Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafanya
ziara ya siku moja kutembelea kituo cha mpira wa miguu wa vijana cha
Alliance cha jijini Mwanza.
Lengo
la ziara hiyo ni kuangalia jinsi Alliance inayoendesha shughuli zake
ili Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liweze kushirikiana na
kituo hicho kwa karibu.
Rais
Malinzi katika ziara hiyo atakayoifanya keshokutwa (Januari 15 mwaka
huu) atafuatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu kwa Vijana,
Ayoub Nyenzi na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ramadhan Nassib.
Alliance
inatarajia kufanya mashindano yatakayoshirikisha vituo vyote vya
kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana (academy) wiki ya tatu ya Februari
mwaka huu jijini Mwanza.
Mashindano
hayo yatashirikisha timu za umri wa miaka 13, 15 na 17 ambapo Alliance
itagharamia malazi, chakula na usafiri wakati timu hizo zikiwa jijini
Mwanza.
No comments:
Post a Comment