Michuano mikongwe barani Afrika ya kombe la Challenge kwa nchi za ukanda wa Afrika ya mashariki na kati Cecafa inatarajiwa kuanza hapo kesho kwenye viwanja vya Nyayo jijini Nairobi na Machakos nchini Kenya, kwa jumla ya nchi kumi na mbili kuwania taji hilo.
Wenyeji Harambee starz ya Kenya, machampioni watetezi wa taji Uganda The Creans, Walya Antelope ya Ethiopia, Ocean boyz wa Somalia, Zanzibar Heroes ya Tanzania visiwani, Kilimanjaro starz ya Tanzania bara, Sudani ya kusini na ile ya Kaskazini, zinamenyanya.
Nyingine ni pamoja na Eritrea, Intamba Murugamba ya Burundi, Amavubi ya Rwanda, na waalikwa kwenye michuano hiyo Askari wa Chipolopolo toka nchini Zambia, zinawania taji hilo.
Timu zimegawanywa kwenye makundi ya A,B na C, ambapo kundi la A wapo Zanzibar Heroes ya Zanzibar, Walya Antelope ya Ethiopia, Sudan ya Kusini, na wenyeji Harambee starz ya Kenya, watasaka nafasi mbili za juu kucheza robo fainali.
Kundi la pili, lina timu za Kilimanjaro starz ya Tanzania bara, Chipolopolo ya Zambia, Intamba Murugamba ya Burundi, na mabaharia wa Somalia.
Kundi la tatu ambalo ni la C, lina timu za Amavubi ya Rwanda, machampioni watetezi wa taji Uganda the Creans, Sudan ya Kaskazini na mabaharia a Somalia.
Mechi za ufunguzi za michuano hiyo zinatarajiwa kuanza kesho kwa michezo baina ya wenyeji Harambee starz ya Kenya dhidi ya Walya Antelope ya Ethiopia kwenye uwanja wa Nyayo, lakini kabla utapigwa mchezo baina ya Zanzibar Heroes dhidi ya Sudani ya kusini.
No comments:
Post a Comment