Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Namibia (Brave Warriors) itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.
Wachezaji walioitwa katika timu hiyo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki wa pembeni ni Edward Charles (JKT Ruvu), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City) na Michael Aidan (Ruvu Shooting).
Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga) wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya Sports Club, Qatar).
Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini Machi 1 mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia inatarajiwa kuondoka Machi 3 mwaka huu kwenda Windhoek.
Wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya kimataifa na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya mechi zao kumalizika.
TAARIFA YA KLABU ZOTE TANZANIA YATAKIWA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimewaagiza wanachama wake- vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwapatia orodha ya klabu zote za mpira wa miguu zilizosajiliwa katika mikoa yao.
Orodha hiyo inatakiwa kujumuisha namba ya usajili wa klabu, viongozi waliopo madarakani kwa sasa pamoja na mawasiliano yao (namba za simu na anuani za email) na eneo yalipo makao ya klabu husika.
Kwa utaratibu huo, vyama vya mikoa vitakusanya taarifa za klabu zinazocheza ligi ya mikoa, lakini wakati huo vinatakiwa kuwasiliana na wanachama wake (vyama vya wilaya) kupata taarifa za klabu zinazocheza ligi za wilaya na baadaye kuziwasilisha TFF.
Klabu ambazo taarifa zake zitakuwa hazijawasilishwa TFF hadi Agosti mwaka huu hazitaruhusiwa kushiriki ligi ya msimu wa 2014/2015 katika ngazi yoyote ile.
RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari juu ya programu ya mpira wa miguu kwa vijana.
Mkutano huo utafanyika kesho (Februari 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio.
AZAM, ASHANTI UNITED KUKIPIGA VPL
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa mechi moja itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mechi itazikutanisha timu za Azam inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 37 dhidi ya Ashanti United iliyoko nafasi ya 12 kwa pointi zake 14.
Wapi Salum Abubakar"Sure boy",Juma Luizio,Kenneth Masumbuko,Abdi Banda?Pia bado kuna upungufu wa beki mmoja wa katikati
ReplyDeletekwa mtindo huu kaka sokala bongo ndo TFF wanalizka hao, kwan ni aibu sana wloifanya hata mbele ya kocha aliyeonekana kuinua soka letu. cha ajabu nawashangaa TFF wametumia kigezo gani kumwita mchezaji aliyekaa nje ya uwanja zaidi ya miezi miwili. hawakuona wengine.
ReplyDeletehiki kikosi kina mapungufu makubwa sana ana maana bila sama na ulimwengu kwenye ligi yetu hakuna natural straiker alieitwa wakati wapo kina luzio,elias magili n.k sijaona jina la salum aboubakar sure boy sisi bado sana sio leo wala kesho tunataka kuvuna wakati hatujapanda
ReplyDeletehakuna kitu hapo sijamuona sure boy,elias maguri,luzio n.k tatizo tanataka kuvuna wakati hatujapanda kitu
ReplyDeleteHii siyo Taifa stars,ni Kidao Stars
ReplyDelete