Kheri ya mwaka mpya ndugu watanzania
mahali popote mlipo. Ujinga ni sehemu ya
maisha na kila mwanadamu yawezekana ana mambo yake ya kijinga. Mimi natumia
muda huu kuja na ombi langu la kijinga kwa raisi mpya wa TFF. Ehe, ngoja
nisisahau, Natumia nafasi hii kuwapongeza wote mliopata nafasi ya kuingia
katika chombo hiki cha kuendesha mpira wa miguu Tanzania (TFF), pongezi zangu
zaidi zinakuja kwako Ndugu Jamal Malinzi “Tata
Okaiyuka, Omukama Akwebembele”. Kabla sijaanza na kuwasilisha ombi hili
naomba niongelee neno moja linaloitwa maadili, hii ni kwa sababu ombi langu la
kijinga kwa siku ya leo linahusu neno “MAADILI”. Hivyo kabla ya ombi langu hili
la KIJINGA kwa raisi Malinzi ni vyema nikaanza kutoa ufafanusu juu ya neno
MAADILI. Kwakuwa tumefundishwa na kukaririshwa mambo mengi ya kimasomo kwa
lugha ya kigeni bila sababu yoyote ile ya msingi nami naomba niendeleze kueleza
hili neno “MAADILI” kwa lugha ya kigeni ya kingereza. Kwa lugha hii ya mapokeo,
hili neno linaitwa “ethics”. Hivyo naanza kwa kulifafanua hili neno kama
ifuatavyo:-
The word
ethics is derived from the Greek word “ethos”, which means
"character," and from the Latin word “mores”, which means
"customs”. It has been defined as the rules of behavior pertaining to a
particular class of human action. They relate to moral principles that control,
influence or guide a person’s conduct or behavior so as to gain respect for
him/herself. (See Dr. Gerald Ndika, (2006):
Judicial Ethics in Tanzania: A Paper presented at a Primary Courts’
Magistrates’ Seminar, IJA, Lushoto)
(Msisitizo ni wa kwangu).
As
Socrates noted about ethics, "It is not just about any question, but about
the way one should live, thus, ethics do not only benefit the client but also benefit of those belonging
to the profession (See Plato,
The Republic
(A. Bloom, transl.), 1968, 352D ).
(Msisitizo
ni wa Kwangu).
Ikumbukwe pia kuwa neno maadili (ethics)
lina maana pana, haliishii tu kwenye kufuata matendo mema ya mwenyezi mungu au
amri zake mwenyezi mungu, maadili kwa maana yake pana ni zaidi ya apo, maadili
hujumuisha vitu vingi sana katika maisha. Hii imeelezwa vizuri na mwandishi Peter MacFarlane na namnukuu kama
ifuatavyo:-
“….we should not use the term 'ethics' to mean only
compliance with the Ten Commandments or other standards of common, basic
morality…” (See Peter MacFarlane, The
Importance of Ethics and the Application of Ethical Principles to the Legal
Profession, Journal of South Pacific Law, Volume 13 issue 1, 2009).
Na pia ni vizuri kutambua kuwa sio lazima maadili
ambayo mwanadamu anapaswa kuyafata lazima yawe yameandikwa mahala flani (ethics
are not necessary to be codified). Kwa mfano kuna jamaa yangu alikuwa
analalamika kuwa kuna Padre mmoja waga ananyoa fasheni/fashion, yaani ananyoa nywele
kwa mitindo ya kisasa na pia anachonga “O”kwenye ndevu zake, akawa anasema huyu
father/padre hana maadili kabisa, nami nilikubaliana naye kuwa kama kweli huyo
padre ananyoa hivyo basi hana maadili ingawa hatujui kama kwenye taratibu zake
za kitume amekatazwa kunyoa KIDUKU
kama MOSE IYOBO,(WCB) na kuchonga
ndevu kama NYOSI ELSAADAT wa F.M
Academia. Sina uhakika na hilo. Nikamdadisi kimakusudi huyu jamaa yangu
muumini mzuri wa kanisa kwa kumuuliza kwanini sasa unalalamika kwani kunyoa
hivyo ni kosa? Akanijibu, aha!, sasa mimi mtu aliyenyoa hivyo siwezi kuungama
kwake(Wakatoliki mnaijua hii), kwanza namuona msela mwenzangu na heshima
inapotea. Hapa nilipata somo, na kuelewa ambacho Mheshimiwa Ndika kama nilivyo
mnukuu hapo juu kuwa maadili/ethics influence respect.(heshima).
