CEO wa klabu ya Manchester United Ed Woodward amesisitiza kwamba klabu yao haihitaji kuendelea kushinda mataji ili kuweza kuendela kuvutia wadhamini.
United imeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa deni lao kutoka na kuongezeka kwa wadhamini wengi kwenye klabu hiyo.
Matokeo ya robo ya kwanza ya mwaka wa kifedha umeonyesha ongezeko la mapato katika udhamini, ambayo yameendelea kuongezeka, huku madili kibao ya udhamini yakiendelea kusainiwa.
Na Woodward ana uhakika kwamba jambo litaendelea haijalishi hali ngumu ya matokeo wanayopitia United katika kipindi hiki.
Akiongea na jarida la fanzine ‘United We Stand’, katika mahojiano yaliyofanyika mwezi wa 10 lakini yamechapishwa leo baada ya mchezo wa jana dhidi ya Everton, Woodward anaelezea sababu zake juu ya mtazamo wake.
'Ukweli halisia ni kwamba huwezi kushinda kila siku.
'Angalia mfano mzuri Liverpool. Bado wanauza namba kubwa ya jezi na dili zuri na la pili kwa ukubwa katika Premier League.
'Wana moja ya mkataba mzuri wa kiufundi - na hawajashinda ubingwa wa ligi tangu 1990.
'Ikiwa tuna mwaka mmoja m'baya then tunao msuli mkubwa wa kiuchumi wa kubadilisha timu. Tuna uwezo mkubwa wa kiuchumi ambao badala ya kuuza wachezaji watatu na kununua watatu, sie tunaweza kununua watano.'
Na msuli huo wa kiuchumi unamaanisha kwamba haki za kubadilisha jina la uwanja wa Old Trafford hazitouzwa kamwe.
'Ni muhimu kwa Old Trafford kubaki Old Trafford,' alisema.
'Akina Glazers ni watu ambao wana misingi ya kufuata sana utamaduni.
'Watu wametuuliza kama tunafikiria kuuza haki za jina la uwanja, hatuwezi kufanya hivyo.'
No comments:
Post a Comment