Na Waandishi Wetu,
Shinyanga na Moshi
Mashabiki wa Simba wameendelea kutangaza ubabe kwa mashabiki
wa Yanga baada ya kuwashinda kwenye mechi za mashabiki hao zilizochezwa jana
kwenye miji ya Shinyanga na Moshi kupitia bonanza la Nani Mtani Jembe,
lililoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambapo pote Simba walishinda. Hata
hivyo Yanga waliweza kujipoza huko Moshi kwa kupata ushindi mnono kwenye michezo
ya kufukuza kuku, kupiga penati kwenye goli dogo na kupiga danadana.
Shinyanga bonanza lilianza mwendo wa saa 9 alasiri
ukitangulia mchezo wa kufukuza kuku ulitangulia ambapo mashabiki wa Simba
waliibuka washindi dhidi ya Yanga. Baada ya hapo ulifuata mchezo wa kukimbia
ukiwa umevaa gunia ambapo Charles Shija wa Simba aliibuka kinara kwa mikimbio 2
dhidi ya 1 wa Yanga. Ulifuata mchezo wa kuvuta kamba wanaume ambapo pia Simba
walishinda yanga 2-1.
Baada ya mchezo huo
kulifuata mechi kali sana kati ya mashabiki wa Simba wa soka wa mkoa wa Shinyanga
na mashabiki wa soka wa Yanga, ambapo katika mechi hiyo simba walipata penati kipindi
cha kwanza na mchezaji Iddi Mobi hakufanya ajizi na kukwamisha mpira wavuni.
Mpaka mapumziko Simba 1 Yanga 0, kipindi cha pili Yanga walikuja juu ili
wasawazishe lakini bahati haikuwa kwao na kujikuta wanapachikwa bao la pili
lililofungwa na Kulwa Mobi. Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na dakika 8
kabla ya kipenga cha mwisho walipata penati iliyotiwa nyavuni na Amani Rashid. hivyo mpaka filimbi ya mwisho Simba 2, Yanga
1.
Huko Moshi mashabiki wa Yanga walishinda mchezo wa kupiga
dana dana na kupiga penati kwenye goli dogo, kufukuza kuku. Kwenye mchezo wa
soka, mashabiki wa Simba walishinda kwa goli 2 – 1 na pia walishinda kuvuta
kamba. Bonanza hilo lilipambwa na Malindi Band, Msanii maarufu wa bongo flava wa
Moshi ajulikanae kama Majirani pamoja na wasanii wa kundi la Black Warriors.
Kupitia kampeni ya Nani Mtani Jembe, bia ya Kilimanjaro
Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi
milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi
milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa
mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni
hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu
nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka
kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la
Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni
kununua bia ya Kilimanjaro ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona
namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani
na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha
anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa
amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki
aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 10,000
kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa
amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.
Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha
zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa
shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.
Mashabiki wa timu ya Yanga Shinyanga wakionyesha mbwembwezao kabla michezo haijaanza ktk uwanja wa Shycom Shinyanga
ushoto ni meneja mauzo wa Shinyanga,Tabora na Katavi Bw
Robert Kazinza akikabidhi jezi kwa viongozi wa vilabu vya
mashabiki wa Simba na Yanga wa Shinyanga ktk bonanza
lililofanyika kwenye viwanja vya Shycom jana ktk kampeni za
NANI MTANI JEMBE kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Timu za mashabiki wa Yanga na Simba zikimenyana uwanjani
ambapo Simba waliibuka washindi kwa bao 2-1. Ni ktk bonanza
la kampeni ya NANI MTANI JEMBE lililofanyika ktk viwanja vya
Shycom Manispaa ya Shinyanga jana.
No comments:
Post a Comment