Tanzania imekuwa ni nchi amabayo
maadili yanaporomoka kwa kasi ya ajabu sana, watu wanaweza kutembea makalio
yako nje, hawa ni jinsia zote, Rushwa ipo idara zote(waulize vijana wa wacheza
mpira mkoa wa Dar-es-Salaam wanavyoombwaga rushwa hili wachaguliwe katika timu
za mikoa yao), waulize vijana wanaofanya applications za kazi, n.k. Nchi hii
imejaa majanga na wananchi wengi washavurugwa kiasi cha kutosha.(Asante Snura Mushi kwa maneneo mazuri ya
Kiswahili). Watanzania wenzangu yote mnayajua, hapa tatizo kubwa ni kukosa
maadili.
Tuachane na porojo hizi, maana mimi
tatizo langu mpaka nalalamikia rushwa ni kutaka kupata kila kitu kwa “ubwete”(Asante kwa neno hili Dr MacRegan
Kipara-Alex Chalamila wa O.K) kumbe lazima utoe kitu. Turudi kwenye mada
hii ya kuhusu neno maadili, hapo juu mheshimimiwa Gerald Ndika pamoja na mambo
mengine anasema kuwa maadili husaidia mtu kupata heshima(tafsiri isiyo rasimi).
Mwanafalsafa (sio mwana FA mwanamuziki
aliyeimba Bila Kukunja Goti), akha! namuongelea Plato(Aristocles), mwanafalsafa wa Kigiriki ambaye aliwahi kusema
kama nilivyomnukuu hapo juu kwamba kuwa na maadili si kwa faida ya mteja bali
hata kwa mhusika katika fani husika. Yaani kama ni mcheza mpira si kwa faida ya
timu yako bali ni kwa faida yako pia. Kwamfano kama ukienda kucheza ndondo YOMBO(katika fainali ya mwenyekiti wa mtaa)
na ukaumizwa hasara si kwa YANGA tu,
bali pia kwako kwani nafasi yako ya kucheza uwanjani inaweza kuchukuliwa na
mchezaji uliyekuwa unamuweka benchi na ukipona husiweze kuichukua tena, na kama
ni ndoto ya kwenda nje basi inaweza kuishia hapo. Hila ukijitunza vizuri faida
si kwa klabu yako tu bali kwako pia, yawezekana nawe MOSE KATUMBI akakupeleka
TP MAZEMBE, ni kweli klabu yako itapata hela ya mauzo(Ingawa najua hela ya mauzo ya wachezaji wetu waga hatujui inaendaga
kwenye benki account ya nani, wanachama na mashabiki wa Simba ni mashaidi kwa
hili) nawe pia kama mchezaji mshahara mzuri itakuwa haki yako.
Kukosa maadili ni pamoja na kuchukua
hela ya mauzo ya mchezaji bila klabu yake kujua, kucheza kwa dharau huku
ukituliza mpira kwa makalio ukimungoja beki umpige tobo, pia ni pamoja na
kukataa kukaa na wenzako baada ya kufanyiwa mabadiliko na ukaondoka moja kwa
moja, ni mengi tu tena kama nilivyotangulia kusema hapo juu si yote yataandikwa
katika document moja, mengine hayaandikwi.
Tanzania imekuwa kichwa cha
mwendawazimu katika nyanja mbalimbali za kimichezo, iwe riadha, kikapu, mpira
wa miguu, n.k, tatizo kubwa kama nilivyotangulia kusema ni kukosa maadili.
