SAA 9:50 Alasiri ya leo,
straika mpya wa Yanga, Emmanuel Okwi ametua nchini kutoka Uganda tayari kwa
kuitumikia timu yake mpya ambayo imemsajili hivi karibuni kutoka SC Villa.
Mashabiki zaidi ya 600
walijitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kumpokea
Okwi ambaye alipokewa na viongozi wa Yanga akiwemo Ofisa Habari, Baraka
Kizuguto na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Seif Ahmed ‘Seif
Magari’.
Muda mfupi baada ya kutoka
nje na kukutana na mashabiki hao, Okwi aliwasalimia kisha akauzngumza kidogo na
waandishi wa habari ambapo alisema kwa kifupi; “Nimekuja kufanya kazi.”
Okwi alisema yeye ni
mchezaji wa kulipwa na anachofahamua sasa ni kutimiza wajibu wake wa kutumikia
mkataba wake aliosaini hivi karibuni kuichezea Yanga.
Muda mfupi baada ya kuzungumza
na waandishi wa habari, msafara wa Okwi kuelekea makao makuu ya klabu ya Yanga
ulianza huku akitumia gari aina ya Toyota Brevis Ai 300 lenye namba za usajili
T 457 CRQ.
Msafara huo ulikwenda
moja kwa moja mitaa ya Jangwani na Twiga yaliyo makao makuu ya Yanga na moja kwa
moja alisaini kitabu cha wageni kasha akapanda juu ya jengo la ghorofa la klabu
hiyo na kuwasalimia mashabiki waliojitokeza.
Baada ya kushangiliwa
na mashabiki hao, Okwi aliondoshwa kutoka Jangwani na kupelekwa hotelini ambako
viongozi wa Yanga wakiongozwa na mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo,
Mohamed Binda.
Kesho asubuhi Okwi
anatarajiwa kuanza mazoezi na kikosi cha kwanza kwenye Uwanja wa Bora
Kijitonyama.
APEWA JEZI NAMBA 25
Okwi amezaliwa tarehe
25 Desemba, hivyo mara tu baada ya kutua nchini alivalishwa jezi namba 25
ambayo hapo kabla ilikuwa ikivaliwa na beki Ibrahim Job.
Jezi hiyo ilikuwa pia
ikivaliwa na Okwi wakati anaichezea Simba ambayo aliachana nayo Januari mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment