Klabu ya Ahly ya Egypt imeshinda taji la nane la klabu bingwa Barani Afrika baada ya kuifunga Orlando Pirates ya Afrika Kusini mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa leo jijini Cairo.
Ahly, waliokuwa mabingwa watetezi
wameshinda kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa nchini
Afrika Kusini kumalizika kwa sare ya 1-1.
Mshambuliaji mkongwe Mohamed
Aboutrika aliipatia Ahly bao la kuongoza mnamo dakika ya 54 kabla ya Ahmed
Abdul Zaher hajaitimisha ushindi pale alipofunga bao la pili kunako dakika 78
kwa shuti lilimshinda kipa wa Pirates Senzo Meyiwa.
Binafsi sikubaliani na CAF fainali kuchezwa nyumbani na Ugenini.Fainali(Final)=Mwisho,yaani mnapokutana ndiyo mwisho.Uchaguliwe uwanja wa fainali mapema kabla ya kufahamu ni timu gani zitakuwa fainali,ichezwe fainali moja tu.Najua viongozi wa TFF mnasoma humu,peleka hilo wazo CAF Cairo.
ReplyDeleteDavid V