Search This Blog

Wednesday, November 20, 2013

MJADALA: SABABU ZA RAGE KUSIMAMISHWA SIMBA ZAFAHAMIKA, NINI MAONI YAKO WEWE MDAU




Jana uongozi wa klabu ya Simba ulitangaza kumsimamisha mwenyekiti wake Ismail Aden Rage.
Maamuzi hayo yalitokana na kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hapo juzi,
Hizi ni Miongoni mwa sababu zilizotolewa kwenye mkutano wa waandishi wa habari zilizopelekea kusimamishwa kwa Mheshimiwa Rage.

Mkataba na AZAM  TV

Rage alisaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya kipindi ya cha Simba TV bila kuishirikisha kamati ya utendaji.
Wakati Rage anasaini mkataba na Azam TV tayari klabu ya Simba ilikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho kuingia mkataba na kampuni ya ZUKU kwa ajili kipindi cha Simba TV uliokuwa na thamani ya dola za kimarekani 300,000 kwa mwaka.

Kampuni ya ZUKU ilipokuwa kwenye majadiliano na viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga jijini Nairobi, kwenye mkutano huo Simba iliwakilishwa na Mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph Itang’are maarufu kama mzee Kinesi pamoja na mwanachama Evans Aveva wakati Yanga iliwakilishwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga na Francis Kifukwe,viongozi hao Simba Ghafla walisikia Rage kasaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya Simba TV.

Sakata la uhamisho wa Emmaanuel Okwi.
Mheshimiwa Rage ndiye aliyesimamia uhamisho wa mchezaji Okwi on CREDIT bila kuishirikisha kamati ya utendaji,matokeo yake klabu hiyo mpaka leo imeshindwa kupata pesa ya uhamisho wa mchezaji huyo.

.
Kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji.

Sababu nyingine iliyoelezwa ni kitendo chake cha kushindwa kuitisha vikao vya kamati ya utendaji, Kuendesha klabu na kufanya maamuzi binafsi bila ya kushirikisha kamati hiyo ya utendaji ambayo ilichaguliwa na wanachama

Strategic plan ( Mpango mkakati )
Hivi karibuni klabu ya Simba ilizindua mchakato wa kutengeneza mpango mkakati (Strategic Plan) lakini cha kushangaza mwenyekiti amekuwa hataki kuona mpango huo ukifanikiwa.

Mkutano mkuu wa katiba

Kushindwa kuitisha mkutano wa marekebisho ya katiba,kuchukua maamuzi binafsi ya kuhairisha mkutano maalumu wa katiba uliotakiwa kufanyika Novemba, mwaka huu.

18 comments:

  1. Wakati Yanga wanagomea mkataba wa Azam TV, kwa kuwa walikuwa na majadiliano na Kampuni nyingine, waandishi wamebeza sana Yanga, na kuwaona ni wapuuzi. Sasa limeiibuka tena kuwa Rage alikurupuka tu Kusaini kwa maslahi yake binafsi.

    Vitu huwa vinakwenda vizuri kama kuna Ushindani Sawia yaani Wazabuni washindanishwe. watanzania bana, tukachukulia AZAM TV kama Mana iliyoshuka toka Mbinguni na sio haki yetu kuchagua Tule nini na kipi kinatufaa. Kwa ushawishi wa kuwatumia Thimba na timu zingine ambazo milioni mia moja za fedha za kitanzania ni nyingi kwao, mkataba kwa miaka mitatu ukasainiwa kwa kupiga kula.

    Kuna watu huwa wanaandika bila ufahamu na wanajifanya kuchambua sharia wakati wao si wanasheria. Haya Rage Huyooo anakuja na atatumia watu wenye njaaa na maswaiba wake na kupindua mpango wa mzima wa Kumsimamisha nahisi Vurugu kubwa itakuwepo Msimbazi.

    Huwezi kuandaa wala kusimamia wala kuthubutu kutoa kipaumbele kwa mpango mkakati kama wewe mwenyewe Haupo kimikakati ya chanya kawa ajili ya Klabu. Rage hata Tabora hawamtaki, sasa Thimba atafanya nini pale zaidi ya porojo na Kuwa mbele kila sehemu inayohusu fedha ndo utamuona.

    Kusainisha wachezaji yupo, kuuza wachezaji yupo, kusaini mikataba yupo na inawezekana hata Mgawo wa mechi kama ya mapacha wetu huwa yupo, mhazini hana sehemu pale ni yeye tu.

