Search This Blog

Monday, November 18, 2013

CAMEROON,IVOY COAST NA NIGERIA ZAKATA TIKETI YA BRAZIL.

 
Huku wawakilishi watatu wa bara la Afrika kwenye fainali za FIFA za kombe la dunia wakiwa tayari wamefahamika,timu hizo ni Nigeria, Côte d'Ivoire na Cameroon ambazo pia zilishiriki fainali za 2010 zilizofanyika Afrika Kusini.
Huku Ghana ikiwa kwenye mazingira mazuri ya kufuzu baada ya kuifunga  Egypt mabao 6-1 kwenye mchezo wa kwanza na Algeria kama itafanikiwa kupindua matokeo ya kipigo cha mabao 3-2 toka kwa Burkina Faso basi huenda tukazishuhudia timu zote zilizoliwakirisha Bara la Afrika kwenye fainali za 2010 nchini Afrka Kusini.



Mabao ya washambuliaji Victor Moses (20 PEN) na Victor Obinna (82) yalitosha kuwapatia Super Eagles ushindi wa mabao 2-0 na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 baada ya kuifunga Ethiopia  mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza.

 Keshi ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza mwafrika kuziongoza timu mbili tofauti kufuzu fainali za kombe la Dunia,aliiongoza Togo kufuzu za nchini Ujerumani mwaka 2006.

Kocha wa Ethiopia  Sewnet Bishaw  amemsifia Keshi baada ya kipigo. "Keshi anajua namna ya kuiandaa timu. Watafika mbali kwenye kombe la Dunia."


kwingineko huko jijini  Casablanca, Senegal ilifungana bao 1:1 na Ivory Coast,Moussa Sow aliipatia Senegal bao la kuongoza kwa mkwaju wa Penati baada ya Didier Drogba kumwangusha Sadio Mane  huku Salomon Kalou akiisawazishia Ivory Coast kwenye dakika za majeruhi,matokeo ambayo yaliwavusha Tembo kwa jumla ya mabao 4-2.


Huko Yaounde, Cameroon  ilifanikiwa kufuzu baada ya kuitandika Tunisia mabao 4-1.

Mabao ya Cameroon yalifungwa na Pierre Webo,Benjamin Moudandjo na kiungo mkongwe Jean Makoun aliyefunga mabao 2 huku Akaichia akiifungia Tunisia bao la kufutia machozi..


3 comments:

  1. Tulicheza na camerron kwa kuiiza lakini wenzetu walikuwa wanaanisha. Tutakuwa wasanii mpaka lini

    ReplyDelete
  2. Hongera cameroon kwani sie tulijaribu nyie mkafanya kweli . Tunahitaji fikra pevu kufika mlikofika nyie lakini kwa kujazaq wachezaji kutoka nje kwenye vilabu vyetu nadhani itatuchukua miaka dahari kuwasogelea

    ReplyDelete