Search This Blog

Sunday, November 17, 2013

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR (SMZ) IMEANDAA MASHINDANO YA MICHEZO 17 KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

Frank Mvungi - Maelezo

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeandaa mashindano ya michezo 17 kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi hayo itakayofikia kilele januari 12,2014 ambayo ni siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari , Utamaduni,Utalii na Michezo  Zanzibar Mh. Said Ali mbaruk wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya michezo ya kuadhimisha mapinduzi hayo.

Mh. Said Ali  Mbaruk amesema kuwa  katika kuadhimisha mapinduzi hayo michezo mbalimbali itafanyika ikiwemo mpira wa miguu,riadha,volleyball,Table tenis na mazoezi ya viungo.

Akifafanua zaidi  Alisema michezo hiyo pia itawahusisha watu wenye ulemavu ambapo kwa kushirikiana na Kamisheni ya utalii michezo mingine itakayofanyika ni  karata,bao,squash na kuogelea .

Akieleza zaidi  Mh. Said Ali Mbaruk aisema kuwa katika michezo hiyo kutakuwa na timu zaZanziba,Tanzania bara,Afrika Mashariki,ambapo mashindano hayo yanapata hadhi ya kimataifa.

Pia alizitaja timu zinazotarajiwa kushiriki kuwa ni Azam FC,Simba, Yanga,Mbeya city kwa upande wa Tanzania bara, baadhi ya timu toka Zanzibar ni chuoni,Pemba combine na Unguja combine.

Katika maadhimisho hayo mechi zote zitatangazwa moja kwa moja kupitia ZBC TV,kwa kushirikiana na Azam TV.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Said Ali Mbaruk akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu michezo mbalimbali itakayofanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayo adhimishwa Mwezi January 2014,wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene.

 

No comments:

Post a Comment