    Hao ndio viongozi wetu, Utaambiwa Thimba ina mpango mzuri wa Vijana, hebu waambie watoe Mpango wao wa miaka miwili, hutaona andiko lolote lile. Juhudi binafsi za watu Fulani na za Mdogowangu Suleiman Matola wanazibebea bango.

    Mimi ningeshauri hivi, Wamsubiri aje wamlazimishe aitishe kikakao cha dharura na wampige chini kwenye kikao hicho, vingenevyo nahofia vurugu.

    THIMBA THOMENI MAKALA YA MWINA KADUGUDA HUWA ANAELEZA YOTE HAYA..... CHOTENI HEKIMA ZAKE KWA MAANDISHI NA MTUMIE AKILI ZENU KUAMUA YALIYO BORA.


    MUNGU TUOKOE WATANZANIA NA TUONDOLEE HAWA VIONGOZI UCHWARA ILI VIPAJI VYA MPIRA ULIVYOTUPATIA TUVITUMIE VIZURI NA KUTUIINUA KIUCHUMI NA KIJAMII.

    ReplyDelete
    Replies
    1. UNACHANGANYA MPIRA NA SIASA soma habari kwanza hapo juu kabla hujaandika upuuzi.Mambo ya kupinduana yalishapitwa na wakati huwezi kuwa viongozi wote wa juu wanakaimu, mwenyekiti anakaimu na makamu mwenyekiti anakaimu isitoshe Kibadeni na Julio hawana kosa lolote Simba kuwa ya nne sio kitu cha ajabu Man United ya tano England sembuse Simba??Kinesi na kundi lake wamechemka.

      Delete
  2. Mimi naona ni sawa Kusimamishwa kwake zaidi ya hayo hapo juu wamesahau kuhusu usajili wa Twite alisema watamkamata hadi leo hii kimya pia muda mwingi anatumia bungeni zaidi ya hayo RAGE ANAOGOPA HATANYIMWA UBUNGE MWAKA 2015 AKIFANYA KINYUME NA MABOSI WAKE WA CHAMA AMBAO NI WADHAMINI WA YANGA, HIVYO ANAFANYA HAYO KULINDA UBUNGE, HERI AONDOKE SIMBA AKAENDELEE NA SIASA ATUACHIE SIMBA YETU.

    ReplyDelete
  3. Aendelee na Siasa soka limemshinda hawezi

    ReplyDelete
  4. ila simba walivyo fanya sio fresh kumsajili coarch na kuntimua kabka ajamiza msimu unategemea mafanikio yataPatikana vp.

    ReplyDelete
  5. shaffih hii taarifa yako mbona inaonyesha haina mashiko mbona yako huyasemi unachojua ni kumchana rage tu!!! Hivi taarifa yako na TFF mmlimalizana vipi mbona hukutupa hitimisho umehamia tena kwa Rage!!!

    ReplyDelete
  6. Tatizo la club zetu ndio hilo. Utaratibu na mipango endelevu viongozi wanopenda maslahi yao binafsi ndio wanakwamishaga maendeleo ya vilab vyetu. Nafikiri Rage anasumbuliwa na 2015 ya jimbo lake kwa sasa, inabidi achague moja siasa kw ajli ya wananchi au mpira kwa ajili ya wananchi. Binafsi nilimkubali wakati anaingia simba sasa nikikumbuka la Okwi napata kichefuchefu kumbe ndiye aliyetoa mchezaji kwa mkopo? cjui la Kapombe nalo limekaa vipi??? Undeni kamati ya maendeleo ya mpira iliyo huru iatakyoshirikiana na kamati ya ufundi. Juzi usajili wa wachezaji waili unafanyikia nyumbani kwa mwenyekiti inashangaza sana hivi ofisi ya club ya simba iko wapi najengo tunalo?
    makocha wa kigeni wanasain mikataba popote pale kuwatishia ni timu kubwa wapeleke kariakoo wazoee mapema mazingira wakati wanaanza. jengo lina ghorofa kibao, lakini wachezaji wanaishi ofisini mbona timu ya sigara iliishi chang'ombe pale. Simba mnashindwa nini. mmepangisha jengo hela hailiendelezi jengo. Basi uzeni kariakoo mkaendeleze Bunju hela zinatosha kuweka kiwanja na maendeleo ya baadae. kama mjini kati hailipi. NIMESHACHOKA BORA SILAHA ZICHASIWE KWENYE MKUTANO WENU MKUU. Kanjanja nyingi mnazo viongozi
    Unachaguliwa kwa sera za kujenga uwanja ukiulizwa unatukana wanachama na wapenzi eti " mna akili timamu kweli? uwanja nadani ya miaka miwili mitatu?? wakati serikari imejenga baada ya miaka hamsini?" ulifikiri utakaa madarakani kwa miaka 50 kama ccm?
    Wapeni wasomi nafasi tuwekee maendeleo ya kweli wenye uchungu na maendeleo ya kizazi kijacho. Wote longolongo tu...

