MUDA mfupi uliopita klabu ya soka ya Yanga imetangaza
kusitisha mkataba na kocha wake Ernest Brandts baada ya kutoridhishwa na
mwenendo wa timu hiyo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga,
Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts ambaye ni raia wa Uholanzi
umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu
juu ya hali hiyo.
“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na
ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga,
kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.
Tetesi
za Brandts kutimuliwa zilizagaa jijini Dar es Salaam tangu jana muda
mfupi baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kwamba hata kama klabu
itaamua kuachana na kocha huyo itafuata taratibu zote.
Uamuzi
huo wa Yanga unaonekana pia kuchagizwa zaidi na kipigo cha mabao 3-1
dhidi ya Simba katika mchezo maalum wa kirafiki maarufu kama Nani Mtani
Jembe uliochezwa wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
i support that,timu haijabadilika alafu anashindwa imudu?ni kocha mzuri bt 4sure katuangusha..2ngekuwa 2mebadili timu ndo angekuwa na utetezi bt wa2 walewale zaidi ya 2yrz bd anachemka bana,Young africaans 4lyf..NYUMA MWIKO MBELE DAIMA
ReplyDeleteMoja kati ya maamuzi mabovu kbisa kufanywa na uongozi wa Yanga,wachezaji wanasajiliwa na uongozi bila kumshirikisha kocha,halafu mwisho wa siku mnamfukuza kwa kufungwa mechi moja tu??? halafu mnajiita viongozi?? fanyeni yenu kama viongozi msimuingilie kocha !!!!
ReplyDeleteBonanza lamfukuza kocha jangwani,manji alisema ni bonanza vp tena kocha kufukuzwa kwa sababu ya bonanza lisilokuw na point?
ReplyDeleteBado mbona huo ndo mwanzo
ReplyDeletewafa maji yanga bonanza linafukuza kocha ? tatizo wanaongeza sana a mpira wa sasa sio wa kuongea na magazeti ni uwanjani badala waandae timu kwa kutafuta wachezaji wanaowafaa wao analeta kukomoa simu pinzani
ReplyDeleteuamuzi sahihi kabisa kwa faida ya timu,ukiangalia kwa jicho la tatu utaona kabisa mwalimu uwezo wake ulikuwa umefikia mwisho na imefikia hatua amekosa mbinu mbadala(plan b).
ReplyDeleteBongo bhana,kw mtndo huu soka letu halitapnda
ReplyDeleteeti wanasema timu imeshuka kiwango.kwa mechi zipi?mana wao wapo top ktk VPL,au kwa hiyo mech ya juz?viongoz wanafanya usajil bila kumshilikisha kocha au wanazan majina ndo yatashinda ubingwa?wawaulize wenzao REAL MADRID pamoja na usajil wao wamajina ktk kipindi cha miaka 6 nini wamevuna?viongoz waache ushamba wao wafanye kaz ilowaweka ktk uongoz na kocha kama kocha apewe nafasi yake ya ukocha na kama atahitaj mchezaji yeye ndo anayejua mchezaji yupi anamuhitaj ktokana na nafasi ambayo imepwaya.
ReplyDeleteBozra hujui kitu au we simpenzi wa yanga mwalimu hana plan B unategemea nini,acha wenye Mapenzi na washughulike na matatizo ya YANGA.
ReplyDeleteBozra mambo ya mpira na wewe wapi na wapi,mwalimu Hana plan B kufukuzwa unaita uamuzi mmbovu
ReplyDeleteBRANDINA DO NOT BE WARRIED COACH ARE HIRED TO BE FIRED, BY MKINGA
ReplyDeleteyanga tulieen mpira sio kuangalia timu pinzani imesajili nan bali ni kushirikisha bech la ufundi.mfan okwi amesajiliwa kocha anashangaa which means kocha hakushirikishwa.tuige soka la ulaya tutafika
ReplyDelete