Aliyeshinda mkanda wa kimataifa wa ngumi(ingawa watanzania kama kawaida yao
walisema ni mkanda feki) nasikia kidogo ndoa yake ivunjike baada ya kuanza
ulevi, akashindwa kujiandaa kwa ajili ya mapambano mengine, na kuna kipindi
akaenda nje ya nchi kupigana bila hata kocha wake kujua yote hii ni kukosa
maadili. Kuna mifano mingi tu katika
hili, kila mtu mwenye akili timamu anayajua na ana yake moyoni.
Tukija katika mpira wa miguu hapo ndo
usiseme, makocha na wachezaji wengi hawafati maadili ya mchezo huu pendwa hapa
nchini. Ndugu Jamal Malinzi ulitoa ahadi
nyingi zenye malengo ya kuinua mpira wa Tanzania na wapiga kura (wajumbe) kwa
niaba ya watanzania wakaridhia kukupa wewe kiti cha urais wa TFF. Tayari
umeanza kazi ukiwa na timu mpya kabisa baada ya kuzivunja kamati zote alizoacha
Ndugu Leodgar Tenga, naamini ni kwa nia nzuri tu(ingawa kuna malalamiko ju ya
hilo). Baada ya kuzivunja kamati, ndugu Malinzi
uliunda timu ya jopo la makocha wa mpira wa miguu kujadili nini
kifanyike kuitoa Tanzania hapa lipo kwenda hatua nyingine mbele kwa maendeleo
ya mpira. Hivi katika ripoti yao pamoja na mambo mengine waliweza kuandika kuwa
kukosa maadili ni chanzo cha sisi Tanzania kushindwa kusonga mbele katika
mchezo wa soka? Basi kama halikusemwa kwenye ripoti basi nami ngoja nichangie
kuwa chukua yote walioleza katika ripoti hila na hili la maadili nakuomba
uliweke, we ukiulizwa limetoka wapi sema ni mtanzania mmoja tu mwenye kuupenda
huu mchezo. Si ulisema kila mtanzania anao wajibu katika kuliinua soka letu?
Nami ndo mchango wangu ingawa najua ni ngumu kusoma hili andiko.
Ndugu Malinzi kama ujuavyo kila kitu
hili kufanikiwa lazima ushiriakiano wa dhati kutoka kwa wadau/stakeholders uwe
juu, waweza kuwa na mipango mizuri lakini ukakosa ushirikiano, ni mbaya zaidi
unapokosa ushirikiano kutoka kwa watu ambao mipango inayo pangwa ni kwa ajili
yao, yaani kukosa support kutoka kwa targeted group. Yaani pale walengwa
wakiyaacha maadili ya kazi yao. Hapa ni kama baba unalipa gharama kubwa ya ada
kwa ajili ya mwanao, unampeleka shule nzuri yenye kila kitu lakini yeye hataki
kusoma, lazima kama mzazi malengo yako na ndoto zako kumuona mwanao akiwa msomi
mzuri zitashindwa kutimia.
OMBI LA KIJINGA.
Ndugu Malinzi wakati Rais aliyekutangulia
anaingia madarakani aliletwa kocha wa kigeni, wote unawajua na mpaka sasa
bado timu ya taifa ipo chini ya kocha wa
kigeni, saivi tunaye Kim Poulsen na baadhi ya wanachama wako, yaani vilabu,
wanao makocha wa kigeni( Simba, Yanga, Azam,na nyinginezo ni mfano katika
hili). Rais wa sasa wa Jamhuri ya
Mungano wa Tanzania amegharimikia kocha wa Timu ya Taifa, wafadhili na wamiliki
wa vilabu nao wamefanya vivyo hivyo kwa timu zao.
