Dilunga amesaini mkataba wa kuwatumikia wanajangwani hao kwa muda wa miaka mitatu akitokea Ruvu Shooting ya Pwani alipokuwa akichezea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Brandts alipokuwa kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Jumatatu kwenye Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama, Dar alisema, amefurahishwa na usajili wa timu hiyo na kudai kuwa nafasi ya kiungo itakuwa imara zaidi kutokana na ujio wa Dilunga.
“Yanga siku zote inahitaji wachezaji wazuri, kila mchezaji mzuri tungependa kuwa naye, wachezaji wote waliosajiliwa nawafahamu vizuri naamini wataisaidia timu katika mzunguko wa pili.
“Lengo letu ni kuhakikisha timu inakuwa imara katika mzunguko wa pili ikiwa ni pamoja na kujiandaa na michuano ya klabu bingwa kwahiyo sina wasi wasi naye naamini kuja kwake hapa ni mchango mkubwa sana kwetu” alisema Brandts.
Alimalizia kwa kusema, anamsubiri mchezaji huyo amuone katika mazoezi baada ya kurudi katika timu ya taifa ya Bara, Kili Stars ili aweze kuuona uwezo wake zaidi.
No comments:
Post a Comment