Search This Blog

Sunday, February 23, 2014

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 2 - 3 JKT RUVU,AZAM FC 2:2 PRISONS - FULL TIME


Full time: Simba 2 - 3 JKT Ruvu

FULLTIME. AZAM 2-PRISONS. Mechi ilikuwa ya mashambulizi hasa kwa Prisons ambao walicheza soka la uhakika na la nguvu mara baada ya Azam kubaki na wachezaji 10 uwanjani. Prisons wameonesha soka safi. Kutoka hapa Azam Complex Chamanzi, ni mimi Baraka Mbolembole, AZAM FC 2-2 TANZANIA PRISONS

Dakika ya 80, kiungo mshambuliaji wa Prisons, Mfalile anaisawazishia timu yake. Azam 2-2 Prisons, 

Dakika ya 78. Azam 2-1 Prisons. Mechi imekuwa ya kuviziana na Azam hawaonekani kuwa na presha ya kutafuta bao lingine, mpira unachezwa sana katikati ya uwanja huku Prisons wakilisakama lango la Azam kwa nia ya kusawazisha ila walinzi wa Azam, Nyoni upande wa kushoto, Mwantika upande wa kulia na wale wa kati , Aggrey na Mourad wanaonekana kwa imara

Dk 84 GOOO....! Tambwe anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa akiunga krosi ya Joseph Owino. Simba 2-3 JKT

Dakika ya 75. azam 2-1 Prisons. Mwadini Ally anapewa kadi ya njano kwa kosa la kuchelewesha muda

Dk 72 RED CARD! Damas Makwaya anaonyeshwa kadi ya pili ya njano na nyekundu. Mwanzo alimchezea faulo Harun Chanongo.

Dk 70 SUB: Simba imefanya mabadiliko ametoka Badru ameingia Issa Rashid Baba Ubaya.

Dakika ya 70. Azam 2-1 Prisons, mpira umekuwa si wa kasi sana na Azam wanaonekana kumiliki mchezo

Dk 64 GOOOO...!  Tambwe anaipatia simba bao la kwanza kwa njia ya penalti. Simba 1-3 JKT

Dk 64 PENALTIIII....! Simba inapata penalti baada ya Bunu kumuangusha Kiemba ndani ya eneo la hatari.

Dakika za 65, Azam 2-1 Prisons.

Dakika ya 60, Azam 2-1 Prisons. Mpira umekuwa na mashambulizi ya kila upande.

Dakika ya 57, Azam 2-1 Prisons

Dk 54 Amissi Tambwe wa Simba anakosa bao la wazi baada ya kutengewa pasi nzuri na Badru lakini shuti lake hafifu linadakwa na Dihile.

Kipre Tchetche anaoewa kadi ya njano na kutolewa kwa nyekundu

Dk 53 GOOO....! Swita anaipatia bao safi JKT akimchambua Berko baada ya kugongeana pasi nzuri na Mgisa. Simba 0-3 JKT

Dakika ya 50, Azam 2-1 Prisons, Kipre Tcheche anaifungia timu yake baada ya kupiga mkwaju mkali

Dakika ya  49. Azam 1-1 Prisons, Aggrey Morris anaisawazishia Azam kwa kichwa

Dakika ya 47. Azam 0-1 Prisons. Prisons wanapata faulo, kiki ya Omega Seme inakwenda moja kwa moja nyavuni na kuipatia Prisons bao la kuongoza

Dk 45 SUB: Simba imefanya mabadiliko ametoka Henry Joseph ameingia Uhuru Seleman.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Dk 45 HALF TIME! Simba 0-2 JKT

Dk 45 GOOOOO.....! Emmanuel Swita anaifungia JKT bao la pili kwa njia ya penalti saafi akimchambua kipa wa Simba, Yaw Berko. Simba 0-2 JKT

Dk 45 PENALTIII....! JKT wanapata penalti baada ya Henry Joseph kumchezea rafu mbaya  Amos Mgisa ndani ya eneo la hatari baada ya kuachwa.

Dakika ya 45. Azam 0-0 Prisons. Half time

Dk 40 Simba inapata faulo ndani ya eneo la 18 lakini Jonas Mkude anapaisha mpira nje.

