Na BARAKA MBOLEMBOLE
Tanzania ipo katika
mkakati mzuri wa kuhakikisha soka la Tanzania linapiga hatua na
kuondokana na hali ya unyonge wa kushindwa kufuzu hata kwa michuano ya
kimataifa kwa miaka mingi sasa. Timu ya Taifa ya Tanzania inajivunia na
rekodi yake ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980 nchini
Nigeria na michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, CHAN
mwaka 2009, nchini Ivory Coast. Kwa upande wa vilabu ni Simba pekee
ambayo inashikilia rekodi ya kufika hatua ya juu zaidi katika michuano
ya Afrika, iliweza kufika hatua ya nusu fainali mwaka 1974 ya michuano
ya klabu bingwa barani Afrika ( ligi ya mabingwa kwa sasa) na kutolewa
na Mehala El Kubra ya Misri, na iliwahi kufika hatua ya fainali ya
michuano ya shirikisho mwaka 1993, na kupoteza mbele ya Stella Abdjan ya
Ivory Coast.
Hayo ndiyo tunaweza kusema ni mafanikio ya juu zaidi
katika soka la Tanzania. Tangu wakati huo hadi sasa Tanzania imeendelea
kuwa na wachezaji wenye vipaji, ila wale wenye usongo wa kushindana
kimataifa wakizidi kupungua. Wakati timu ya Taifa ilipotwaa taji la
Castle mwaka 2001, wachezaji wengi walionekana kucheza kwa usongo
michuano hiyo, ni wakati ambao soka la Tanzania lilikuwa likichezwa kwa
mtindo wa kujitolea na mapenzi. Hali ni tofauti sana na miaka ya hivi
karibuni ambayo imeshuhudia timu ya Taifa ikifuzu kwa michuano ya CHAN,
na kutwaa ubingwa wa Challenge mara moja, mwaka 2010. Hali na hamasa ya
soka la mapenzi na kujitolea limeondoka.
Kwa sasa wachezaji wanahitaji pesa nyingi ili
kufanya kazi, iwe klabuni kwao au katika timu ya taifa. Hivyo ndivyo
inavyotakiwa kwa wakati huu ambao hali ya maisha ikizidi kupanda, na
soka kuwa kazio inayotoa malipo mazuri zaidi. Ila, kwa nini tunashindwa
kuwa bora kama miaka ya nyuma? Nje ya matatizo ya kiutawala, mfumo mbovu
wa mashindano, uendelezwaji wa wachezaji vijana, wachezaji wa Tanzania
wamekuwa na mapungufu mengi ya kiufundi katika uchezaji wao, inawezekana
mimi nikawa nimeyaona machache ila umefika wakati wa kuwapa ukweli
wachezaji wao kuwa wanatakiwa sasa
KUPIGA PASI ZA NGUVU,
Wakati
wa mchezo wa Simba na Yanga mwezi uliopita, wachezaji wa timu hizo
kubwa za Tanzania walionekana kuanguka anguka. Hao walikuwa wachezaji wa
timu kubwa zaidi, zenye makocha bora zaidi, inakuwaje kwa wale wa timu
kama Mgambo JKT, ambayo inakosa walau bajeti ya kugharamia na kuendesha
kambi yao ya timu?. Kiujumla wachezaji wengi kwa sasa wanakosa nguvu za
kutosha na hilo linatokana na wachezaji wenyewe kushindwa kujilinda na
kufanya mazoezi ya ziada.
Timu inayokosa stamina mara zote huishiwa pumzi na
hilo huchangia timu kutocheza kwa kasi. Wachezaji kama Amri Kiemba,
Wazir Mahadhi, Frank Domayo, Salum Abubakary, ni kielelezo tosha katika
hilo kwa kuwa mchezo wao wa taratibu hufanya timu nzima kucheza pasi za
za kudonyoa, na si kuupiga mpira. Itazame Barcelona inapokuwa katika
mchezo wowote tazama namna wanavyokuwa wanapasia wa kupigiana pasi za
nguvu hata kama wapo karibu karibu, wanaufanya mpira kukimbia kwa kasi
hivyo inawabidi waukimbilie ni hapo ndipo unaweza kuona ubora wao wa
pasi za haraka zinazoambatana na kasi. Wanakuwa timamu kimwili na
kiakili, na wanapasia mipira ya nguvu. Mtazame Ramadhani Chombo, ni
kiungo mwenye kipaji ila hapigi pasi bali huwa anagusa tu mpira, huyu
anawakilisha wachezaji wengi wa Tanzania ambao sasa wanatakiwa
kubadilisha stahili yao ya upigaji pasi na kucheza pasi ambazo zitakuwa
zinaikimbiza timu.
KUKIMBIA UWANJANI...
Nilikuwa
nikitazama mchezo wa Manchester City na Cardiff City ambao City
walishinda kwa mabao 4-2. Ukiitazama timu hiyo ambayo ilikuwa ikitamani
kucheza kama Barca, utaona hivi sasa wameongeza kasi katika uchezaji
wao. Pasi za nguvu na wachezaji wakikimbia uwanjani muda wote. Hakuna
kusimama. Bao ambalo lilifungwa na Jesus Navas ni kielelezo kuwa magoli
marahisi ya City yanatokana na wachezaji wake kukimbia mchezoni, Edin
Dzeko alipiga pasi laini, na Navas akatoka pembeni ya uwanja na kuukuta
mpira huo umeshapoa, umbali ambao alitoka Navas ulikuwa ni mrefu kuliko
aliotoka mlinzi wa Cardiff, ila ni Navas ambaye aliwahi kufika katika
mpira na kuupiga ' kibao kikali'. Aliwekewa pasi njiani naye akakimbia
huku akiwa na nguvu. Kama mchezaji unakuwa unasajiliwa kwa pesa ya
kutosha basi inakiwa kujituma na kujitolea kama Navas. Kukimbia uwanjani
ni jambo lisilofanyika kwa mastaa wa soka Tanzania.
KUCHEZA KWA MUDA....
Mara
nyingi timu za Tanzania zimekuwa zikifungwa mabao katika dakika 15 za
mwanzo, iwe kwa klabu au timu za Taifa. Makocha wengi huwaagiza
wachezaji wao kumaliza mechi mapema. Timu nyingi hushjambulia dakika 15
za kwanza, hupumzika katika robo saaa ya pili na hushambulia tena kwa
kasi katika robo ya mwisho. Hivyo wanakuwa na dakika 30 za kufanya
mashambulizi na dakika 15 za kupumzika mchezo. Hapa ni lazima wachezaji
wao na uwezo wa kumiliki mpira, kupiga pasi sahihi, kukaba kwa nafasi,
huku wakimtumia mchezaji mwenye sifa kama za Saimon Msuva kuwasaidia
katika mbinu zao. Mchezaji hasiyechoka haraka na mwenye kasi. Wachezaji
wa kitanzania hawachezi kwa maelekezo ya kuzingatia umuhimu wa kucheza
kwa muda uwanjani na hilo hupekea kukosa uelekeo muda mwingi uwanjani.
KUMSUMBUA MPINZANI HADI MPIRA WA MWISHO...
Arsenal
ilikuwa na mechi ngumu sana siku ya jumamoso dhidi ya mahasimu wao wa
London Fulham, ila baadae wakashinda kwa mabao 2-0 na kujiimarisha
kileleni mwa msimamo wa ligi kuu England. Wakati Fulham walipomuingiza
Darren Bent na kuwa na Dimitor Berbatov pia ilikuwa na maana kuwa kosa
lolote watakalofanya kurusu bao ndani ya dakika 10 za mwisho lingeweza
kuwanyima ushindi. Si mara moja Fulham kutoka nyuma na kupata sare au
ushindi dhidi ya Arsenal katika dakika za mwisho. Somo hilo alikuwa nalo
Laurent Koncienly ambaye alimfuata mshambuliaji wa Fulham na kumgasi na
akashindwa kufunga bao la wazi. Kukata tamaa na kuamini tayari umepitwa
ni jambo moja, ila kugeuka na kumfukuza mpinzani ni kitendo ambacho
huondoa hutulivu kwa mpinzani wako na hivyo anaweza kuingia katika hali
ya kuwa na mapepe na kushindwa kufanya maamuzi ambayo angeweza kuyafanya
kwa uhuru kama asingehisi kitu chochote kumharasi. Stamina, mbio, na
moyo wa kujituma ni mambo yenye msukumo sana kwa mchezaji wa kisasa.
KUFUNGA BAO SI MSAADA WA MWISHO KWA TIMU YAKO...
Wachezaji
wengine wanafikiri kufunga ni jambo muhimu sana kuliko kuisaidia timu
yao kupata ushindi wa jumla. Mtazame kiungo Jacky Wilshere wa timu ya
Arsenal. Jacky kwa sasa amekuwa akifunga mabao tofaoti na mwanzoni ila
mchango wake si mkubwa sana kwa timu. Sijui ni kusifiwa sana ama vipi
lakini hamasa ya Jacky hushuka anapofunga mabao. Wakati fulani Jose
Mourinho aliwahi kumtoa Joe Cole uwanjani japo alikuwa ameshafunga bao
muhimu la timu, baada ya mechi Jose alisema aliamua kumtoa nje Cole kwa
kuwa aliona mechi imekwisha kwa upande wake baada tu ya kufunga bao. Ni
hivi ndivyo ilvyokuwa kwa wachezaji wengi ambao wanapongia katika orodha
ya mara kwa mara ya wafungaji mabao katika timu hujisahau majukumu yao
mengine na kujikuta wakiicha timu ikiyumba.
MASHUTI YA MBALI....
Mbona
siku hizi hakuna wapigaji wa mashuti ya mita 18 na zaidi, wako wapi kina
Gerlad Hillu, Salvatory Edward, Abdi Kassim, SAid Sued, Mecky Mexime
wapya? Hao ni wachache tu, soka la Tanzania halina wapigaji wa shati ya
umbali mrefu na bahati mbaya limekosa hadi viungo wa kucheza pasi za
kupenyeza. Mtazame Yaya Toure, mchezaji bora hupiga pasi nne hadi sita
za aina tofauti mchezoni, na kupiga mashuti ya kushtukiza wakati wowote,
Sued na Mecky walikuwa walinzi wa pembeni ila ufiti wao ulikuwa
ukiwafanya kupasua na mpira kutoka nyuma na kusonga nao mbele kabla ya
kupiga shuti la kushtukiza. Wachezaji wa sasa hawapigi mashuti japo wapo
wanaojitahidi kufanya hivyo ila si kwa kiwango cha juu.
Nadhani umetoa wazo zuri sana, lakini tujiulize tatizo liko wapi? Mara nyingi huwa tunakuwa na uono wa tatizo lakini pia ni vyema zaidi pia tukawa na udadisi wa kwa nini hatuwi kama inavyotakiwa tuwe?
ReplyDeleteUmetoa mifano mingi mizuri lakini timu au wachezaji tajwa wanaofanikisha hayo ni Pro, fanya utafiti uangalie coaching progam zao halafu uje utazame Amateur coaching program utaona tofauti kubwa sana, na hii inatokana na mambo mengi sana ambayo cpati nafasi ya kuzungumzia yote ktk colum hii.
Labda kwa mtazamo wangu finyu na wa harakaharaka ningeishauri tff ipitie program za team ambazo angalau ni semi-profession halafu zijaribiwe kutumika na Vilabu vyetu vya league kuu, lakini bado utaona kuna mikwamo ya miundo mbinu ya soka ya nchi, uchumi wa vilabu na ufukara wa wachezaji wenyewe.
Na kabla ya yote pia tazama team za bench la ufundi za kila team, je zinafanana na team zetu? Pro team ina zaidi ya watu nane ktk bench la ufundi bila kuwaweka madaktari, walimu wa Gym na wataalam wa diet wanao support coaching program ya team.
Juzi tu Arsenal imefanya ukarabati wa daktari wa team ili kutazama kwa nini wachezaji wa team yao wanapata serious injury zinazowaweka nje muda mrefu kuliko team nyingine ktk EPL.
Shaffih Dauda kuna mengi sana ya kubadilishana mawazo iwapo utawekwa mtandao wa wadau kuchangia hoja kama hizi za msingi ambazo unazileta, na zikasaidia kujua tunaanzia wapi?
Niishie hapa kwanza, Im a soccer coach.