Search This Blog

Monday, November 18, 2013

KWANINI TOTENHAM INA UKAME MKUBWA WA KUFUNGA MABAO KATIKA PREMIER LEAGUE?

soldad
Wakati ligi kuu ya England ikiwa ipo kwenye mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa za mwisho mwaka huu, kuna habari nzuri na mbaya kwa timu ya Tottenham Hotspur: Michezo 11 wameshacheza, Spurs wana pengo la pointi 1 kuingia Top 4, na pointi 5 kutoka kwenye uongozi wa ligi pamoja kuleta wachezaji saba wapya ndani ya kikosi hicho. 
Hii inatokana na kuwa na kikosi kilicho bora kwenye ulinzi ambacho, ukitoa kipindi cha pili dhidi ya West Ham, kimeruhusu mabao 3 katika vipindi 21 ya mechi za soka - kwa maana ya mabao 3 kwa wastani wa mechi 10.5.

Kwa bahati mbaya, taarifa mbaya kwa Spurs ni kwamba mpaka kufikia kwenye mechi ya 11 wamefunga mabao 9  tu. Timu pekee ya premier league zilizofunga mabao machache kuliko Spurs zipo katika ukanda wa kushuka daraja. Spurs wamefunga mabao sawa na timu zilizopanda daraja kama Cardiff City na Hull na kikosi cha Sam Allardyce West Ham. Kuongeza chumvi kwenye kidonda, Stoke City wamewazidi kwa goli moja la kufunga na sihitaji kukuambia timu hizi zote vikosi vyao vinavyoanza vina thamani ya wachezaji wawili au watatu wa Spurs.  

Lakini kwanini Spurs wamekuwa wabovu kwenye ushambuliaji? Kuna sababu kuu tatu, ambazo zote zinatabirika; kwanza, Spurs utumiaji wa mawinga umesababisha sehemu ya kati kucheza kwa kutokushambulia, Pili, Spurs wanakosa ubunifu katikati ya dimba. Tatu, Spurs hawana mshambuliaji mwenye uwezo wa kujitengenezea mwenyewe mara kwa mara. 


Mfumo wa kiufundi wa Spurs msimu huu
Changamoto ya kwanza kabisa, Spurs msimu huu wameamua kutumia mfumo ambao aidha unaweza kuelezea kama  4-2-3-1 au 4-2-1-3 ambao ndani yake wanatumia kiungo mchezeshaji kucheza pembeni ya mshambuliaji pekee. Kawaida hawa washambuliaji wa pembeni wakicheza kwenye nafasi tofauti na mguu wanaotumia zaidi ama wenye nguvu zaidi, kwa maana hupokea mpira pembeni kabla ya kuingia ndani katika kuelekea kwenye upande ambao mguu wanaotumia wenye nguvu. Unapounganisha wachezaji wa aina hii pamoja na kiungo mchezeshaji ambaye anapenda kwenda mbele zaidi katika kujaribu kuamua mechi, basi kunakuwa na kunaibana sehemu ya kati, jambo ambalo linapelekea kupunguza kasi ya wachezaji wa kushambulia na hivyo kufanya mashambulizi ya timu kuwa rahisi kuzuilika. Yoyote aliyeangalia utumiaji wa Roberto Mancini wa  mfumo wa 4-2-3-1 akiwa na City katika miaka ya karibuni au siku za mwisho za Di Matteo alipotumia 4-2-3-1 ndani ya Chelsea msimu uliopita ungeweza kutabiri au kuona tatizo hili. Na kama mfumo huu ulifeli wakati ukiwa na wachezaji kama Samir Nasri, Yaya Toure na David Silva au Juan Mata, Oscar, na Eden Hazard, basi haiwezi kushangaza kuona ikifeli kwa wachezaji kama Gylfi Sigurdsson, Lewis Holtby, na Andros Townsend.

Timu ambazo zinatumia mfumo wa 4-2-3-1 huwa zinategemea hudua kutuma mshambuliaji wa pili ambaye hucheza kwenye shimo kama Thomas Muller au Tony Kroos pale Munich au Mesut Ozil alipokuwa Real Madrid. Wachezaji hawa hucheza namba 10 hurudi nyuma kidogo katika kiungo na kuunda mfumo wa utatu wa safu ya kiungo au kwenda kwenye aidha winga ya kushoto au kulia kupokea mpira, wakibadilishana nafasi na mawinga wenyewe. Mchezo hutengeneza nafasi katika dimba la kati na kufanya timu isitabirike kwenye mashambulizi, lakini vitu hivi Spurs wanakosa kutoka na uchezaji wa Christian Eriksen na Lewis Holtby. 

