Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara na vinara wa ligi hiyo
timu ya Young Africans itashuka dimbani siku ya jumatano kucheza mchezo
wa pili wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Altay S.K iliyopo Ligi
Daraja la Pli nchini Uturuki.
Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi leo asubuhi na
jioni katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side kujiandaa na mchezo
huo wa siku ya jumatao ambao ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili
wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya klabu
Bingwa barani Afrika.
Kaimu kocha mkuu Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wote
wanaendelea vizuri katika kambi ya mafunzo, hakuna mchezaji ambaye
amekosa mazoezi hata siku moja na hali ya hewa inaruhusu kabisa kufanya
mazoezi hivyo vijana wanaitumia ipasavyo nafasi
hiyo.
Akiongelea mchezo wa keshokutwa Mkwasa amesema anawaandaa vijana
kuendelea kufanya vizuri katika mchezo huona ataendelea kutoa nafasi kwa
kila mchezaji aliyekuja nchini Uturuki apate nafasi ya kucheza kwani
kupata nafasi ya kucheza michezo ya kirafiki
huku ni njia ya kuwakomaza na kuweza kujiamani katika michezo ya
kimataifa.
Kesho timu ya Young Africans itafanya mazoezi mara moja tu asubuhi
kujiandaa na mchezo huo wa jumatano dhidi ya timu ya Altay SK ambayo pia
inajiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Daraja Pili nchini Uturuki.
Mara baada ya mchezo huo wa jumatano Young Africans itakamlisha
ziara yake ya mafunzo wiki ijayo kwa kucheza na timu ya Simurq Zaqatala
FC ya nchini Azberbaijan iliyopo katika Ligi Kuu ya nchi hiyo na msimu
uliopita ikiwa imekamata nafasi ya nne kwenye
msimamo wa Azerbaijan Premier League.
Imeandaliwa:Baraka Kizuguto
No comments:
Post a Comment