Bunu Wa JKT Ruvu atolewa nje kushughulikiwa na benchi la ufundi baada ya kufanyiwa madhambi na Henry Joseph anayelimwa kadi ya njano Dk 36

Kadi ya njano kwa mfungaji wa JKT Ruvu Hussein Bunu

Chamazi Azam na Prisons dakika ya 31 bado 0-0

Dk 32 YELLOW CARD! Bunu anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kupiga mpira mbali baada ya mwamuzi kupiga filimbi.

 Dakika ya 25. Azam 0-0 Prisons.

Dk 31 JKT wanafanya shambulizi kali langoni kwa Simba na kupata kona huku Amos Mgisa akionekana kumsumbua Henry Joseph wingi ya kulia.

Dk 28 Amri Kiemba anapaisha mpira baada ya kutengewa vizuri na Harun Chanongo.

  Huyu kiungo wa ulinzi wa Prisons, Magetha ni mchezaji ambaye anaituliza timu na kuipandisha pale inapobidi kufanya hivyo. Mlinda mlango wa Prisons, MWETA, ameoneshwa kadi ya njano kwa kosa la kuchelewesha muda. azam 0-0 Prisons, dakika ya 21

Dk 26 Edward Charles anachezewa faulo na William Lucian 'Gallas'.

Dk 22 SUB: Simba inafanya mabadiliko ametoka Said Ndemla anaingia Ali Badru.

Azam wamefika katika lango la Prisons mara tatu lakini washambuliaji wake bado hawajaweza kuona lango. Ni dakika ya kumi na hadi sasa hakuna shambulizi la hatari.

Dk 13 GOOO....! Hussein Bunu anaipatia JKT bao la kwanza baada ya kupokea pasi safi ya Mbaga. Simba 0-1 JKT.

Dk 11 Simba na JKT zinacheza soka safi na zinacheza kwa kukamiana sana

Dk 06 - Idd Mbaga anakosa bao la wazi akiwa amebaki na Kipa wa Simba Yaw Berko akishindwa kuunga pasi safi ya Amos Mgisa aliyemtoka Henry Joseph. Shuti la Mbaga lilidakwa na Berko.

Uwanja wa Chamazi ni dk ya 6 kati ya Azam na Tz Prisons bado 0-0

Dk 05 Idd Mbaga wa JKT anamchezea faulo Donald Mosoti


Dk 02 Damas Makwaya wa JKT anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Harun Chanongo.

Dk 00 Mpira umeanza! Simba 0-0 JKT

Mwamuzi ni David Paul wa Mtwara msaidizi wa kwanza ni Ferdinand Chacha wa Kagera na msaidizi wa pili ni Lulu Mushi wa Dar es Salaam.

VIKOSI VINAVYOANZA LEO

SIMBA SC VS JKT RUVU

Simba line up: Yaw Berko, William Lucian 'Gallas', Henry Joseph,  Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Awadh Juma, Said Ndemla, Amissi Tambwe, Amri Kiemba, Haruna Chanongo.

JKT Ruvu line up : Shaaban Dihile,  Damas Makwaya, Edward Charles, George Minja, Salum Mtaki, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Emmanuel Swita, Idd Mbaga, Hussein Bunu, Sosthenes Manyasi


AZAM FC VS PRISONS

1. Mwadini
2. David
3. Erasto
4. Moradi
5. Aggrey
6. Bolou
7. Himidi
8. Sure Boy
9. Bocco
10. Brian
11. Kipre
Subs
1. Aishi
2. Jabir
3. Mwaipopo
4. Mcha
5. Kone
6. Malika
7. Kelvin

Tanzania Prisons .
 1 Wilbeth Mweta 2 .Salum Kimenya 3.Lauriun Mpalile 4.Nurdin Chona 5.Lugano Mwangama 6.Jimmy Shoji 7.Godfrey Magetha 8. Omega Seme 9.Peter Michael 10.Frank Wiliam Muwi .Fred Chudu .
Sub .Beno Kakolanya ,Bryson Mponzi ,Henry Mwalugala ,Hamisi Maingo,Six Ally Mwasekaga ,Jumanne Elfadhili ,Ibrahimu Isihaka,Jeremia Juma ,Denis Lwanda

1 comment:

  1. Haya ndio matatizo ya kupania mechi za mabonanza na kombe la mbuzi kama vile nani mtani jembe halafu timu ikija kwenye ligi nyanya tupu.Kelele nyingi kumbe hamna kitu.Bado mechi saba na Yanga,Azam,Coastal,Kagera sugar,Prison na Ashanti tutarajie vpigo na vilio zaidi kwa simba

    ReplyDelete