    ReplyDelete
  7. Simba ina njia nyingi sana za kuongeza kipato ambazo zinaweza kusaidia kujenga kiwanja.
    Tafuteni wasomi wawaelekeze nini cha kufanya.
    Tunaendeshana kiswahili sana.
    Madudu mangapi kayafanya Rage anaangaliwa tu, leo mnashangaa la kusainisha wachezaji nyumbani kwake na hela keshi. Hahahahahahaaaaa

    Tunapochagua viongozi tuwe tunaangalia na asili zao

    Mfano; Mchaga mpe duka, msukuma mpe kilimo na ufugaji, mkurya mwanajeshi msomali anakazi zake pia sio uongozi wala kujenga nchi....hahahaha

    ReplyDelete
  8. ukijiona unapenda mpira pori wa tz ujue haupo sawa kiakili

    ReplyDelete
  9. Naipenda sana Simba lakini nilistaafu uanachama na ushabiki pale tu Rage alipotutanganya kuhusu Yondani.
    Ntarudi akiondoka. katika kipindi chake cha uongozi ni makocha wangapi wameingia na kutoka? Makocha wangapi wanaidai Simba.

    ReplyDelete
  10. Nachukia watu wenye siasa za mpira.mmojawapo ni Rage,huwa anasema vitu ambavyo anasahau kama yeye ndie alisema.vipi kuhusu uwanja huko bunju?watu wapo kwa maslahi binafsi ,they dont care about football kwa upande wangu walichofanya hao viongozi ni sawa .Lakini pia isijekuwa na hayo waliyoyafanya ni kwa maslahi binafsi ya mtu au watu fulani.Mzunguko unakuwa ni ule ule.yawezekana hata wanaofanya hivyo nao walishapinduliwa nao wanatafuta njia za kurudia.kuna haja ya kubadilisha mfumo mzima wa soka la Bongo nje ya hapo tutaendelea kuona madudu tu.Najaribu kujiuliza hata hao wachezaji waliosajiliwa na simba je ni mapendekezo ya kamati ya ufundi au mtu kajisikia ili apate sifa kuwa amesajili.

    ReplyDelete
  11. Kama kikao kilichomsimamisha Rage hakina mamlaka hayo watakuwa wanafanya kama walivyofanya mwanzo na why wafanye mkutano wakati Rage hayupo? Hiyo ina maana viongozi waliopo wanamuogopa jamaa kwa kuwa ni talkative, mkorofi na zaidi sheria anazijua sana.

    ReplyDelete
  12. mpira wa bongo banna kama sarakasi

    ReplyDelete
  13. Nina wasiwasi na Mwandishi wa Makala hii... Kakurupuka.

    ReplyDelete
  14. nakumbuka shaffih uliponda utaratibu wa kuwasainisha wachezaji kwa kuweka minoti mbele yao,sasa umeona ya rage? unakumbuka yondani kinda na minoti yake kwa yanga na yondani mkubwa kubaki simba?, simba tulishapotea siku nyingi sana msomali kazi zake sote tunazijua fitna, bisckuti na maji anaishi miezi 6 na minoti ya simba ndo kabisaaa hatumtowi..... shaffih naomba criterial za kumchagua mchezaji bora wa dunia zinakuwa zipi na ninani wanaochagua? inamaana hadi kufikia tarehe 15/11/013 mess alikuwa ameshinda ndo maana fifa wanaona aibu hadi kuongeza muda ili ronado ashinde? ronado watu hawampendi kwa personality behavior zake n exagrations anapoguswa mchezoni kama vile kaumizwa sana ili kumchiti mwamuzi mpinzani wake hana hizo personality behavior za kujiskia na attention seeking behavior alizonazo ronado, lakini uwezo anao....... by

    ReplyDelete
  15. hahahaaa amakweli nyani haoni......ww shabik wa mess inamaana huyaoni maovu yakee..au ndo ukipenda ua na boga lakee.

    ReplyDelete
  16. Fanya kazI shaffie usiogope kelele za chura.... mti wenye matunda kawaida hukosi kupigwa mawe

    ReplyDelete