Cristiano Ronaldo au Franck Ribery oyote anaweza ksuhinda tuzo ya Ballon d'Or, Zlatan Ibrahimovic haihitaji tuzo hiyo.
Mshambuliaji huyo wa Sweden amekuwa kwenye fomu nzuri sana msimu huu na klabu yake ya Paris St Germain, akifunga mabao nane katika Champions League - sawa na Cristiano Ronaldo.
Ronaldo anaonekana kupewa nafasi kubwa kushinda tuzo hiyo ya Fifa-Ballon d'Or baada ya hat trick yake katika ushindi wa Ureno dhidi ya Sweden wiki iliyopita na hivyo kuiwezesha nchi yake kufuzu kushiriki michuano ijao ya dunia.
Winga wa Ufaransa Ribery aliisaidia Bayern Munich kushinda makombe matatu msimu uliopita na alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kutwaa mwanzoni.
"Sihitaji Ballon d'Or kujua kwamba mimi ni bora," alisema Ibrahimovic, ambaye pia amesaidia timu yake ya PSG jana usiku kuvuka hatua ya makundi.
"Hii tuzo ina maana kubwa kwa wachezaji wengine."
Hakuna msweden aliywahi kushinda Ballon d'Or au mchezaji bora wa mwaka wa FIFA lakini hilo jambo halimkoseshi usingizi hata kidogo Cadabra.
"Sio kitu ambacho nakifikiria sana na sio kitu ambacho kina umuhimu kwangu," alisema.
No comments:
Post a Comment