Pambano la aliyekuwa bingwa mtetezi Liston dhidi ya mwanasumbwi kinda Clay - ambaye baadae alikuja kuitwa Muhammad Ali – lilifanyika mnamo February 25, 1964, huko Miami.
Clay, akiwa just 22, aliingia kwenye ulingo akiwa hapewi nafasi kabisa ya kushinda mchezo huo, lakini akaustua ulimwengu na ushindi wa kushtukiza ulioweka msingi mzuri katika maisha yake ya ndondi.
Pambano hili, lilitajwa kushika nafasi ya nne katika matukio makubwa katika karne ya 20 na jarida la Sports Illustrated, lilimalizika baada ya Liston alipovua gloves katika raundi ya saba na Clay akaanza kuruka na kushangilia ‘I’m the champ!’
Sasa nyaraka zilizotolewa na The Washington Times chini ya sheria ya uhuru wa habari zinaonyesha kwamba FBI walikuwa na mashaka kwamba mchezo huo ulikuwa umepangwa kwa maana ya matokeo na mtu mmoja ambaye alikuwa na anahusika na kikundi cha uhalifu huko Las Vegas pamoja na Liston.
Kulikuwepo na memos zilizopelekwa kwa mkurugenzi J. Edgar Hoover, zinaonyesha kwamba FBI ilikuwa na mashaka na bwana Ash Resnick, mcheza kamari wa huko Las Vegas ambaye anahusika na vikundi vya uhalifu, wakiwa wanatuhumiwa kupanga matokeo ya mechi kadhaa za ndondi likiwemo pambano hilo Clay-Liston.
Katika vielelezo vya ushahidi wa FBI, moja ya memo yenye tarehe May 24, 1966, inaelezea mahojiano na mcheza kamari wa mji wa Houston aliyeitwa Barnett Magids, ambaye anasema mazungumzo yake na Resnick kabla ya pambano la kwanza Clay-Liston.
Magids aliwaambia maofisa wa FBI kwamba Resnick alimwambia asicheze kamari/asimuwekee mzigo Liston kwa upande wa ushindi. Ripoti pia zinaeleza kwamba Resnick na Liston wote walitengeneza zaidi ya $1million kupitia kamari waliyocheza kwenye pambano hilo.
Nyaraka zote hazionyeshi kwamba Ali alikuwa ana ufahamu wowote juu ya mchezo mchafu uliokuwa ukiendelea nyuma ya pambano hilo.
Ali na Liston wote walikuwa watu wenye matukio ya utata, Liston alikuwa mfungwa wa zamani ambaye alikuwa na mahusiano na makundi ya kihualifu, wakati Clay alijiunga na Black Muslims wiki kadhaa kabla ya pambano na kuamua kubadili dini kabisa na kujiita Ali baada ya pambano.
Mwanzoni mwa pambano Clay alipatwa na matatizo, alipoteza uwezo wa kuona vizuri kwa wakati fulani, kabla ya kurudi vizuri na kumnyoosha vizuri Liston.
The result was such a shock at the time that there was speculation that the outcome might have been manipulated.
No comments:
Post a Comment