Katika miaka ya hivi karibuni klabu ya Tottenham imekuwa ikjaribu kwa kila hali kuweza kumaliza katika nafasi nne za juu za msimamo wa ligi kuu ya England, ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kucheza kwenye michuano ya klabu bingwa ya ulaya. Pamoja na jitihada zote lakini wameshindwa kufikia malengo.
Msimu huu kama ilivyo misimu kadhaa iliyopita Tottenham wanaonekana kabisa hatma yao itabaki katika kucheza michuano ya Europa, hasa baada ya kipigo cha jana kutoka kwa Norwich.
Kuna pengo la pointi sita baina yao na Liverpool ambao wanashika nafasi ya nne na pia wamepitwa kwa namba kubwa ya tofauti ya mabao.
Zaidi ya £100million zimetumika katika kununua wachezaji, kubadili kocha, lakini hali bado inaonekana kuwa ile ile ya miaka yote.
Ikiwa watashindwa kuingia top 4 itakuwa sahihi hata kwa wale viongozi wa juu nao wajiangalie, maana kama watabaki nafasi ya tano wataishia kwenye Europa League kama msimu uliopita.
Ushiriki wa timu katika michuano ya Europa umekuwa moja ya sababu klabu hii kushindwa kupenya katika kundi la timu za juu katika Epl.
Kocha wao Tim Sherwood anakataa kwamba kufungwa kwao kwenye dimba la Carrow Road chanzo chake kimeanzia huko Ukraine walipotoka kucheza mechi ya Europa Alhamisi wiki iliyopita. Lakini hii ni mara ya tano msimu huu Spurs wanafungwa siku chache baada ya kucheza katika Europa League, vipigo ambavyo vimeifanya kufikisha jumla ya vipigo saba kwenye ligi.
‘Ilikuwa kama kufungwa mechi nyingine tu' hivi ndivyo kocha wa Spurs alivyoelezea kipigo cha 1-0 dhidi ya Dnipropetrovsk lakini kusafiri kwa safari ya umbali wa 3,000-mile baina ya siku ya Alhamisi na Jumapili ni sababu nyingine ya kufanya kwao vibaya kutokana na uchovu.
Hali huwa hivyo pia kwa timu zinazocheza Champions League katika safari ndani ya bara la ulaya, lakini michuano ya ulaya mechi zake zinachezwa baina ya Jumanne na Jumatano, ikimaanisha kwamba kuna nafasi ya kupumzika siku 3 au mbili - muda mwingine zaidi.
Utafiti uliofanywa na kocha wa kidachi Raymond Verheijen mnamo mwezi May 2012 uliangalia matokeo ya mechi 27,000 ndani ya bara la ulaya na kugundua kwamba timu ambazo zinacheza baada ya siku mbili baada ya mapumziko dhidi ya ambazo zinakuwa na mapumziko ya angalau siku tatu - zilionekana kuwa na 39% ya kushinda nyumbani na 42% ya kupoteza ugenini.
Kwa timu zinazocheza katika Europa League, utafiti huu unawagusa zaidi. Baada ya mechi ya Alhamisi usiku, Jumapili ndio hucheza mechi yao ya ligi hasa katika EPL, lakini bwana Verheijen anasema Jumatatu ingefaa zaidi badala ya jumapili.
Sherwood anataka taji katika CV yake, hivyo ni jambo la kueleweka anataka kushinda kombe la Europa. Lakini, mashindano haya kwa hakika yanakuwa kizingiti kwenye kiwango cha mechi za ligi.
Mashabiki wa Spurs, na mwenyekiti Daniel Levy, wanaweza wakakutana na hali ile ile waliyokutana nayo siku ya mwisho ya ligi kma msimu uliopita. Jinamizi la Europa league linawamaliza Spurs.
No comments:
Post a Comment