Kampeni ya Nani Mtani Jembe
iliyozinduliwa Oktoba 6 mwaka huu itamalizika Jumamosi kwa klabu za
Simba na Yanga kuchuana vikali pamoja na kuwania Sh milioni 100 zilizotengwa na
Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa timu hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe alisema wanakabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh milioni 6.8 kwa ajili ya kuzipa mwonekano mpya timu hizo katika mechi hiyo.
“Bado tunaendelea kuhesabu siku kuelekea siku ya mwisho ya
kampeni yetu ya Nani Mtani Jembe Desemba 21 mwaka huu, Yanga ndio hadi sasa
wanaongoza wakiwa na Sh Mil 91 na Simba wao wana Sh Mil 9,” alisema.
Katika kampeni hiyo ya
Mtani Jembe mteja atabandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium
Lager ataona namba. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na
namba hiyo ya kwenye kizibo kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa nafasi
timu yake.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ aliwashukuru wadhamini
hao Bia ya Kilimanjaro kwa vifaa hivyo huku akitamba timu yake kuibuka na
ushindi.
Naye Ofisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto aliwashukuru
wadhamini hao kwa kuwafanyia mambo mazuri na kuahidi kuendeleza mambo mazuri
kwao na wataibuka na ushindi katika mechi hiyo.
George Kavishe - Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini Simba na Yanga akimkabidhi
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itangare (Mzee Kinesi) na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Simba, Ibrahim Masoud (Maestro) jezi maalum
itakayotumika kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe itakayozikutanisha Simba na
Yanga kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumamosi tarehe 21
Desemba. (Picha: Executive
Solutions).George Kavishe - Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini Simba na Yanga akimkabidhi Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto jezi maalum itakayotumika kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe itakayozikutanisha Simba na Yanga kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumamosi tarehe 21 Desemba. Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Yanga, George Simba. (Picha: Executive Solutions).
George Kavishe - Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini Simba na Yanga akiwakabidhi Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itangare na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto jezi maalum zitakazotumika kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe itakayozikutanisha Simba na Yanga kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumamosi tarehe 21 Desemba. (Picha: Executive Solutions)
Inamaanisha mashabiki wa Yanga ni walevi kupindukiaa?
ReplyDelete