Sasa makocha wa kigeni wenye ngozi
nyeupe na nyeusi tumewazoea hapa Tanzania, saivi twaweza kujua ufanisi wao na
ukanjanja wao, Pia Tanzania sasa tunao
makocha wazawa wenye vyeti vizuri (wengine wamepata Leseni B ya CAF hivi
majuzi). Hivyo suala la makocha walau twaweza sema uko akuna shida sana.
Ndugu Malinzi sasa mimi nakuja rasimi
baada ya porojo nyingi na ombi langu la “KIJINGA”, ni hivi, kama Raisi Jakaya Mrisho Kikwete alileta kocha
wa kigeni kwa lengo la kuinua mpira wetu basi nakuomba nawe saivi jiandae
kumuomba raisi ajaye atuletee kwa gharama ya serikali mchezaji walau mmoja wa
kigeni aje kufundisha wachezaji wetu kuishi kama wana taaluma wa mpira/ yaani kuishi
kiprofessional. Hivi serikali haiwezi kumlipa hata Thiery Henry akaja akafanya
kazi hii? Si inaonekana hivi karibuni ataacha kucheza mpira huko aliko
Marekani? Serikali yetu haishindwi, wewe waconvice tu watakuelewa. Au wamlete anayecheza saivi ulaya kwa mfano
Chiek Tiote, tena huyu mwafrika mwenzetu aje afanye hi kazi. Inawezekana kweli?
Hapana, Hili ombi limekaa kijinga sana maana hakuna mchezaji wa kulipwa toka
ulaya ataacha mihela aje kufundisha maadili Tanzania. Haitawezekana, labda
tumtafute aliyestaafu kucheza mpira aje kufundisha haya, tuwaombe Airtel
wamlete Fortune si kastaafu kambumbu Yule aje akae mwaka. Achana na hiyo, nimekumbuka,
Stewart Hall( Kocha wa Zamani wa AZAM AFC) kapewa Academy nina imani kati ya
mambo atakayo fundisha ni kuishi kiprofessional kwa kufuata maadili na miiko ya
kiuchezaji. Asante Mungu, nina imani wachezaji wataokulia kwenye hii academy
watakuwa maprofessional wa ukweli. Ila mpaka tuje tuvune uko ni muda mrefu
sana, ila atasidia.
Swali ni kwa hawa ambao saivi bado wanacheza, na bado wana miaka mingi mbele
kucheza mpira na lengo lako Ndugu Jamal Malinzi ni kuona Tanzania ikishiriki
mashindano ya kimataifa kwa mafanikio. Sasa naona bado ombi langu la KIJINGA
niendelee nalo, ni hivi naomba aletwe mtu ambaye atawanusuru hawa wachezaji
wetu hili nao angalau waishi kiprofessional. Maisha ya wachezaji wetu na
mienendo yao inatia shaka kama lengo lako ndugu rais wa TFF litatimia. Haiwezekani
kufikia malengo yako mkuu wa TFF kama leo hii mchezaji wa ligi kuu anaishi kama
mpiga debe wa stand kisa eti hasionekane anajidai, mchezaji anakaa kijiweni na
masela wakipuliza naye anapuliza hapo hapo, mchezaji anacheza ndondo bila
kujali afya yake, ni mengi bwana hata nawe unayajua.
Kwa mfano ulio hai, mchezaji unacheza
AZAM F.C (Timu yenye kila kitu katika soka la bongo) na wewe pia ni kiungo wa
kutumainiwa wa Taifa Stars na Kilimanjaro Stars na majuzi kati umepewa tuzo ya
mchezaji bora wa mechi kati ya Kilimanjaro Stars na Zambia kwenye mashindano ya
chalenji leo hii unaonekana kwenye ligi ya diwani tena una siku moja umetoka
mapinduzi cup Zanzibar.
Hujui tu ulivyoniumiza, Naikumbuka
sana hela yangu niliyoitumia kununua kifurushi (MB) niangalie kwenye internet
highlights za mechi zenu mkiwa Zanzibar, nilitaka nikuangalie ulivyokuwa unatembea
katikati ya uwanja. Ilikuwa lazima niingie gharama kukuona wewe supa star,
kukuona pasi zako murua, kukuona unavyosababisha goli alilofunga Himid Mao.
