WAKATI Arsenal inaonekana ipo juu katika Ligi Kuu ya England huku matokeo ya hivi karibuni ya mechi zake yakishtua watu, nayo Liverpool haipo nyuma na inaweza kufanya jambo la kushangaza katika ligi hiyo.
Kama unakumbuka, mwaka 1988, Liverpool ilitwaa ubingwa wa England kwa tofauti ya points tisa. Mwaka 2011, Manchester Utd walibeba ubingwa huo kwa tofauti ya points tisa pia.
Mwaka 1989, Liverpool ilipoteza ubingwa wake iliyoutwaa mwaka 1988 kwa bao lililofungwa dakika za majeruhi. Nayo Man United mwaka 2012 ilishindwa kutetea ubingwa wake baada ya bao la dakika za majeruhi la Man City
Baada ya kupoteza ubingwa mwaka 1989, mwaka uliofuata Liverpool ikarudisha tena ubingwa mikononi mwao kama ilivyokuwa kwa Man United mwaka huu ilipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Mara tu baada ya kutwaa ubingwa, Liverpool ilibadilisha kocha, kutoka kwa Kenny Dalglish raia wa Scotland na kumpa kazi raia mwingine wa Scotland, Graeme Souness.
Hata Man United nayo muda mfupi baada ya kutwaa ubingwa mwaka huu, kocha wake Sir Alex Ferguson alibwaga manyanga na nafasi yake ikachukuliwa na David Moyes.
Tazama Liverpool ilivyopotea tangu ilipoachana na kocha wake mwaka 1989 muda mfupi baada ya kutwaa ubingwa na hadi leo hii inaangaika kutwaa ubingwa na mazingira yanaonyesha hali ni mbaya na haina nafasi ya kutwaa ubingwa.
Hivyo mashabiki wote wa Man United lazima wachukue mfano huu wa Liverpool na hii inamaanisha kwamba, Man United itatumia muda mrefu zaidi kutwaa ubingwa na kama hazitokuwepo jitihada za haraka itaichukua miaka mingi kwa klabu hiyo kutwaa ubingwa kwa mara nyingine.
Kama Liverpool pamoja na nguvu iliyokuwa nayo wakati huo, ilishindwa kuendeleza ubabe wake hata Man United nayo sasa inapita katika njia zile zile ambazo Lierpool wamepita. Na mazingira yote yanaonyesha uwezo wa Man United utazidi kupungua siku hadi siku.
No comments:
Post a Comment