Mbinu mbadala za kiufundi 
Mfumo mzuri utakaowafaa Spurs kutoka na aina ya wachezaji walionao ni 4-2-3-1 ambao hutumia winga asilia na mmoja aisye wa asili: Lennon akicheza kulia huku Chadli au Sigurdsson akicheza kushoto. Pia Townsed anaweza kucheza kushoto huku Lamela akicheza kulia ni chaguo lingine linaloweza kufaa zaidi.  Kwa kumtumia winga halisi katika upande mmoja wa mfumo, inasaidia kufungua nafasi zaidi katikati mwa tatu ya kushambulia kitu ambacho kinaweza kumpa Eriksen au Holtby nafasi zaidi na muda kwenye mpira, hivyo kuhirahisha kucheza kwao dhidi ya safu ya ulinzi iliyojifunga.

Kumiliki sana mpira bila kuwa na cheche. 
Tatizo lingine la Spurs wamekuwa wakimiliki sana mpira bila kutengeneza nafasi za kushinda. Spurs wana wachezaji wengi wenye ubora wa kiufundi lakini wanakosa wachezaji wabunifu  (Tom Huddlestone alikuwa bora kiufundi Modric akicheza kama kiungo mbunifu.) Holtby, Townsend, Sigurdsson, Paulinho, na Chadli wote wameshaonyesha ubora wao kwenye mpira mwaka huu, kitu ambacho hawajaonyesha kuwa na ubunifu wa hali ya juu kama ilivyokuwa kwa Modric. Spurs wana wachezaji watatu ambao wameshaonyesha kuwa na uwezo japo sio mkubwa wa kuwa wabuniful; Christian Eriksen (katika assist yake ya kwanza dhidi ya Norwich), Erik Lamela ( assist yake dhidi ya Cardiff), na Roberto Soldado.
Kati ya watatu hawa ni mmoja tu Soldado, ambaye amekuwa akipewa muda mwingi wa kucheza na AVB, lakini ameshindwa kucheza vizuri ndani ya mfumo unaoonyesha sana mapungufu yake kuliko ubora wake. Wakati huo huo Eriksen alikuwa ameanza kuonyesha  ubora wake lakini amerudishwa kukaa benchi kama ilivyo kwa Lamela ambaye hapati nafasi ya kutosha. 
Kwa maana hiyo Spurs wanahitaji kuwatumia vizuri wachezaji katika mfumo ulio sawa ili kuondokana na tatizo la kutotengeneza vizuri nafasi na kuzitumia

Tatizo la kushambulia?
Tatizo la tatu, Spurs wanakosa mshambuliaji ambaye anaweza kujitengenezea nafasi mwenyewe mara kwa mara. Soldado sio aina ya mchezaji ambaye anapenda kupokea mpira huku mgongo wake ukigeukia nyuma ya goliau kujaribu kuwatoka mabeki mara anapopokea mpira, Soladado yupo kama mhispania mwenzie Fernando Torres, anafanya kazi nzuri zaidi akiwa ameliangalia lango, akitumia uwepesi wake na ufundi kutengeneza nafasi ya kufunga.

Torres anafunga mabao akiokea mpira kwenye njia au kukimbizana na mabeki, Soldado anafunga zaidi kwa ufundi wake wa kuchezea mpira ndani ya box, akitumia moves zenye akili, pamoja na kufunga kwa mguso wa kwanza au mpira wa mpira kutoka kwa mpigaji pasi ya mwisho. Kwa maana hiyo inaonekana kwamba Soldado anahitaji kuletewa krosi jambo ambalo linashindikana kwa mfumo wa kuchezesha mawinga wanatakiwa na mfumo na mpira ya kupitishia inakuwa tatizo kwa sababu ya ugumu wa ukuta wa mabeki waliojipanga vizuri. Kwa maneno mengine kufeli kwa Spurs kwenye upangaji wa kikosi chenye mawinga wasiokuwa wabunifu kunailetea matatizo timu. 
 Kitu ambacho AVB anapaswa kufanya ni kumchezesha viungo sahihi kulingana na mfumo wa timu.   
Ikiwa Spurs wataweza kutatua tatizo, kuna kila sababu ya kufikiria kwamba wanaweza kushindania kombe au kumaliza katika top 4. Safu yao ya ulinzi ndio nzuri zaidi katika Premier League. Lakini mpaka timu itakapoanza kufunga mabao basi wataendelea kucheza  kwa kupigania kushiriki kwenye Europa League.

No comments:

Post a Comment