Yaani wewe niliamini hili mtu aenjoy
mambo yako ya uwanjani lazima aingie gharama/alipie aende Taifa, Chamazi, au
afuatane na Azam ikiwa inaenda mikoani au aifuate Timu ya Taifa au alipie kwa
wenye vibanda vya mpira akuone na aje asimulie wale waliokosa mia tano ya
kulipia, aweke na uongo mwingi huku akitukuza kipaji chako. Wewe ni si mtu wa mchezo bwana, kama
Waingereza wanamtukuza Lampard wakati hakufikii kipaji cha kuuchezea mpira
kwanini nasis tusikutukuze?
Nilitamani nikutane nawe kwa bahati
kwenye moja wapo ya SHOPPING MALL yoyote hapa Dar ukifanya shopping nikuombe
tupige wote picha na unisainie mahali popote ningeona panafaa kwa muda huo,
nikirudi mtaani nianze kutangaza kuwa leo nimekuona na ukakubali kuoiga name
picha, au umetia sahihi kwenye shati langu jeupe. Mbona wangenikoma jamani,
duh, kumbe niliingia cha kike, sivyo ulivyo nilikuwa naota ndoto ya KIJINGA.
Niliumia sana na kukereka nilipokuona
mtaani kwetu tena si kwa bahati mbaya, yaani ukiwa umedhamiria kuja kucheza
ndondo. Nilikusogelea ghafla ile hamu ya kukuona ikaisha maana sikutegemea
kukuona maeneo yale, na thamani yako kwangu kama shabiki wako ikaisha pale,
mbaya zaidi pale watu/mashabiki walivyokuwa wanakutukana matusi. Najua
kutukanwa na mashabiki kwa mchezaji ni jambo la kawaida, lakini linakuwa la
ajabu pale mchezaji wa kariba yako unapotukanwa na mashabiki wa mbagala kuu wakati ulipaswa kutukanwa
na mashabiki wa timu za ligi kuu. Tena kwa uwezo wako uwanjani wewe unapaswa
kuzomewa na mashabiki wa Ajax cape town, TP Mazembe, na nyinginezo toka nchi
kama Dernmark, Ufaransa, Sweeden, n.k, maana ungekuwa umefanya hesabu hii ndogo
(miiko + maadili=Kujitambua), wewe ungekuwa unacheza ligi za huko. Baada ya
dakika tisini kwenye ule uwanja wa mchanga wenye vipimo vya kubuni ile thamani
niliyokuwa nakupa iliisha ghafla, na siko peke yangu wapo wengine wengi. Wewe
si mtu wa kuonekana sehemu zile ukicheza mpira wa ushindani, hapana kijana
mwenzangu, hapana.
Inasikitisha sana wachezaji wetu
wapendwa hamjitambui, hivi mnajua hao mnaotaka kuwaridhisha (masela wa kitaa)
waga wanawacheka pale mnaposhindwa kujieleza mbele ya vyombo vya habari,
wanasema ati hamjui kingereza. Sasa hutajuaje jinsi ya kuongea na vyombo vya
habari wakati muda wote wewe ni ndondo tu, vijiweni na glossary za kitaa. Mkihojiwa na waandishi wa kitanzana mnasema
mna ndoto ya kucheza ulaya, kweli? Hapana, nayo ni ndoto ya KIJINGA. Hiyo ndoto
inaanza kutimilika kuanzia kwako, kwanza jiweke kiprofessional then mengine
yatafuata. Leo hii watanzania tunamuona DIAMOND PLATNUMZ anavyong’ara kimuziki,
na akikwambia anataka siku awe kama P-Square au Usher kwanini usikubali na kumuombea
kwa Mungu afike huko, yeye kajiweka kiprofessional, wadada wakimuona wanadata,
wanaomba awasainie mpaka kwenye mashati yao ya shule, hawajali. Huyu ni mtu
anayejitambua anafanya nini (achana na
isues zingine za upande wa pili mnazojua juu yake, hata Ashley Cole,
Ronaldinho, na Rolnaldo wote kwenye hiyo sector hawajambo). Mimi nikisikia
katoa video ya wimbo nakimbilia YOU TUBE kuona kafanya nini PLATNUMZ. Kamuulize PLATNUMZ kajifunzia wapi kuongea na
vyombo vya habari? Nani kamfundisha English? Tulimuona wakati amekaribishwa BBA
alichokifanya, tuliduwaa, MAGAZETI pendwa yakaandika sijui kafundishwa na
naniii!!! Sawa, ata kama alijifunzia Mchikichini si tayari anajua? Amejiandaa
kuwa wa kimataifa si siri.
