Na Oscar Oscar Jr
0789-784858
Mechi ya Mtibwa Sugar vs simba iliyopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri pale
Morogoro wiki moja iliyopita,ilimalizika kwa matokeo ya sare ya
1-1,Mussa
Hassan Mgosi akiifungia Mtibwa sugar na Hamis Tambwe akiisawazishia timu
yake ya Simba.Jonisia Rukyaa toka
Bukoba ndo mdada aliyekuwa mwamuzi wa kati wa mchezo huo.
Kisaikolojia na tamaduni za kwetu,zinamuonea sana mwanamke.Mwanaume siku zote anajiona yuko juu,nafsi yake haikubali kuongozwa na mwanamke.Mwanamke nae anapokuwa kiongozi wa mwanaume,hupoteza hali ya kujiamini ingawa sio wote! Jambo hili sio kwenye soka tu,hutokea hata kwenye ofisi nyingine lakini pia ni lazima nikiri kwamba wapo baadhi ya wanawake wanauwezo mzuri sana wa kuongoza wanaume na mambo yakanyooka.
Wachezaji wengi wa Simba na wale wa Mtibwa walipewa kadi za njano nyingi sana,na Shabani Nditi nahodha wa timu ya Mtibwa sugar kuzawadiwa kadi nyekundu.Ukichunguza vizuri kadi hizo utagungua kwamba chanzo ni wachezaji kumdharau mwamuzi wa kike na mwamuzi huyo kujihami baada ya kuhisi anadharauliwa.Jonisia Rukyaa aliitendea haki mechi ile sema tu,hata angechezesha vipi,hawezi kupewa Ballon D'or!

Watangazaji wa skysports Andy Burton na Andy Gray waliwahi kuingia matatizoni mara baada ya kutoa comment zao za kumbeza mwamuzi mdada wa EPL Sian Massey.Kocha wa zamani wa manchester united Sir Alex Ferguson aliwahi kuulizwa kama na yeye anafikiria kuajiri Daktari wa kike kama klabu ya chelsea inavyomtumia mdada Daktari mwenye shahada ya Uzamili(masters) Eva Carneiro,Ferguson alijibu "mchezo wa soka ni mchezo wa wanaume hivyo wachezaji wake hawatokuwa huru kueleza matatizo yao kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa daktari wa kike"
Kumekuwa na mtazamo hasi sana kwa wanawake wanaojihusisha na mchezo wa soka lakini ukweli utabaki pale pale,tuna wauguzi na madaktari wengi tu wa kike na kama tutawakwepa viwanjani,tutakutana nao Hospitali.Tatizo kwenye soka sio mwamuzi wa kike au wa kiume ni ukweli usiopingika kwamba mchezo huu uko kwenye kasi sana na kwa mwamuzi ambaye hapati fursa ya kutazama tukio zaidi ya mara moja,ni rahisi sana kufanya makosa.
Nadhani
kabla ya kuwanyooshea kidole kina Israel Mkongo,Oden Mbaga na wengine
kwamba wamepewa kitu kidogo au wanaonyesha mapenzi kwa timu fulani ni
lazima kwanza tuwapongeze kwa kazi ngumu sana wanayoifanya.Makocha
hufanya makosa,wachezaji wanakosea,viongozi wa timu wanakosea na hata
wachambuzi wa soka nao kuna muda wanakosea.Unadhani waamuzi ni malaika?
No comments:
Post a Comment