ED 305 TIMES
Mlinda
mlango namba moja nchini Juma Kaseja Juma leo ameanza rasmi mazoezi na
timu yake mpya wa Young Africans katika uwanja wa Bora Mabatini -
Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na
mashindano ya kimataifa.
Kaseja ambaye amesajiliwa na Young Africans kipindi cha dirisha dogo
ataitumikia timu yenye makao makuu yake mitaa ya Twiga/Jangwani kwa
kipindi cha miaka miwili mpaka mwaka 2015 mwezi wa Disemba.
Mara
baada ya kufika mazoezini leo asubuhi Kaseja alipokelewa na kocha mkuu
Brandts, kocha msaidizi Minziro pamoja na wachezaji wenzake wa Yanga,
huku golikipa Ally Mustapha "Barthez" akimuongoza katika mazoezi yao ya
magolikipa chini ya usimamizi wa kocha wa makipa Razak Siwa.
Kocha
wa makipa Razak Siwa amesema ujio wa Kaseja ndani ya Yanga ni mzuri,
kwani kwa sasa ana magolikipa wanne wote wenye uwezo wa hali ya juu,
hivyo jitihada za mchezaji ndio zitakazompa nafasi ya kuanza katika
kikosi cha kwanza.
Kikosi cha Young Africans kinaendelea na
mazoezi wiki ya pili sasa katika uwanja wa bora-mabatini Kijitonyama
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili, mashindano ya Klabu
Bingwa Afrika na mchezo wa hisani wa Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC
Disemba 14, 2013.
Source:www.youngafricans.co.tz
No comments:
Post a Comment