Na
Mwandishi Wetu
Mashabiki wa Simba na Yanga kwenye miji ya
Shinyanga na Moshi watapambana vikali na kuburudika katika michezo mbalimbali
kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Shycom mjini Shinyanga na uwanja wa CCM
Mkoa mjini Moshi siku ya Jumapili wikendi hii.
Mratibu wa mabonanza hayo Lawrence Andrew, amesema
kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta
kamba, na pia mpira wa mezani maarufu kama fussball itapamba mabonanza hayo.
Burudani mbalimbali pia zitapamba bonanza litakalofanyika Moshi zikiwemo
burudani ya muziki kutoka bendi ya Malindi Band pamoja na wasanii mbalimbali wa
muziki wa kizazi kipya wa mkoani Kilimanjaro.
Kwa Mkoa wa Shinyanga bendi maarufu mkoani
humo ya TMA Band itatoa burudani kabambe kwa mashabiki watakaojumuika kushiriki
bonanza hilo.
Andrew pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo
mbalimbali ya kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na
gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba mabonanza hayo
ambayo yatafanyika katika mikoa hiyo kwa mara ya kwanza kupitia Nani Mtani
Jembe. Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao
kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na
utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha
mapenzi kwa timu zao.
Mabonanza hayo yanalotarajiwa kuanza saa
tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo ilizinduliwa
Oktoba 2 na inafanyika nchi nzima
ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni
hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga
kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila
timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe
alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki
kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi
zaidi ya timu nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe
alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa
shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga
anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye
kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia ya
Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua
simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la
timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye
namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo,
atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki
aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 10,000
kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa
amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.
Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa
fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya
mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment