazuri basi mambo yanaweza kumbadilikia. Uvumilivu utawashinda mabosi wa familia ya Glazers.
Inaaminika The Glazers wapo katika presha kubwa hasa baada ya mfululizo wa matokeo mabaya hivi karibuni, huku maofisa wengine wa bodi ya wakurugenzi tayari wameshaanzisha hoja ya kufanyika mabadiliko kwenye benchi la ufundi.
Inaaminika The Glazers wapo katika presha kubwa hasa baada ya mfululizo wa matokeo mabaya hivi karibuni, huku maofisa wengine wa bodi ya wakurugenzi tayari wameshaanzisha hoja ya kufanyika mabadiliko kwenye benchi la ufundi.
Vyanzo vya habari Old Trafford vinaripoti kwamba imeonekana hata Sir Alex Ferguson haonekani kumsapoti Moyes hadharani katika mikutano ya bodi, ingawa pia bado hajambadilika mrithi wake. Hata hivyo Moyes bado anasapotiwa na Bobby Charlton.
Wakati huo huo mtandao wa gazeti la The Sun umeripoti kwamba David Moyes amepewa mechi 3 - dhidi ya Olympiakos, Westham United na Manchester City na endapo atapoteza mechi 2 kati ya hizo basi ataondolewa na Ryan Giggs atakaimu nafasi yake mpaka msimu ujao utakapoanza mchakato mpya wa kutafuta kocha wa kudumu.
No comments:
Post a Comment