Kuna vijana huku mtaani wakisikia
Taifa stars au Kilimanjaro stars inacheza na wakajua yupo Samatta lazima
wakalipie kwenye banda la mpira kumuona Samatta. Wao wanasema wanatamani wawe kama yeye,
unajua kwanini? Mi naamini si kipaji chake ila anavyojiweka nje na ndani ya
uwanja.
Ndugu Malinzi naomba ulifanyie kazi
ombi langu la “KIJINGA”, Raisi ajaye( sijui
wa Tanganyika, ama Zanzibar, ama wa Muungano, maana hii rasimu ya katiba
nasikia walioisoma wanasema tutakuwa na marais watatu, wewe chagua kati ya hao)
atuletee mtu ambaye kazi yake itakuwa ni kuwafundisha wachezaji wetu wenye
vipaji vilivyotukuka jinsi ya kuishi kama maprofessional. Hiyo ndo iwe kazi
yake tu hapa Tanzania, na ikibidi kila klabu iajiri mtu wa aina hiyo aweze
kuwafunda wachezaji wetu wapendwa jinsi ya kuishi angalau kama Tresor Mputu kama kuishi kama Christiano Ronaldo ni ngumu.
Ndugu Jamali Malinzi ombi langu la
KIJINGA ndio hilo, Please! nakuomba katika mambo yako nalo hili uliweke. Enyi
wachezaji wetu namaliza kwa kusema kuwa ombi langu la kijinga lilikuwa kwa
ajili ya Raisi wa TFF sio ninyi, kwenu sio ombi ni lazima muishi kama wachezaji
wa mpira sio wa bao kama mnataka kwenda huko ulaya mnakokutaja kila mara, na
ngoja niliweke kwenye lugha hii ya kidhungu (maana kabila linaruhusu), Hey Tz Footballers,
ethical responsibility and duty
are an inherent part of your profession as a footballer.
ASANTENI SANA,
ELPHACE RWESHABURA
ELPHACE RWESHABURA
.
Ahsante sana mtoaji wa makala hii, nikweli kabisa wchezaji wetu hawajitambui imefika wakati wanatakiwa wawe ni wenye kujitambua, lkn mwandishi jarib kuwa na ufupishe wa maneno watu wakuelewe vzr umekusudia kuwafahamisha maadili lkn longolongo nyingi sana mpaka kufika ktk fundisho hilo la maadili,yani huyo mlengwa atasoma makala hii lkn mpaka akifika katikati ya kusoma kashasahau mwanzo jinsi longolongo zilivyokuwa nyingi,
ReplyDeleteWatanzania tunapenda sana njia za makato...Barrack Obama licha ya majukumu yake anapata muda wa kusoma kitabu cha kurasa 500.Leo hii tunalalamika mwandishi kuandika kurasa tatu.
DeleteKumbe tusiwalaume wachezaji wanaolalamika mzaoezi ya kocha fulani wa kigeni kuwa ni magumu, ni zao la jamii yetu ambayo inapenda kila kiwe 'vodafasta'.
Makala nzuri sana. Lovely efforts from the author.
Barak obama ni mtume mpaka umtolee ushahidi
ReplyDelete