Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa mara nyingine imeendelea kudhamini mashindano ya mpira wa miguu ya kila mwaka ya Mpinga cup Yenye lengo la kusaidia kutoa elimu kwa waendesha pikipiki ili kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani.
Akiongea
na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya ya shilingi
milioni 5 kwaajili ya kuendesha mashindano hayo Meneja uhusiano wa Airtel
Tanzania Jackson Mmbando alisema kampuni yake bado inaendelea na harakati za
kuhakikisha inasaidiana na jeshi la usalama barabarani na wadau wengine wote
ili kuhakikisha inapunguza idadi ya ajali barabarani kupitia njia yoyote
ikiwemo michezo kama hii ya MPINGA CUP
“Airtel
tumeamua kuyapiga tafu mashindano haya ya Mpinga cup kwa kuwa lengo lake ni
kutimiza dhamira ya kijamii ya kupunguza na kutokomeza ajali barabarani , fedha
hizi zitatumika kuendesha mashindano haya ya waendesha boda boda wa jijini Dar
es salaam ambapo pia kupitia nafasi hii ya kukutana katika michezo tutaweza
kutoa elimu ya uelewa wa usalama barabarani kwa lengo la kuwaokoa ndugu zetu na
jamaa katika ajali zinazoepukika” alisema Mmbando
Mbali na
Airtel kampuni ya Be forward nayo imejitokeza kudhamini mashindano hayo kwa
kutoa mipira 50 ili kuwezesha mshindano hayo yanayoshirikisha madereva wa piki
piki maarufu kama bodaboda.
Akipokea
msaada huo, Kamanda Msaidizi kikozi Usalama Barabara .Jehansen Kahatano
aliwashukuru Airtel na Be forward kwa udhamini wao na kubainisha kuwa,
mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisismko mkubwa kulinganisha na mwaka jana
kwa kuwa ytayari yamepata mashabiki wengi na kuteka hisia za kiushindani kwa
washiriki wa wilaya zote.
“ninawashukuru
sana Airtel Tanzania na kampuni ya Be forward kwa kutuunga mkono katika
harakati zetu za kusambaza uelewa kwa watumia bara bara wote kupitia mashindano
haya ya Mpinga Cup yanayoshirikisha waendesha bodaboda wa jijini dar es salaam,
tunajua kuwa mashindano yamekuwa na yatakuwa na mvuto sana mwaka huu kwa kuwa
tayari washiriki wote wamejipanga toka walipomaliza mashindano ya mwaka jana,
sasa naomba tu niwakumbushe kuwa isiwe ni kushindania kwenye mpira tu bali pia
tujiweke tayari kupokea elimu ya usalama barabarani ili tutimize pia lengo letu
la kupunguza ajali barabarani” alisisitiza ACP Kahatano
Mbali Airtel Kudhamini Mpinga Cup 2013 pia tunatumia
vyombo vya habari ambavyo ni wadau wetu kuhakikisha wananchi au wadau wasomaji
na watazamaji wa vyombo hivi wanapata habari za elimu hii ya usalama barabarani
ili kuhakikisha tunasaidia jamii kupunguza athari zinazotokana na kukatishwa
maisha kwa ghafla na kupoteza nguvu kazi ya taifa
Kamanda msaidizi wa kikosi cha usalama barabarani, ACP Jehansen Kahatano akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando iliyotolewa leo kwa dhumuni la kudhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa waendesha pikipiki maarufu kama Mpinga cup. Anayeshuhudia katikati ni Raisi wa Be forward Tanzania Bw. Hironori Yamakawa na Mkuu wa usalama barabarani kanda ya Dar es salaam ACP Amiri Konja (wakwanza kulia)
Kamanda msaidizi wa kikosi cha usalama barabarani, ACP Jehansen Kahatano (katikati) akipokea mipira itakayotumika kwenye mashindano ya Mpinga Cup. Anayekabidhi kushoto Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando pamoja na Raisi wa Be forward Tanzania Hironori Yamakawa. Katika makabidhiano hayo Airtel pia ilikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kudhamini mashindano hayo ya Mpinga Cup. Anaeshudia ni Mkuu wa usalama barabarani kanda ya Dar es salaam ACP Amiri Konja (wakwanza kulia)
No comments:
Post a Comment