WAKATI straika mpya wa Yanga,
Emmanuel Okwi akitua nchini tayari kuitumikia timu yake mpya, Shirikisho la
Soka la Uganda (Fufa) limesema mchezaji huyo ni halali kuichezea Yanga na ndiyo
maana walikubali kutoa hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC).
Ofisa Mtendaji mkuu wa Fufa, Edgar
Watson ameuambia mtandao huu kwamba, anachojua kama bosi wa Fufa ni kwamba ni
kweli Okwi amesaini kuichezea Yanga na shirikisho lake limetuma ITC kwenda Tanzania
kwa Yanga ili aweze kuichezea timu hiyo.
“Kwanza nataka kuweka wazi kwamba,
Okwi alikuwa na kesi dhidi ya timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia juu ya masuala
ya mkataba, Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) lilimruhusu kucheza kwenye
klabu ambayo anaitaka kwa muda maalum.
Okwi alipewa kibali maalum, hivyo si
kweli kuwa alikuja kucheza SC Villa ya hapa (Uganda) kama mchezaji wa mkopo,
huyu alipewa kibali maalum sasa hapo kuna tofauti ya kibali maalum na mkopo,”
alisema Watson.
Alisema Okwi aliruhusiwa kucheza na
Fifa na ruhusa ambayo amepewa haikuwa ikimzuia kuhamishwa au kusajili kwenda
klabu nyingine, hakuna mahali anapozuiliwa kusajiliwa bali kilichofanyika ni
sawa na ruhusa ya kucheza.
Watson alisema kilichotokea ni kati
ya Villa, mchezaji na huko alikosajiliwa ni baina yao na hakuna kinachomzuia
asisajiliwe.
“Kwa mazingira yaliyopo, hakuna
kipengele chochote ambacho kinamzuia mchezaji mwenye ruhusa maalum kuhamishwa
hivyo tumetoa ITC na hakuna ambacho kingemzuia Okwi kwenda kule anakotaka,”
alimalizia Watson.
BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA MAHOJIANO YA EDGAR WATSON.
Haya Bana, mi huwa nawakumbusha kuwa Tusitumie nguvu kubwa kutafasiri sheria wakati SISI sio Wanasheria. Hanspope alijiapiza kuwa Okwi hachezi yanga, alishawahi jiapiza Kwa Ngasa na hivyo kuwahadaa wanachama. Tatizo lipo kwenye taarifa ya kwanza iliyotolewa kuwa OKwi amesaini Villa kwa miezi sita. Haikutafasiriwa vizuri na sote tukaamini bila kufanya utafiti, Kumbe "Provisional" si Sawa na "Loan" na hicho ndicho kimetumiwa na akina Bin Kleb na Villa kumleta Okwi Tz.
ReplyDeleteWaandishi tuwe makini na kutoa habari vizuri na kuweka kwenye mizani ili tuwe na picha halizi,
Mambo ndo mambo na sasa kinaendelea kunuka kwa Rage, TFF wamekaa kimya ila angekuwa kaka yangu Angetile yeye Fasta kama anaona ukweli basi angetoa jibu lakini akina wamb.... mhhh.
Kuna muandishi aliwahi kusema kitu kuhusu hili la Okwi sijui ni Salehe Ally. Sinema inaendelea.
mm nimehamia lipuli simba nimehama
ReplyDeleteHapo juu mchangiaji wa kwanza, umeandika vzuri bt umekosea sehemu moja kumsifia mvurugaji, mwenye uwezo mdogo Angetile Osiah. Jifikirie mara mbili
ReplyDelete